Ndoto ya kumiliki EV naona inayeyuka. Anaehusika na kuset kikokotoo TRA amelisikia ombi, ila kapunguza Milioni 2.5 tu!

Hivi kwenye ile dira ya taifa waliyotoa maoni kipengele cha kupunguza hewa ukaa hawakukigusia au wako busy na kampeni ya mama yao ya nishati ya kupikia ili wauze cylinder za LPG kupitia kwa dalali mhajemi?
 
Aisee hivi ndio vyuma tuvitakavyo. Kwa hiyo kwa ushuru wa sasa, bajeti yake inakua kiasi gani mpaka gari iwe mkononi kwako?
Kwa Nissan Leaf hii generation ya pili (201😎 naona ushuru sio rafiki. Lazima uwe na 35 Mil kuja juu.
 
Hivi kwenye ile dira ya taifa waliyotoa maoni kipengele cha kupunguza hewa ukaa hawakukigusia au wako busy na kampeni ya mama yao ya nishati ya kupikia ili wauze cylinder za LPG kupitia kwa dalali mhajemi?
Wao wamewekeza kwenye gesi, wanataka tufunge mitungi.
 
Noma sana.
Mwonekano wake sijauelewa naona kama umekaa ki prius
 
Nissan Leaf inawakimbiza katika aspects tatu:
1. Cheap/Affordable
2. Reliability
3. Spare/Body parts

Ila ina mapungufu makubwa matatu
Nimemaanisha muonekano wake wa nje na ndani, body ipo vizuri sana.

Kuhusu hizo changamoto zake, vipi kwa matoleo ya kuanzia 2022 hadi 2024 hazijafanyiwa kazi?.
 
We jamaa una madini mengi sana..

Sasa hiyo nissan leaf mfano ikapata mzinga front end yote ikazingua una uhakika mafundi wa hapa watairudisha road?
 
Wao wamewekeza kwenye gesi, wanataka tufunge mitungi.
Duh kazi ipo!

Nachofikiri kuna mgongano wa kimaslahi ukichunguza vizuri wanasiasa wengi wanamiliki hizo gas station[filling stations] na ndio collateral zao hivyo ili mpate EV lazima bill ya conflict of interest kuhusu EV ipite pale bungeni kitu ambacho ni kigumu tofauti na hapo msubiri mabadiliko makubwa ya kisera duniani 2035 nadhani kwenye ile mikopo wanayopata kuna kipengele kitawabana.

Hapa nilipo nadhani tuliobaki na hizi gari za mafuta tumebaki wachache wengi washahamia kwenye EV nami naona soon by February nitawaunga mkono kwenye kampeni yao waliyoipa jina #100green.
 
Nimemaanisha muonekano wake wa nje na ndani, body ipo vizuri sana.

Kuhusu hizo changamoto zake, vipi kwa matoleo ya kuanzia 2022 hadi 2024 hazijafanyiwa kazi?.
Muonekano iko poa sana ingawa watu wengi wanasemaga haijakaa kama EV imekaa kama "magari ya kawaida" sio futuristic kama EV zingine.

Changamoto ni izo tu, na still 2022-2025 bado ni zile zile second generation ZAA-ZE1 hadi mwakani 2026 ndio 3rd gen itatoka.

Hii inatabiriwa kya na battery kubwa (range zaidi ya 400 km), thermal management nzuri, NCC chargers etc.
 
We jamaa una madini mengi sana..

Sasa hiyo nissan leaf mfano ikapata mzinga front end yote ikazingua una uhakika mafundi wa hapa watairudisha road?
Labda cha kuwaza sana ni spare, sio mafundi. Maana fundi yoyote anaejua kazi yake anatengeneza.

Uzuri wa EV haina vitu vingi kama magari ya mafuta ICE.

Mfano ulivyosema ikipata mzinga mbele hakuna engine, battery iko chini so mbele kitachoharibika ni motor, battery ndogo 12V na vitu vidogo vidogo.
 
Yeah hapo umenepa mzee.

Lazima kuna mgongano wa kimaslahi maana mafuta yana pesa sana aisee.
 
Kusema kweli mi Prius 3rd gen uwa naielewa.
Nimeitamani prius phv(xw50) aisee ni katamu japo inachukua abiria wa3 tu, ila changamoto mpaka unaitia barabarani si mchezo, inaenda kati ya km 50+ hivi kwa lita moja ya mafuta.
Kisha kuna mitsubishi outlander phev ipo ya gg2 na gg3, toleo la gg3 ni unyama zaidi, changamoto ni hizo kodi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…