Bob Manson
JF-Expert Member
- May 16, 2021
- 4,158
- 7,787
Binafsi naamini purpose kuu ya mwanamke katika dunia hii ni kuwa mama bora wa familia yenye furaha na Amani.
Mimi ndoto na matamanio yangu ni siku moja nimuone mwanangu wa kike akiolewa kwa wakati sahihi na mtu sahihi, awe mama bora na mlezi bora wa familia yake, hiyo ndiyo itakuwa furaha kuu kwangu.
Japo mambo kama shule na elimu nyinginezo zina umuhimu, umuhimu ambao hupatikana kwa matumizi ya taaluma hizo kwa manufaa ya kupata ajira na tutengeneza kipato.
Nitajitahidi kadri niwezavyo kumlea na kumuandaa aje kuwa mama bora wa nyumba yake tofauti na kuwa Boss au mfanyakazi bora katika ofisi yake.
Itakuwa na maana gani endapo Binti akifanikiwa kupata kazi na kipato kikubwa ilhali hana familia imara na yenye furaha?
Nahimiza wazazi wenzangu kuwaandaa watoto wao wakike kuwa Mama bora na si kuegemea upande mmoja wa elimu kisha kusahau purpose halisi ya mwanamke katika dunia hii.
Pia soma: Nachukizwa na wanaomuita mwanangu Zuchu