Ndoto ya mke wangu imepunguza upendo na amani kwenye nyumba yetu

Ndoto ya mke wangu imepunguza upendo na amani kwenye nyumba yetu

Mwambie ni ndoto tuu asiwekee sana kwenye mawazo hutokea chamsingi a ombe dua kabla hajalala.....
 
huwa tunasali kila siku kabla ya kulala, lakini mwenzangu tangu aote ndoto hiyo hataki hata kusali na mimi.
Ndio pepo lenyewe,
Nenden kwa viongozi wenu wa maombi mkaombewe,
Waje na nyumbani kwenu wapaombee,
Msikubali pepo huyo akapata mamlaka kati yenu na kuivunja ndoa yenu,tena msipoteze mda kwan mnapambana na nguvu isiyoyakawaida na mnahitaji msaada wa nguvu za mungu haraka.
 
Kweli njozi nyingine za tisha, mi mwenyewe kihoro na kitete kimenijaa baada ya kusoma hiyo njozi

Isaya 41:10 Basi, usiogope, mimi nipo pamoja nawe. Usifadhaike, mimi ni Mungu wako. Nitakuimarisha na kukusaidia; nitakulinda kwa mkono wangu wa ushindi
 
images

....lol, niki 'connect- - the- -dots' cobra na tendo la ndoa....hahaha...ni ndoto tu hiyo "Snake Charmer!"
 
Kwa elimu yangu ya Ndoto ni kuwa huyo nyoka kama ni Mkubwa ni dalili ya kuwa Mke wako ana Pepo mbaya ndani ya mwili wake na huyo Shetani ni dume huwa anamjia katika usingizini kwa njia ya ndoto. Na itafika wakati atakuwa akilala na wewe kwenye kitanda huyo mke wako atakuwa analala kwa ubavu kwa pembeni hataki muwe pamoja na wewe mtakuwa mnalala kitanda kimoja na

hamfanyi tendo lenu la mapenzi tunaweza kusema ana shetani Mwanamme huyo mke wako itafika wakati hata kama utakuwa unafanya nae mapenzi atakuwa hajisikii raha ndani ya mapenzi yenu. Na atakuwa akiamka asubuhi mke wako atakuwa anajisikia kama

kuumwa na kichwa kwa wakati mwengine atakuwa ni mchovu wa mwili kama vile aliyefanya kazi nzito wakati wa usingizini usiku. Nakushauri fanya hii dawa kwanza kwa muda wa kama siku 3 upate magamba ya vitunguu saumu uchanganye na maji kila anapolala
usiku awe anajipakaa yale maji yaliyochanganyika na magamba ya vitunguu saumu ili kumfanya yule shetani dume amkimbie ili ndoa yenu idumu atumie hiyo dawa kwa muda wa siku kama 3 kila usiku anapolala ajipake hayo maji ya magamba ya vitunguu

saumu kwa huo muda wa siku3. Na kama wewe na mke wako ni wakristo mpeleke kwa Mchungaji akamuombee dua la kama wewe ni Muislam mpelkee kwa Sheikh amuombee dua ili huyo shetani mbaya amtoke ndani ya mwili wa mke wako asante. Huo ndio ushauri wangu.

Hii ilimu nzito sana....
 
maisha ya pamoja naona yanawashinda. HIVI SIKU AKIOTA KALALA KITANDA KIMOJA NA RAIS , ATAHAMA KWAKO AENDE IKULU.........?
 
Mke wangu mwezi uliopita aliota ndoto. Ndoto yenyewe ni hii:-
eti alikuwa ameniudhi, kwa hasira nikamwambia utanikoma.
Nikaondoka kwa hasira, niliporudi nikarudi na nyoka mkubwa sana aina ya cobra, akawa ananisihi nisimdhuru na huyo nyoka.
Kwa hasira nikamuwekea huyo nyoka kwenye mkono wake.
Nyoka akawa anamtafuna mkono na hakuwa na mtu wa kumsaidia.
Watu wote walikuwa wakimshangaa, na mwishoni akasaidiwa na shehe mmoja.
Tangu ameota ndoto hiyo upendo umeshuka sana ndani ya nyumba, hamna amani, muda wote ni mnyonge na hana raha kabisa.
Muda wote amekuwa akibubujikwa na machozi na amepoteza kabisa hamu ya tendo la ndoa.
Wapendwa naomba msaada wenu, je nifanye nini ili kurudisha furaha na upendo, pia imani na amani vilivyo potea??
Je hiyo ndoto ina tafsiri au maana gani?
Naamini JF ni kisima cha hekima nitapata msaada wa kutosha kutokana na busara na hekima zennu.

Acha ushirikina, ndoto ni kiut cha kawaida. Ukiota unakufa huwa inatokea kweli? Acha!!!!!!!!!!!!!
 
Wee mzizimkavu, umeanza lini kutafsiri ndoto?

Kwa elimu yangu ya Ndoto ni kuwa huyo nyoka kama ni Mkubwa ni dalili ya kuwa Mke wako ana Pepo mbaya ndani ya mwili wake na huyo Shetani ni dume huwa anamjia katika usingizini kwa njia ya ndoto. Na itafika wakati atakuwa akilala na wewe kwenye kitanda huyo mke wako atakuwa analala kwa ubavu kwa pembeni hataki muwe pamoja na wewe mtakuwa mnalala kitanda kimoja na

hamfanyi tendo lenu la mapenzi tunaweza kusema ana shetani Mwanamme huyo mke wako itafika wakati hata kama utakuwa unafanya nae mapenzi atakuwa hajisikii raha ndani ya mapenzi yenu. Na atakuwa akiamka asubuhi mke wako atakuwa anajisikia kama

kuumwa na kichwa kwa wakati mwengine atakuwa ni mchovu wa mwili kama vile aliyefanya kazi nzito wakati wa usingizini usiku. Nakushauri fanya hii dawa kwanza kwa muda wa kama siku 3 upate magamba ya vitunguu saumu uchanganye na maji kila anapolala
usiku awe anajipakaa yale maji yaliyochanganyika na magamba ya vitunguu saumu ili kumfanya yule shetani dume amkimbie ili ndoa yenu idumu atumie hiyo dawa kwa muda wa siku kama 3 kila usiku anapolala ajipake hayo maji ya magamba ya vitunguu

saumu kwa huo muda wa siku3. Na kama wewe na mke wako ni wakristo mpeleke kwa Mchungaji akamuombee dua la kama wewe ni Muislam mpelkee kwa Sheikh amuombee dua ili huyo shetani mbaya amtoke ndani ya mwili wa mke wako asante. Huo ndio ushauri wangu.
 
Sasa kama hataki hata kushiriki sala wakati wa kulala, huyo ana lake jambo, sijui mnaabudu wapi, lakini mngeenda kwenye vipindi vya fellowship na maombi kanisani akaombewe

huwa tunasali kila siku kabla ya kulala, lakini mwenzangu tangu aote ndoto hiyo hataki hata kusali na mimi.
 
Pigeni maombi maana wanasema watu, shetani (kwa kutumia vimada na vidumu) anaziwinda sana ndoa. Huwezi jua what is behind.:A S 465:
 
Back
Top Bottom