Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wao wamewekeza kwenye gesi, wanataka tufunge mitungi.Hivi kwenye ile dira ya taifa waliyotoa maoni kipengele cha kupunguza hewa ukaa hawakukigusia au wako busy na kampeni ya mama yao ya nishati ya kupikia ili wauze cylinder za LPG kupitia kwa dalali mhajemi?
Noma sana.Niseme tu 2025 kumiliki EV yangu ya kwanza kushakauka kama hivi.
Baada ya kukesha na kuomba muhusika wa TRA acheki vizuri kikokotoo nilete Nissan Leaf nisupport juhudi za green environment na kuwaunga mkono TANESCO naona mission imefeli.
Anaehusika na kuset kodi za magari used TRA aangalie vizuri ushuru wa Nissan Leaf 2019 EV nataka ivuta Februari!
Mzigo umeishia kupunguzwa million mbili na nusu tu.
Kutoka hapa Mil 23.2 ushuru wa mwaka jana.
View attachment 3190804
Kuja Mil 20.8 tu ushuru wa mwaka huu 2025.
View attachment 3190809
Hii ndio ilikua dream car yangu ila kuwapa TRA Tanzania mil 20 sitakaa nikafanya ivo kwa kipato changu cha sasa.
Kila lakheri EV, tutaonana miaka ijayo.
Nimemaanisha muonekano wake wa nje na ndani, body ipo vizuri sana.Nissan Leaf inawakimbiza katika aspects tatu:
1. Cheap/Affordable
2. Reliability
3. Spare/Body parts
Ila ina mapungufu makubwa matatu
We jamaa una madini mengi sana..Nissan Leaf inawakimbiza katika aspects tatu:
1. Cheap/Affordable
2. Reliability
3. Spare/Body parts
Ila ina mapungufu makubwa matatu:
1. Battery dogo (40kWh) lina range ya 260km tu likiwa full charge.
2. Thermal management ya joto kwenye battery ni air-cooling wakati magari ya siku hizi ni liquid-cooling. Hii inapelekea battery kupata joto sana wakati wa kucharge na inapelekea battery degradation kua kubwa. Ila kuna jinsi ya kuepuka, mfano kukwepa fast charger, kucharge usiku au muda ambao hamna jua kali, na kuzuia battery isifike below 30% na isivuke 80%
3. Nissan Leaf inatumia charger za CHAdeMO ambazo ni technology ya zamani siku hizi zimephase out. Kwahiyo kupata public charger yenye hii connector ngumu. Siku hizi magari yanatumia universal CCS. Yaan kwa lugha nyepesi ni kama tuseme kampuni itengeneze simu ambazo charger zake zile za kizamaniii wakati kila mtu ana type C. Inamaana charger ikiisha kazini we huna wa kumuazima hadi hurudi home. PS: Kuna adapter ya kutoka CHAdeMO to CCS ila last time niliona inauzwa $700+
Like serious huu mwaka nilikua naleta Nissan Leaf ila TRA jau sana.
Duh kazi ipo!Wao wamewekeza kwenye gesi, wanataka tufunge mitungi.
Muonekano iko poa sana ingawa watu wengi wanasemaga haijakaa kama EV imekaa kama "magari ya kawaida" sio futuristic kama EV zingine.Nimemaanisha muonekano wake wa nje na ndani, body ipo vizuri sana.
Kuhusu hizo changamoto zake, vipi kwa matoleo ya kuanzia 2022 hadi 2024 hazijafanyiwa kazi?.
Mimi nazielewa ila siku hizi nimekuwa mpenzi wa SUV au crossover zaidi.Kusema kweli mi Prius 3rd gen uwa naielewa.
Labda cha kuwaza sana ni spare, sio mafundi. Maana fundi yoyote anaejua kazi yake anatengeneza.We jamaa una madini mengi sana..
Sasa hiyo nissan leaf mfano ikapata mzinga front end yote ikazingua una uhakika mafundi wa hapa watairudisha road?
Yeah hapo umenepa mzee.Duh kazi ipo!
Nachofikiri kuna mgongano wa kimaslahi ukichunguza vizuri wanasiasa wengi wanamiliki hizo gas station[filling stations] na ndio collateral zao hivyo ili mpate EV lazima bill ya conflict of interest kuhusu EV ipite pale bungeni kitu ambacho ni kigumu tofauti na hapo msubiri mabadiliko makubwa ya kisera duniani 2035 nadhani kwenye ile mikopo wanayopata kuna kipengele kitawabana.
Hapa nilipo nadhani tuliobaki na hizi gari za mafuta tumebaki wachache wengi washahamia kwenye EV nami naona soon by February nitawaunga mkono kwenye kampeni yao waliyoipa jina #100green.
Hivi ile anaconda vipi mkuu? Japo hainivutii sanaMchawi budget na mapenzi. Ila kama Hybrid kutoka Honda naToyota ni nzuri.
Nimeitamani prius phv(xw50) aisee ni katamu japo inachukua abiria wa3 tu, ila changamoto mpaka unaitia barabarani si mchezo, inaenda kati ya km 50+ hivi kwa lita moja ya mafuta.Kusema kweli mi Prius 3rd gen uwa naielewa.
Nenda kwa wachina mzee.. wapo seriousMimi nazielewa ila siku hizi nimekuwa mpenzi wa SUV au crossover zaidi.
Sema mimi now ni mpenz wa hybrid. Ipi hybrid unayoiona inafaa mkuu?
Ila betri yake ikifa jasho lazima likutoke.Umeme wa nyumbani wa kuchajia simu mkuu unachaji fresh tu.
Si kama wana usikivu basiKama nasema kama serikali ikiamua kushift kutoka mafuta kwenda EV wata save 70% ya gharama za uendeshaji wa mambo ya usafiri.