Mtu halisi yupo kwenye ndoto.
Usipuuze ndoto uotayo Hasa ikijirudia,
Hata watu waliokufa Kwa AJALI, wengi waliona ktk ndoto wakapuuza au kukosa tafsiri ya ndoto.
Mtu ni ROHO anayo NAFSI na anaishi ndani ya MWILI.
Kuna ndoto aina tatu.
1. Ndoto zitokanazo na uchovu au shughuli za Kila siku.
KAZI uliyofanya mchana itajirudia vile vile nk nk
2. Ndoto Kutoka Kwa Shetani.
Hizi huja kimkakati kukutoa katika kusudi la Mungu,
Mara nyingi zinawakuta waendao Kwa mganga, Atakuotesha mama Yako mzazi ndiye mchawi na utamwona kwenye ndoto Ili mfarakane ktk familia.
Zingine utajikuta unapata maoni ktk ndoto, mfano Mfalme daudi aliletewa mawazo Kutoka Kwa Shetani Ili awahesabu Wana wa Israel kinyume na mapenzi ya MUNGU.
3. Ndoto Kutoka Kwa Mungu.
Mtu Kwakuwa ni ROHO, huona Kila kitu kubaya anachopangiwa na maadui au wema Kwa maana hakuna Siri ktk Ulimwengu wa ROHO, Mungu Ameweka macho hayo ya ndani Kwa Kila mtu.
Ukiota unakimbizwa au kushambuliwa na Wanyama, ni wachawi hai wamevaa sura za wanyama usiwatamvue lakini utawaona ukiwaamuru waonekane Kwa sura zao kupitia Jina la YESU.
USHAURI: Rudi kazini Kwa kuomba radhi, na uache kufanya maamuzi Kwa kukurupuka, tafuta kuisikia sauti ya Mungu ktk Kila uamuzi unaotaka kufanya utafanikiwa.
Amen.