Ndoto yangu 2025 - 2030 tuna na Bunge kama la Makinda na Samweli Sitta

Ndoto yangu 2025 - 2030 tuna na Bunge kama la Makinda na Samweli Sitta

Kiranja wa jamii

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2023
Posts
1,222
Reaction score
2,912
Nipo kwenye daladala, dereva amefungulia mziki mnene wa singeli, kondakta amevalia suruali ya bluu imejaa viraka kila kona na sehemu nyingine imechanika chanika, hana mpango wa kuishona wala kuifua

Fulana yake ndiyo iliyonitambulisha kuwa kumbe zile ni yunifomu zake na polisi wa usalama barabrani hajali uchafu wake na hizo nguo anachojali ni kwamba yupo ndani ya sare rasmi ya kondakta na akimpa mkono utaachia kitu kidogo alichoshika, hayo ya uchafu na viraka havimuhusu!

Daladala imejaa pomoni, nimebahatika kupata siti lakini waliosimama ni wengi! Wanaume kwa wanawake, watoto kwa vijana! Wengi wanafurahia singeli ya dereva na wachache wanajisugua sugua kwenye viuno vya kina dada walisimama wima na wala hata wakiguswa hawajigusi. Raha mustarehe!

Ghafla nikaegemeza kichwa changu kwenye siti nisiendelee kuangali yanayoendelea.

Usingizi ukanipitia, nikaanza kuota kwa kuwatafakari wale abiria wenzangu kama kuna anayejali hayo mambo yenu ya katiba mpya? No reform No election? Oktoba tuna tick?

Ndoto ikawa nzito zaidi nikaanza kuona wabunge wanasimama kidete wakaanza kuhoji;

1. Kwanini Bandari imeuzwa? Mkataba ukapelekwa mezani kwa Spika wakaanza kuchambua kipengele kwa kipengele

2. Hoja nyingine ikaibuliwa, Kwanini wamasai walihamishwa kwenye ardhi yao? Spika akamuamuru Waziri Mkuu alieleze bunge lakini akakumbana na maswali ya nyongeza mengi sana hadi akachanganyikiwa;
i. Kama ni kuhifadhi wanyama kwanini taarifa zinasema kuna mahoteli yanajengwa, ni ya kina nani? Nani karuhusu, kwa ruhusa ya nani, kwanini bunge halijui? au siku hizi bunge sio la wananchi?

ii. Kwanini kuna taarifa kuwa kuna ndege zinatua na kuruka kutokea mambugani huko? Ni za kinani? Serikali inazijua?

3. Mara mbunge mwingine akaibua hoja kwanini hadi leo wanafunzi wanakaa chini? Wagonjwa wanalala wawili kwenye kitanda kimoja? kwanini hamna dawa?

Basi maswali yakawa mengi, mawaziri wakashindwa kuyajibu, mwanasheria mkuu wa serikali hakueleweka

Ghafla nikamuona Spika amechukia kwa serikali kushindwa kutoa majibu ya kueleweka. Akawapa muda wa kujipanga tena na hapo hapo akaahirisha kikao cha bunge

Nikaja kushitushwa na zomea zomea za wabunge! Hapo ndo nikagundua kumbe naota.

Nimeamka najikuta toka nimelala hadi nilipoamka, tumevuka vituo viwili tu kwasababu ya foleni

Katika tafakari ya ndoto yangu, nikagundua maswala ya msingi ya nchi mara ya mwisho kuibuliwa bungeni ni kipindi Anna Makinda na Samweli Sitta wakiwa maspika kwenye mabunge yao

Nimejaribu kutafuta hoja yoyote iliyoibuliwa bungeni hivi karibuni yenye maslahi kwa nchi kama zilivyokuwa hoja za ESCROW, RICHMOND, na nyinginezo. Nimekosa!!!

Mwisho nikamkumbuka Gwajima aliyehoji nje ya bunge maswala ya utekaji halafu akajibiwa na mwenyekiti wake kwa kejeli "Gwajimanization" huyu mwamba ndo kashapotea tayari?
 
Back
Top Bottom