Ndoto hii ina maanisha nini?

Ndoto hii ina maanisha nini?

Yohimbine

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2019
Posts
873
Reaction score
1,841
Habari wakuu poleni na Majukumu ya kutafuta ugali ,japo ni mgumu naamini sote tutaupata.

Wakuu kuna hii ndoto imenishtua sana leo naomba wale wenye utaalamu wa ndoto hii wanielezee iko hivi.

Nimeota nipo shule ya bweni sasa siku hiyo ilikua ni siku ya kufunga shule majira ya mchana hivi mimi nikaamua nisiondoke nyumbani kwa maana nitakosa usafiri ndipo katika nikaamua kutoka nje ya shule nitambue mazingira yapoje ,katika kutoka huko ndipo nikakutana na mtu mmoja tunafahamina (huyu ni padri katika parokia ya nyumbani kwetu)akaamua anipe malazi mpaka hiyo kesho itapofika niweze kuondoka.

Padri yule pale kwake akapata dharura akaondoka nikabaki pale na watu wa nyumbani kwake mda wa usiku nikapewa chakula changu pendwa nikala sasa shida inakuja mda wa kulala.Wakati nimelala usiku ghafla wakatokea watu wawili kama wachawi na watu hawa walikua wanaongea maneno kama wana ugomvi na yule padri kwahiyo wakaanza kunichukua na kutafuta nguvu nilizonazo ili wazichukue wakaanza na nguvu moja baada ya nyengine.

Katika uchunguzi wao nikajikuta nna nguvu ya kuteleport(kupotea na kutoonekana kwa muda) ,nguvu ya pili wakakuta nna uwezo wa kupaa yani nlikua na mabawa kama yale ya malaika pia wakakuta nna uwezo wa nguvu za mikono.

Mwisho kabisa wakaanza kuzichukua zile nguvu lakini mpaka wanamaliza wakaonyesha kusikitika wakiwa na maana jaribio lao limeshindwa na hapo ndio ghafla nikashtuka usingizini.

Mwenye uelewa na hii ndoto
Rakim
 
Hizo nguvu za ajabu ni aina ya bangi unayotumia, labda ni adimu sana. Wahi serikalini ujisajili mkuu watakuja physically
 
Ulikuwa unagombana na roho za kichawi. Mwili ulipumzika nafasi ilikuwa inafany kazi ya kuituma roho kuokoa mwili usidhieike na roho za kichawi zilizo kufuata. Shukuru ulishinda huo ugomvi.
 
Wewe ni mtu wa imani, ila kuna wakati unalega (either kutokana na mizaha, kufuata makundi, uvivu, nk). Mlinzi wa kwanza kwetu ni Mungu mwenyewe, na mlinzi wa pili ni sisi wenyewe, yaani tujilinde wenyewe, na Mungu alitupatia uwezo huo. Unavyolega kiimani, ni sawa na kuacha godown lenye mali nyingi bila mlinzi (au walinzi), ambapo wezi watavamia na kuiba kila kitu.

Unachokiona ni roho chafu zinakunyemelea baada ya kuona unaanza kupoteza nguvu, na wao wanaweza kukufanya chochote. Unakumbuka tulipokuwa watoto, tulikuwa na tabia ya kuoneana, hasa ukimwona mwenzako ni mdogo kwako? Sasa hata hawa viumbe wana tabia hiyo. Wanachungulia kwanza kwa mbali, wakibaini pale kuna udhaifu, hujisemea huyu ni mnyonge wetu, ndipo wanakuja mazima.

Jiimarishe kwenye imani yako, wakikuangalia kwa mbali, hawakuoni wewe, bali wanaona moto tu unawaka. Hapo hujikatia tamaa na kuondoka zao.
 
Tatizo ni hiko chakula ulichopewa kwenye ndoto ni chakula chao wachawi, sasa wanataka wakakufanyishe kazi...
 
Wewe ni mtu wa imani, ila kuna wakati unalega (either kutokana na mizaha, kufuata makundi, uvivu, nk). Mlinzi wa kwanza kwetu ni Mungu mwenyewe, na mlinzi wa pili ni sisi wenyewe, yaani tujilinde wenyewe, na Mungu alitupatia uwezo huo. Unavyolega kiimani, ni sawa na kuacha godown lenye mali nyingi bila mlinzi (au walinzi), ambapo wezi watavamia na kuiba kila kitu.

Unachokiona ni roho chafu zinakunyemelea baada ya kuona unaanza kupoteza nguvu, na wao wanaweza kukufanya chochote. Unakumbuka tulipokuwa watoto, tulikuwa na tabia ya kuoneana, hasa ukimwona mwenzako ni mdogo kwako? Sasa hata hawa viumbe wana tabia hiyo. Wanachungulia kwanza kwa mbali, wakibaini pale kuna udhaifu, hujisemea huyu ni mnyonge wetu, ndipo wanakuja mazima.

Jiimarishe kwenye imani yako, wakikuangalia kwa mbali, hawakuoni wewe, bali wanaona moto tu unawaka. Hapo hujikatia tamaa na kuondoka zao.
Asante mkuu ntafanyia kazi
 
Kuota upo shule uliyosoma kuna maanisha ni nguvu za kichawi au wachawi wanataka wakurudishe nyuma dhidi ya mafanikio yako ya kiroho, kiuchumi au kimwili.
 
Hilo ni tukio halisi roho yako ilikuwa inapambana live kushindana na wachawi, na itoshe kusema hata huyo padri ni mmoja wao. Au yeye ndo kawawekea kauzibe kwa maana bila yeye ungeendelea na safarii huko huko njia wakakudakia, kumbuka walikuwa wakikufatilia kabla hata ujaingia shuleni hapo.
 
Ahsante kiongozi
 
Sema padri hatufahamiani ni kwa sura tu
 
Habari wakuu poleni na Majukumu ya kutafuta ugali ,japo ni mgumu naamini sote tutaupata.

Wakuu kuna hii ndoto imenishtua sana leo naomba wale wenye utaalamu wa ndoto hii wanielezee iko hivi.

Nimeota nipo shule ya bweni sasa siku hiyo ilikua ni siku ya kufunga shule majira ya mchana hivi mimi nikaamua nisiondoke nyumbani kwa maana nitakosa usafiri ndipo katika nikaamua kutoka nje ya shule nitambue mazingira yapoje ,katika kutoka huko ndipo nikakutana na mtu mmoja tunafahamina (huyu ni padri katika parokia ya nyumbani kwetu)akaamua anipe malazi mpaka hiyo kesho itapofika niweze kuondoka.

Padri yule pale kwake akapata dharura akaondoka nikabaki pale na watu wa nyumbani kwake mda wa usiku nikapewa chakula changu pendwa nikala sasa shida inakuja mda wa kulala.Wakati nimelala usiku ghafla wakatokea watu wawili kama wachawi na watu hawa walikua wanaongea maneno kama wana ugomvi na yule padri kwahiyo wakaanza kunichukua na kutafuta nguvu nilizonazo ili wazichukue wakaanza na nguvu moja baada ya nyengine.

Katika uchunguzi wao nikajikuta nna nguvu ya kuteleport(kupotea na kutoonekana kwa muda) ,nguvu ya pili wakakuta nna uwezo wa kupaa yani nlikua na mabawa kama yale ya malaika pia wakakuta nna uwezo wa nguvu za mikono.

Mwisho kabisa wakaanza kuzichukua zile nguvu lakini mpaka wanamaliza wakaonyesha kusikitika wakiwa na maana jaribio lao limeshindwa na hapo ndio ghafla nikashtuka usingizini.

Mwenye uelewa na hii ndoto
Rakim
ushindi
 
Back
Top Bottom