Ndoto ambazo nimekuwa nikiziota kwa muda mrefu sasa na kiukweli zinanitesa sana

Barikiwa sana Mtumishi, nimeyapokea na nitayafanyia kazi maandiko
 
Yaaani kama mm uwa naota tupo shule alafu tunakaribia kufanya mtihani na mtihani unafika nakuja gundua sjajiandaa kwa lolote,Yaan naanza kuangaika na cha kushangaza uwa nnaota nipo na jamaa mmoja tu yule yule,Yaani mpaka naogopa kumuuliza.
Wewe ya kwako na tafsiri ya mleta uzi upande wa shule ni sawa! Mara nyingi ndoto za kupimwa kiwango chako cha maisha kama kimepanda au kimekwama hutoka kwa Mungu! Shetani hana haja ya kukupima! Akupime kwa lipi? Yeye ni kukuangamiza! Ukiona mambo ya mitihani/darasani/wanafunzi/aina au namba ya wanafunzi inaonyesha ni kwa kiwango gani umekwama. Wewe unaonekana kati ya woote wa kiwango chako mmekwama wawili tu (yaani wewe na huyo jamaa). Wakati mwingine huo mkwamo umesababishwa na mambo ya wasoma nyota! Kuna watu wanasoma nyota (wana roho za utambuzi) na wakigundua huko vizuri basi ujifungamanisha na kujiambatanisha na wewe ili ukifanikiwa na wao wafanikiwe! Ujawahi kuona mtu anatoboa alafu bila sababu ya msingi anaenda anamchukua mtu baki na kumbeba mpaka naye anafanikiwa? Sasa wewe uenda huyo jamaa mnayefeli naye kakung'ang'ania na kukufungia liziki! Tumia damu ya Yesu ujitenganishe naye utaanza kufanikiwa Rwankomezi
 
Hizo ndoto za shuleni huwa watu wengi sana wanaota, hata mimi kuna kipindi nilikuwa naota ila sasa zimepotea
Hazina maana yoyote zaidi ya kumbukumbu za zamani kujirudia tu

 
Shukran kwa ufafanuzi
 
Shukran kwa maoni yako
 
Mi kinachonishangazaga kwenye ndoto ni unaota mnajuana na mtu kwenye ndoto kwa kipindi kirefu sana hata miaka 20 wakati hiyo ndoto usikute hata dakika kumi za kuiota hazifiki.Ndani ya dk chache za kuota ndoto unaota mmesoma na jamaa shule mpaka mkamaliza
 
Sio kila position unayolala mwili unakuwa comfotable nina maana kuwa kila mtu kuna style akilala mwili hukubali na haoti njozi mbaya. Ni brain yako hutengeneza scenario ili uondokane na hiyo position uliyolala ili uwe comfotable. Ni sawasawa na mkojo ukiubana sana lazima brain itengeneze mazingira ili uutoe likewise kwa wanaume huwezi kuretain sperms kwa muda mrefu ni lazima yatengenezwe mazingira ya kufanya tendo ili zitoke hii yote ni scientific perception na sio uchawi wala nini.
Ndoto huja kwa ajili ya body normalization ukiwa na stress au maumivu fulani kubalance mwili lazima uote. Kuna vitu vingine hata wanasayansi hawavijui ni kwa nini vinakuwa hivyo ndani ya mwili wa mwanadamu mfano jicho lako kiulinzi linajitegemea na once kama ingekuwa tofauti bila shaka vitu vinavyohusika na ulinzi wa mwili wako vingelishambulia jicho kama adui nk.nk. kuna mengi ya kujifunza bro.
 
Ndoto ni tafsri na ishara za mambo ya kiroho kwenye nyakati zote wakati uliopita, uliopo na ujao. Lakin si ndoto zote ni zakiroho. Msijikute wasomi wa kindezindezi mnatoboa mpaka chuo kikuu kwa d mbili, mkifika humu mnajikuta mnajua kila kitu....



Ndoto ya kwanza umeota unaporomoka kwenye mabonde huko, Hii tafsri yake ni kushuka kwenye ubora wako kwa nyanja yoyote ile labda kiuchumi, kiafya, kielimu, heshima n.k

Ndoto ya pili umeota upo mazingira ya shule, hii tafsiri yake ni kudumaa kimaendeleo yani kila siku upo palepale upigi hatua, unafanya mambo yaleyale.

Ndoto zote zinaonekana ni za kurudi nyuma, kwaiyo mkuu kwa imani yako omba sana hizo roho zishindwe
 
Nashukuru kwa maoni yako
 
shukran kwa maoni yako kiongozi
 
Sijuhi una abudu wapi maana mimi ni muhanga wa kuota ndoto za kutisha,kama nakimbizwa na nyoka n k ila hii inajuludia siku zote,jitahidi kusali before hujalala Sali muite Yesu akulinde
 
Mimi ni mkristo Mkatoliki, Nashukuru kwa maoni na ushauri wako
Sijuhi una abudu wapi maana mimi ni muhanga wa kuota ndoto za kutisha,kama nakimbizwa na nyoka n k ila hii inajuludia siku zote,jitahidi kusali before hujalala Sali muite Yesu akulinde
 
Pole na hongera kwa ushindi,

Kwanza ili uelewe ni kujua kusudi,tulikusudiwa tuwe na ONO ili tuone ya mbele kama ni mazuri tushukuru yatokee na kama ni mabaya tushukuru yafutike (efeso 3:10).

Hayo ulioota ni mambo uliyopitia tangu unazaliwa hadi sasa yanamadai kwako yanataka kukuzamisha (korongo la giza)

Muumba pekee aliyekuja juu ya nchi (zekaria 14:9,Isaya 57:15,ufunuo 21:1-3) ndiye wa kukutoa kwenye mfumo huo uliotangulia kwako ili sasa uishi kwa amani na furaha baada ya kujua aliyekuumba amekukusudia mema na amekuja kukutoa kwenye uteka uliokuwepo bila kujijua.
 
Ndoto ya kuwa kwenye korongo kubwa nikwambaadui amefunga milango ya baraka zako naamekufungia mbali sana ambapo hautowezakupata msaada wa haraka unaopoona umerudi shule na marafiki utakaofanikiwa kuwaona kwenye ndoto au wanafunzi ina maanisha unarudishwa nyuma kiuchumi maisha yako yatakuwa ya shida sana, OMBA MUNGU BABA, YESU KRISTO ALIYE HAI AKUTOE WALIKOKUFUNGIA MAADUI, akafungue milango ya baraka kwenye maisha yako , sali sana kabla hujalala ukiwa kwenye ndoto unaweza kutaja jina la BWANA YESU NAMOMBA UNISAIDIE NENO HILO LINA NGUVU KUPITA MAJINA YOTE DUNIANI BASI MUNGU ALIYE HAI atakusaidia kila adui akitaka kukuangusha chini tusali sana jamni kuna mengi hatuyajui
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…