Ndoto ya kupaa na kuelea hewani huku unakatiza mitaa

Ndoto ya kupaa na kuelea hewani huku unakatiza mitaa

baharia 1

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2019
Posts
1,580
Reaction score
1,773
Habari wakuu,

Naombeni kuuliza leo nimeota nipo mtaani kwangu nikawa naruka kama ndege lakini sina mabawa naruka huku nimesimama wima, nazunguka zunguka mtaani kila kona napita nakutana na watu wanaonifahamu wananishangaa nakutana na watu wazima nashuka chini huku tunapeana mikono tunasalimiana naendelea tena kupaa watu wengi wananishangaa sana japo nilikuwa napaa siyo juu sana, mbele nikakutana na rafiki yangu mmoja hivi namfahamu amekaa na watu nikashuka tukawa tunatembea nikajaribu tena kuruka nikaona nashindwa nikapotezea tukawa tunatembea.

Mwenye uelewa na ndoto hii wakuu.

Mshana Jr karibu


NB: Jamani kuota unapaa raha sana.
Asanteni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahaha hii ndoto ni ya kipumbavu sana, halafu usikute sisi binadamu kuna ndoto fulani fulani za kipumbavu huwaga tunaota wote sema hatupati muda wa kujadili kwa pamoja tu.

Kwa mfano mbali na hiyo, mimi kuna moja naotaga mara kwa mara kuwa nikiwa natembea zile sehemu zenye michanga michanga barabarani nikienda kutifua tifua nakuta sarafu nyingi sana za pesa yani ni mwendo wa kuziokota kiubwelelele kabisa yani kila unapogusa masarafu tu basi akili inakuwa imeridhika unakuwa kwenye extreme level ya comfort zone ila kimbembe ukiamka sasa [emoji1][emoji1]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anything can happen in a dream, hakuna laws zozote za sayansi zinazo apply ndotoni. Maana yake ni kwamba chochote ubongo wako utakachotaka kufanya kitawezekana.

Nakumbuka utotoni nilijitrain kuota nikiwa najua kwamba naota, nilifanya mambo mengi niliyowahi kutamani kufanya including dating with my childhood crush[emoji1]

Maamuzi uliyoyafanya ndotoni ndio maamuzi unayoyafanyaga kila siku kwenye maisha halisi. Kwa maoni yangu nafikiri, u have a powerful mind ila u always doubt uwezo wako ukiwa na watu fulani. Ukiondoa mashaka utafanikiwa zaidi katika mambo unayo yafanya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom