Ooo kibibi upo?. Lengo lako kama kawaida ni kumlenga Marehemu Raisi Nyerere. Chuki yako kwa huyo mzee ambae leo hii hayupo duniani inashangaza sana. Kwanza kibibi wewe nikueleze kwamba majaribio ya mapinduzi si kiegezo cha kipimo kwa utawala bora wa nchi. Hiyo hutokana na na hali ya kisiasa ya kiujumla duniani ilivyo. Kipind cha uongozi wa hayati Nyerere, kilikuwa kipindi cha vita kali vya baridi kati ya mataifa ya mrengo wa kushoto na wakulia. Mataifa makubwa ya yalisababisha kuangushwa kwa serekali mbali mbali hasa Africa na majaribio kabao ya kupindua serekali, na hata kufanikisha kuuwawa kwa baadhi ya viongozi wa nchi za Africa. Kipindi cha Nyerere kama sikosei yalifanyika majaribio mawili, lakini watuhumiwa walifikishwa mahakamani kama sheria na katiba inavyohitaji, na sheria ikachukua mkondo wake. Sikumbuki kusikia kama kuna adhabu ya kifo ilitekelezwa kwa waliokutwa na hatia. Tofauti kabisa na yanayo onekana siku hizi, watu kung'olewa meno, kuteswa, ama kupotezwa bila ya maelezo pale wanapotuhumiwa kwenda kinyume na utawala ama kutoa mawazo yanayo pishana na utawala.