Ndoto mbili za kweli (ndoto za kichawi) - unashauriwa kufanya sana ibada

RIGHT MARKER

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
129
Reaction score
473
💼MHADHARA WA 7
Wakati mwingine ndoto tunazoota usiku wakati wa kulala zinatokana na uchovu, mawazo, n.k. Lakini ndoto zifuatazo zinakuwa ni ndoto zinazoeleza matokeo ya kweli yanayotarajia kukutokea baadae.

1. NDOTO YA KWANZA
Kuota mara kwa mara umekufa. Au kama umeoa/umeolewa unaota mara mwa mara Mwenza wako amekufa ilhali upo nae kitandani mzima wa afya ------ Hii ni ndoto ya kweli na kwa asilimia kubwa inakulenga wewe mwenyewe, ni ndoto inayokukumbusha kwamba unawindwa na wanaokuwinda wamechachamaa kwelikweli. Kama umefikia hatua ya kuota hivyo tafadhali nenda kamuone Shekhe au Mchungaji uombewe kisha uanze kufanya ibada haraka sana, kama tayari ni mtu wa ibada kaza kamba ya kuabudu kwelikweli. Achana na makandokando yanayodhohofisha ibada yako wabaya wako watakupindua.

2. NDOTO YA PILI
Kuota mara kwa mara mtu (mchawi) anakutokea chumbani kwako ----- Kama unaota ndoto ya kutokewa na mchawi ndani kwako na ndoto hiyo isipojirudia mara kwa mara yawezekana ikawa ni ndoto ya kawaida. Lakini ndoto hiyo ikijirudia mara kwa mara kwa staili ile ile, hiyo ndoto ni ya kweli. Nikisema staili ile ile namaanisha kwa mfano unaota mtu mbaya mwenye mavazi fulani ya kutisha amekuja chumbani kwako amesimama anakutazama au anakufanyia mambo ya kichawi, halafu ndoto hiyo inajirudia mara kwa mara vivyo hivyo. Hiyo ndoto ni ya kweli, anza kufanya ibada haraka sana.

MATOKEO YA HIZI NDOTO:
Kama nilivyoeleza hapo awali, hizo ni ndoto za kukukumbusha kuwa umezingirwa, na matokeo yake ni;
1. Kuchukuliwa msukule.
2. Mikosi kwenye maisha yako - Kujitafuta bila kujipata.
3. Kuchukiwa na kila mtu (nuksi), na kila jema unalolifanya haliwi jema kwa watu kama ulivyokusudia.
4. Kuvunjika kwa ndoa yako, au kutoelewana na ndugu zako.
5. Kutokuwa na bahati kwenye utafutaji wako wa maisha, hata kama una nyota ya mafanikio inachafuka.
6. Kuugua mara kwa mara, au kuwa mlevi na malaya wa kupindukia ili kupoteza hela unazopata.
7. Kupoteza ajira, au biashara yako kufirisika.

USHAURI:
Usikimbilie kwa Waganga, bali anza kufanya ibada. Kama tayari umekuwa Mcha Mungu hakikisha usiwe na makandokando yanayodhohofisha ibada yako.

BY: RIGHT MARKER-TZ
Mbezi Louis, Dar es salaam.
 
Haya mambo haya!!! Siku unaamka mara umenyonyolewa nywele na wachawi. Hahaaaa nikikumbuka nacheka nachoka nachakaa
 
Huyo

Huyo Mungu wanamfahamu? Ibada kwa miungu inamfunga mtu. Bila kumwamini na kumpokea Yesu Kristo hakuna namna ya kumshinda shetani.
 
Imani nayo itamfaa mwenye kufikiri kwa kina na aliyesoma dini akaelewa. Ukiamini bila kusoma Maandiko vizuri utaishiatu kutajataja majina ya mitume.
 
Back
Top Bottom