Ndoto yangu ni kuepukana na umasikini sijui nini kitatokea

Ndoto yangu ni kuepukana na umasikini sijui nini kitatokea

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2022
Posts
25,258
Reaction score
48,589
Katika dunia hii kila mtu amekuwa akiuchukia umaskini, na familia zisizokuwa na uwezo nazo zimekuwa zikifedheheshwa na watu matajiri wakiamini katika jamii hawana mchango wowote! Leo tunakutana na binti aitwae GORYANAH kwa kifupi muite (GORII )ni binti shupavu mwenye umri wa miaka kumi na saba anaishi na mamake mzazi pekee kwani Babake alipoteza maisha ikiwa bado ni binti mdogo.

Mamake huwa anauza mbongambonga analangua kwa wakulima kisha anampatia binti yake kutembeza mtaani huku yeye akiendelea kuchoma vitumbua nyumbani kwake ilimradi wazidi kuzichanga shilingi. Ndoto kubwa ya binti Goryanah aliamini ipo siku atauepuka umaskini katika familia yake kama ataongeza nguvu katika kupambana, fedhea kwa mamake kuitwa “msimbe” zitaisha endapo watapata pesa nzuri!



SONGA NAYO… SEHEMU YA KWANZA

Huku mtaani Goryanah alikuwa akizidi kutembeza mboga mboga! Jua nalo halikuangalia kuwa binti huyu anapitia wakati mgumu liliweza kuangaza zaidi misiri ya Moto uwakao.

Goryanah alifika kwenye mti mkubwa uliokuwa na kimvuli aliamua kutua hapo, huku akichukua chupa yake ya maji angalau anywe! Wakati akiwa anamalizia kunywa alisikia sauti ikimuita kwa nyuma ilibidi ageuke.

“” Mudy! Ulijuaje kuwa nipo hapa!

“”Dada Gorii!!” Siku ya leo naona biashara ni ngumu! Nimejaribu kutembeza matunda hutaamini watu hawanunui! Hapa nawaza labda twende stand angalau tutauza!?” Goryanah Alibaki akimtizama, Kisha alimpatia chupa ya maji anywe.

“” Utakuwa na kiu Sana mudy! Ila na wewe unisaidie, Mimi na njaa huwezi kunipatia hata ndizi mbili tu nikapunguza njaa?

“” Aaah! Dada Gorii” unajua huwa wanisaidia sana! Mimi nikikutana na wewe naomba uchukue tu! Kuhusu mama nitamwambia ziliharibika!”



Goryanah aliishia kucheka huku akichukua zile ndizi na kuanza kula, baada ya kumaliza kula ilibidi amgeukie.

“” Lakini mudy! Mi kwenda stand haitowezekana! Mimi nauza mboga mboga! Stand wamejaa wasafiri hawawezi kununua! Fanya hivi wewe nenda ukatembeze stand, Mimi naingia mtaani! Jioni tukutane hapa ili tuaangalie mahesabu Kama tutakuwa tumefanikiwa!

“” Sawaa! Kuwa makini Dada” halafu usipite zile chocho unazopitaga Kuna wahuni huwa wanakuwinda!”

“” Usijali, Goryanah ni binti jasiri! Anapambana na watu waovu siku zote! Kuwa makini hata wewe wasikunyanganye matunda pamoja na pesa.

Huku mtaani Goryanah alikuwa akizidi kutembeza mboga mboga! Kuna wamama walikuwa wakisukana walimuita akawa ameenda.

“” Wewe Binti wa Ma’ Goryanah! Naona unamsaidia mamako mlipe Kodi! Kazana make hii mabibo mtazidi kuhama hama muda wote!

Ni mama mmoja aliongea huku akizidi kuchagua mboga mboga, upande wa pili kulikuwa kunae kina mama wawili wakizidi sukana, walimtizama Goryanah Kisha walinong’onezana.

“” Huyu ndie binti yake! Mamake anatoka na mzee rajab Yule! Naskia ameungua! Daaah! Maskini binti wa watu atabaki yatima sahii tu! Sijui maisha ndio yalimfanya mamake amchukue Yule mzee apate kula!?”

Wakati wakizidi kuzungumza Goryanah hakuwasikia, muda wote alikuwa akihesabu pesa alizoziuza Kisha aliweka kwenye kimkoba alichokuwa akitunzia pesa!

Baada ya kumaliza mboga zote ilibidi arudi kwenye ule mti waliokubaliana watakutana! Alikaa huku akimsubili Mudy Kisha alitoa pesa huku akizihesabu, siku hiyo alikuwa amekusanya Kama elfu kumi na moja na Mia mbili, wakati akizidi kuhesabu Kuna kikaratasi kilianguka ilibidi akiokote Kisha alikikunjua akisome.

“” Huyu nae Kila siku haishi kuniletea vibarua! Eti anioe ili niepukane na kuungua jua! Ani ananionea huruma Mimi! Sa akifanya vile ndio ataniepusha umaskini vipi kuhusu mamangu!?”



Goryanah ilibidi acheke kwanza, huku akiichana ile karatasi! Kwa mbali ndio anamuona Mudy akija na beseni lake likiwa tupu huku akicheza cheza njiani.

“” Ooh! Afadhari hata Mudy nae kamaliza! Muone anavyocheza kwa furaha! Barabara kaifanya yake!”

Mudy baada ya kufika ilibidi akae kwanza chini Kisha alijilaza kwenye mchanga chali akibaki kutizama mti ule, alimuita Goryanah kwa kifupi.

“” Gorii! Unajua leo umeninenea vizuri! Hutaamini nimefika pale stand! Kuna wasukuwa watatu wamenunua ndizi zote!”

Goryanah baada ya kusikia vile ilibidi alale nae kifudifudi huku akikaa sitaili fulani ya kumsikiliza mtu kwa umakini.

“” Ni wasukuma watatu ndio wamenunua!?” Kwanini wawe wasukuma tu!?” Mudy alicheka huku akigeuka kumtizama Goryanah! Kisha aliongea..

“” Mamangu anaumwa ujue! Nimemuacha akikohoa muda wote! Sijui ni vumbi la shambani, majuzi kati tulienda kupalilia mihogo nahisi ni hili vumbi ndio limemuathili.”

Goryanah ilibidi akae huku akikumbuka kipindi yupo anauza mboga alisikia kwa mbali wale wamama wakimuita Msimbe(mwanamke aliyeachika au asiye na mme) mamake” Ilibidi ajikaze japo hapendi kusikia mamake akiitwa vile.

“” Tuondoke kwanza! Hata Mimi mamangu atakuwa akinisubili kwa hamu!”

Mudy aliinuka taratibu, walianza kutembea huku sitori zikiendelea njiani, lakini kwa Mudy alikuwa akitembea Kama akichechemea Gorii alimuona ilibidi amsimamishe Kisha alichuchumaa chini.

“” Ayaa! Nyanyua mguu wako nijue umekuwaje? Make watembea ukichechemea.”

Mudy baada ya kuinua mguu, alikuwa kajeruhiwa na chupa, Gorii ilibidi amkalishe chini Kisha alitizama upande wa pili aliona Kuna mgomba, alitabasamu Kwanza huku akikimbia kuchukua jani la mgomba akija nalo taratibu akilipikicha.



“” Hii inakata sumu! Baada ya siku tatu mguu wako utakuwa vizuri! Tutaendelea kufanya biashara tenaa!”

Mudy alibaki akimtizama Goryanah! Alimchukulia Kama Dadake na yeye alimchukulia Kama Kaka japo umri wao ulikuwa sawa! Mudy nae alikuwa akiishi na mamake pamoja na wadogo zake wawili wao walikuwa Darasa la tatu! Mamake ni mtu mwenye khari ya chini, anae genge anauza mboga mboga Nyumbani kwake, na muda mwingi alimtegemea Mudy. kwa ujumla maisha yake na Goryanah ni Kama yalifanana kutokana na kipato chao.

Baada ya Goryanah kumaliza kumhudumia alimwambia akanyagie mguu wake chini, ili dawa ifanye kazi vizuri. Goryanah Alibaki akimtizama Mudy jinsi dawa inavyozidi kumuingia, aliona uso ukianza kukunjamana ilibidi acheke kwanza.

“” Hivo hivo! Piga hatua ndio unazidi kupona! Kama vile unaumia ee!?”

“” Naumia “Gorii” siyo Kama natania hapa!”

“” Basi kaa tena!”

Ilibidi akae huku akizidi kuunyosha mguu wake misuri ikae vizuri, baadae alijisikia unafuu ilibidi amtizame kwanza Goryanah.

“” Goriii…!”‘

“” Vipi? Bado inauma!?”

“” Hapana..!”

“” Ilaa…!”

“” Wewe ni mzuri!”

Goryanah ilibidi asitishe kwanza zoezi lake make alikuwa akimchua taratibu kwenye mishipa ya miguu.

“”Aaah! Twende bhana! Unanitizama Sana! Au wataka nikuonee huruma! Mimi kwenye maisha ya mtu huwa naangalia afya yake tu.

Walianza kutembea taratibu huku Goryanah akipiga hatua ndefu, akifika mbele kidogo ilibidi asimame kumsubilia Mudy, make mwendo wake ulikuwa ni wa taratibu

“” Aaah! Mudy nawee! Unakuwa Kama sio mwanaume tu! Wewe huwezi ukatembea kwa uharaka tukawahi!?” Harafu tupo maeneo siyo!”

Mudy baada ya kumfikia ilibidi asimame nyuma yake make alikuwa amenuna. Goryanah ndio anageuka huku akipaza sauti, ndipo anakutana na Mudy uso kwa uso ilibidi hasira zishuke Kisha alicheka tu.

“” Hapo sawa’ make nilikuwa naenda kukufokea vibaya! Harafu leta hizo pesa ulizokusanya make Kuna vijana hapa nimeona mtu mmoja akirusha jiwe upande wa pili naona Kama wanashituana hivi! Hawa wanahitaji pesa, fanya hivi wewe kaa utulie.”
 
SEHEMU YA PILI-02

“” Lakini Gorii”

“” Tulia bhana.. ushaanza kuitana bila sababu..! Nipe haraka hizo pesa!”

Mudy ilibidi afanye vile, Goryanah alizihifadhi vizuri zile pesa Kisha alipaza sauti..

“” Kama mna nguvu si mjitokeze! Najua ni wewe Hammad na group lako! Harafu hivo vi barua unavokuwa wanitumia sivitaki.”

Mtu nne zilitokea chemba huku zikiwa na malungu zikiongozwa na Hammad Kama kiongozi wao.

Goryanah baada ya kuwaona ilibidi amfuate kiongozi wao.

“” Lakini Hammad.. unafanya haya yote ni kwasababu ya kutaka kunioa tu! Wewe ni mkubwa kwangu wanizidi miaka mitatu! Huoni Kama utafungwa na serikali Mimi sijatimiza miaka kumi na nane!

Hammad alimsogelea Karibu huku akimtizama machoni, Kisha alinyanyua mkono wake akishika nywele ya Gorii” iliyokuwa imefungwa nywele ya uzi, alifanya kunusa mkono wake Kisha alitema chini.

“” Wewe ni binti mrembo sana! Sema ni vile huelewi tu! Nikikuoa Mimi hutakuwa ukinuka jua!”



Goryanah ilibidi acheke kwanza Kisha alimshika kichwani akikagua nywele zake.

“” Kama ni kunuka jua, naona mwezi huu ndio mwisho! Huoni dalili za mvua zimeshaanza tayari!? Wewe ni msomi lakini hujui Kama dalili ya mvua ni mawingu!”

Hammad alitazama juu kwanza, kweli kunae dalili ya mvua alitabasamu Kwanza kisha alisogea Karibu alimnong’oneza sikioni.

“” Kesho ni birthday yako unatimiza miaka kumi na nane! Hiki kipinganizi Cha kusema utimize miaka kumi na nane! Kwasasa familia yangu naenda ishilikisha ije kuposa kwenu!”

“” Hata iweje… kamwe sitaolewa na wewe! Mimi kwasasa sinae mpango wa kuolewa nataka nitimize ndoto yangu kwanza, nataka mamangu aishi mazingira mazuri!” Hammad aliamua kuondoka na kikosi chake.

Huku kwa Goryanah Alibaki akimtizama Hammad mpaka anaishilia.

“” Gorii!! Kipi waenda kukifanya naona jamaa amekuganda kweli! Lakini hamna huwezi ukaolewa, wewe bado ni binti mdogo Sana!”

Gorii Alibaki akizunguka kutafuta namna ya kufanya

“” Sasa Mudy! Kuna kitu nimewaza! Unaonaje nikitoroka Nyumbani nikaenda kufanya kazi za ndani mjini! Nahisi hapo hataniona!”

“” Mimi je? Utaniacha na Nani?”

“” Aaah! Wewe utabaki na mama pamoja na mamangu nitakukabizi umtunze!”

“” Hapana sitaweza! Mamangu Mimi ananichanganya kumhudumia iweje mamako mzazi!”

“” Ooh uu! Sasa nafanyaje!?

“” Twende Nyumbani Kwanza!”

Huku Nyumbani Mamake Goriyanah alikuwa akifanya usafi, baadae Simu yake ilipigiwa ilibidi apokee Simu Huku akiangaza upande wa pili, ilionesha ni Simu ya Siri.

“” Nimekwambia nakuja! Ila ngoja Kwanza Gorii aje!

Muda huo Gorii anafika Huku akiwa na kelele akipiga beseni lake Kama ngoma.

“” Maamaa! Mwaka huu tunaondokana na umaskini! Leo nimeuza mboga zote.”

Mama baada ya kusikia vile alikata simu haraka Kisha aliiweka mezani.

“” Ooh binti yangu Gorii” kauli yako moja to ndio imebaki ni kuondokana na umaskini!”

Gorii alifungua pesa kutoka kwenye mkoba wake Kisha alimpatia Mama, Mama alipokea zile pesa Kisha alitabasamu Kwanza huku akiongea moyoni.

“” Hizi pesa haziwezi kuuondoa umaskini! Hivi ni vi shilingi tu! Lakini hongera kwa kuwa unazidi kupambana!”

“” Mamaa! Mbona kimya hujapenda? Halafu nina njaa..!””

Ilibidi waingie ndani wapate kula, muda huo Simu ya Mamake iliita, Gorii ndie alikuwa wa kwanza kuiona make ilikuwa upande wake, alichukua Kisha alitizama mpigaji aliona imeseviwa “” Mzee Rajab” ilibudi amtizame mamake kwanza huku akiwa na hasira.

“” Maamaa! Si uliniahidi hautawasiliana na Mzee Rajab!? Mbona anakupigia simu?”

Mama Alibaki na wasiwasi huku akimtizama binti yake, ilionesha hafurahii mahusiano yake kabisa na Mzee Rajab!

Goryanah aliamua kuondoka huku akimuacha mamake sebuleni, alielekea bustanini kunyunyuzia bustani!

“” Mama Kila siku ni yeye na Mzee Rajab! Mzee mwenyewe kachoka kweli nasikia anae TB mama kamganda kweli nahofia siku moja nitampoteza!”

“” Gorii”

Mama aliita alitoka kumfuata binti yake!

“” Wewe nenda tu! Nimemuona Mzee Rajab anakusubili kule mnakokutaniaga!”



Mama alipigwa butwaa Kwanza Kisha alitazama upande wa pili ndio anamuona Mzee Rajab! Akimpungia mkono ilibidi apunge na yeye!

Mambo yote Gorii alikuwa akitizama, aliamua kumruhusu mamake aende japo hakupenda kuona hivyo!

Baadae aliingia ndani huku akikusanya nguo zake na kuweka kwenye sarfet, baada ya kumaliza ilibidi ampangie mamake nguo kwenye begi huku akiamini siku akiondoka itabidi waongozane wote kwenda mjini na hapo ndio atamkomboa mamake kutoka kwenye mikono ya Mzee Rajab!”

“” Hapa Mama lazima umuache Mzee Rajab ukaanze maisha mapya mjini!”

Siku hiyo Gorii alibaki kumgonjea mamake asimuone tangu aende kwa Mzee Rajab! kiza kilianza kuingia ilibidi ajiandae kulala.

Lakini alikumbuka Kuna kiakiba alikuwa akikiweka chini ya kitanda ilibidi abinue Godoro aangalie! Alijaribu kukagua lakini hakuona mwisho kabisa aliona mfuko umeanguka chini aliuchukua na kuufungua! Alikuta Kuna makopo ya dawa Kama manne ilibidi afungue ndio anakuta kunae vidonge vikubwa! Alifunika kwanza Kisha alipiga kelele huku akisema…

“” Tayari mama ana TB ya Mzee Rajab!!!!?”

Mwisho alijikaza tena Ili afungue kopo la pili, baadae alifungua alifunga huku akiligeuza upande wa pili ndio anaona limeandikwa HIV ilibidi arudie tena japo alikuwa na elimu ya Darasa la Saba nayo ilimsaidia kuelewa.

Kwa ujumla alithibitisha mamake ni muathirika ilibidi akae chini kwanza huku akilia, baada ya kumaliza kulia wazo likabaki je atamuuliza Mamake Kama ni Muathirika? aliamua kurudisha zile dawa kwenye mfuko Kisha alirudisha sehemu yake!

Wakati anarudishia Godoro ndipo anaona ile pochi aliyokuwa akiwekea akiba ipo chini, aliifungua lakini hakukuwa na pesa tena, hapo hapo hasira ndio zilizidi kumjaa akiangalia ndio akiba alotegemea itawapeleka mjini wakapange chumba lakini mamake kaikwapua, akili ilimuijia alijua ni Mamake kaenda kumhonga Mzee Rajab kwasababu ni tabia yake amekuwanayo toka mwanzo.



Alichukua rungu huku akikata mtaa kuelekea kwa Mzee Rajab! Amweleze hizo pesa anazomuomba mamake atakuwa kapeleka wapi?

Baada ya kufika, Aligonga mlango ndipo anatokea Mke wa Mzee Rajab! Na yeye baada ya kumuona Gorii, ilibidi aingie ndani Kisha alitoka na Rungu na yeye huku akianza kumkimbiza.

“” Wasimbe nyie! Mamako amebaki kula pesa za Mume wangu halafu unakuja kumtafuta Mamako kwangu! Nakwambia na huyo mamako anaendeleza umalaya na waume za watu! Chakula chenyewe ni ugali mboga mboga! Jumlisha hivo Virus sahii tu unaitwa yatima kwa umalaya wa mamako, tena nakupa pole!”

Gorii” alikuwa akikimbia baada ya kusikia Maneno ya Mke wa Mzee Rajab ilibidi asimame huku akiamini kumbe kweli mamake ni Muathirika, hapo hapo alianguka chini akazima.
 
Mke wa Mzee Rajab alibaki akimtizama baada ya kuona kazima, aliamua kumuacha palepale.

Asubuhi yake ndio kunapambanzuka Gorii” aliinuka pale, aliangalia sehemu ile ndio anakumbuka tukio la Jana lilivokuwa, aliinuka taratibu akijikongoja kuelekea Nyumbani!

Baada ya kufika Nyumbani alikuta mlango umeegeshwa ilibidi aingie ndani akimtafuta mamake baada ya kufika alikuta Kila kitu kipo vururuvuru aliangaza upande wa pili ndio anashituka begi la mamake halipo, ilibidi aanze kukagua kila eneo vizuri lakini nguo hazikuwepo.

Alitoka nje huku akimwangaza mamake Kama atamuona lakini hakuwepo, alirudi tena ndani alitazama mezani ndipo anaona barua imewekwa pale ilibidi aisome.

“” Binti yangu Gorii” naomba unisamehe kwa maamuzi niliyochukua, najua unapambana ili Mimi mamako niishi vizuri, ninachokuomba binti yangu olewa na Hammad make familia yao wanayo pesa itakufanya uepukane na umaskini hata hilo jua halitakuunguza tenaa!”

Aliweka kituo kwanza huku akifikilia neno kuungua na jua ndio lililizidi kumchanganya zaidi, yeye alilichukulia Kama anaonewa huruma na wakati hapendi, Kuna maswali alikuwa akijiuliza mamake atakuwa wapi sahii.

Majibu aliona yatakuwa kwenye barua make alikuwa hajamalizia kusoma.

”’ Kuhusu Mimi mamako nimeamua kwenda mjini kutafuta kazi! Hata Mimi bado Nina nguvu za kupambana!”

Gorii” aliishia kusoma mwisho pale, akili yake iliwaza ni sawa kaenda kutafuta kazi jijini Dar! Na vipi Kuhusu hivo vidonge na afya yake itakuwaje?

Alianza kupaki nguo kwenye begi lake la mgongoni alikuwa ameliandaa muda mrefu atatumia kusafilia akienda mjini.

“” Mama nitakutafuta muda wote popote utakapoenda nami nitakufuata!”

Alifungusha Kila kitu kilicho ndani akifunga mafurushi, Kisha alifunga mlango kuelekea kwa kina Muddy.

“Gorii” mbona mapema hivi umebebelea begi! Leo unasafiri?”

Mamake Muddy Alihoji huku Muddy nae akitokeza nje.

“” Gorii” ndio wakimbia kuolewa na Hammad?”

Goryanah ilibidi amvute Kisha alimsogeza kunako banda la kuku aongee nae!

“” Muddy sikia!! Mama kaenda mjini kutafuta maisha, kaondoka na nguo zake! Ninachotaka kumwambia hii hapa funguo utakuwa waenda kupaangalia Nyumbani, naenda kumtafuta mama mjini ila nitawahi kurudi.”

“‘ Aaa a! Gorii” we baki uendelee na biashara mama atarudi tu! Kwani lazima umfuate!?”

“” Hapana Muddy! Wewe niamini Mimi nahisi mama bado hajafika mbali kwasasa! Halafu nahisi mamangu anae ugonjwa mkubwa huwa anameza dawa nyingi!”

Muddy alibaki akimtizama kwa mara ya kwanza alimkumbatia Gorii” alimkumbatia pia huku wote wakibaki kulia! Muddy alimuachia Kisha aliingia ndani alirudi na kiasi Cha pesa Kama elfu kumi.

“” Hii hapa itakusaidia kumtafuta Mama! Najua mjini bila hela huwezi kuishi!”

Goryanah alipokea ile pesa Kisha aliweka kwenye begi, alimuaga tena ili aondoke lakini alisikia sauti ya Mamake Muddy ilibidi ageuke kumtizama

Alimfuata na kumkumbatia, kumbe maongezi yote mama aliwasikia, Mama alifungua kitenge chake kwenye pindo alikuwa Kama na elfu Saba alimpatia huku akimtakia Kila la kheri katika Safari yake.

Huruma ya mama Kama mama ilimuuma Sana hasa akimtizama Gorii” ni binti mdogo hajui ataendesha vipi maisha akiwa mjini.

‘”‘ Mama unauhakika kweli Gorii” atampata Mamake” Lile ni jiji kubwa anaweza kutana na wahuni wakamlagai!”

Mama Muddy aliamua kumshika mkono kijana wake huku wakiingia ndani, ukimya ulitawala walibaki wakitazamana kwanza huku Kila mtu akionesha kukosa furaha Ghafra!



“” Mamaa! Hivi Mama’ke Gorii” anae magonjwa mengi, make kanambia anazo dawa nyingi anatumia.”

Mama alishituka Kwanza inaonesha alikuwa akifahamu maradhi ya Mamake Gorii”.

“” Wewe Nani kakwambia haya yote!?

“” Ni Gorii”

“” Gorii…!!?”

“” Kaniambia kipindi kaniita kule nyuma! Nahisi hizo dawa aliziona!

Mama alipata kikohozi kwanza, Muddy alimletea maji ya kunywa Kisha aliondoka kuelekea nyumbani kwa Gorii make alikuwa haamini kama kweli kaondoka.

Huku kwa Goryanah alikuwa tayari yupo kwenye Basi akielekea jijini Dar es salaam, siku hiyo alipata siti ya dirishani ilikuwa ni kukenua kutizama mazingira muda wote.

Majira ya jioni ndio wanaingia ubungo, baada ya kufika stand walishuka, kimbembe kilianza kwa Gorii” wapi ataenda? Alitizama vijana waliokuwa wakiuza vinywaji ilibidi awaulize sehemu ya kulala Kuna wakaka wawili walijitokeza huku wakimuomba wampeleke nyumba za wageni.

Gorii” aliwashukuru kwanza Kisha aliondoka nao walipita Kama mitaa miwili, walipofika kule mbele ilibidi wasimame kwanza huku wale vijana walirudi nyuma baadae walipeana ishara, muda huo huo wakamgeuka Gorii” mmoja alikwapua begi Kisha mwingine alichukua Simu wakaishia mtaani, Gorii” alianza kuwakimbiza lakini wapi, mwisho kabisa alichoka aliamua kukaa chini nakuanza kulia.

“” Haya yote ni kwaaajili yako Mamaa! Upo wapi kwani ona Mimi binti yako nazidi kuhangaika peke yangu!

Wakati amekaa alisikia king’ola kinapita ilibidi akimbie huenda Kuna msaada, ili kutokeza tu alikamatwa na police kwa uzururaji ovyo akawa amebebwa kwenye tenga. Walifikishwa police walipatiwa kichapo Cha nguvu kilimfanya azidi kuumia zaidi.

Kesho yake asubuhi walitolewa selo Kisha walianza kuhojiwa, wale wenzake wote walitolewa na ndugu zao ikabakiwa yeye akihojiwa.

“” Binti unaitwa Nani?

“” Gorii!!!”

“” Kwa kilefu nanii!!?”

“” Gorii Goryanah!””

“” Babako Goryanah ndie Baba?”

“” Ndie Mimi!”

Askari aliahirisha kumhoji kwanza make alijua binti hakunemo, Kuna Askari mmoja alimuuliza.

“” Unaishi kwa Nani au upo mtaa gani!?”

“” Sina makazi maalumu, siku nikimpata mama ndio nitajua naweka wapi makazi!

Kuna mama mmoja kati ya wale Askari aliamua kumchukua Gorii” ili amhoji vizuri, Gorii” na yeye alimwelezea Kila kitu, mama Yule alimuonea huruma alimuahidi atamsaidia kumtafuta Mamake.

Siku hiyo Gorii alichukuliwa kupelekwa kwa Yule mama, alimpatia hifadhi alikuwa akiishi kwenye jumba zuri la kisasa!

Ilipita Kama mwezi mmoja Gorii” alikuwa ameanza kubadilika rangi yake ya asili ilionekana vizuri make alikuwa ni maji ya kunde.

Kwaujumla alianza kuzoea kazi za pale Nyumbani huku akisaidiana na mabinti wenzake pamoja na mdada wa kazi, baada ya kumaliza majukumu yake aliomba ruhusa angalau akamtafute mamake tenaa make mji alikuwa tayari kauelewa, siku hiyo alitafuta Kila sehemu hakufanikiwa mwisho kabisa alirudi Nyumbani akiwa ni mnyonge.

Wakati anaingia ndani alikuta familia imechangamka, kumbe ni baba wa familia amerudi, siku hiyo aliwaletea binti zake zawadi, Gorii” alipofika sebuleni ilibidi asalimie kwanza Kisha alielekea kunako chumba chake, angalau akapumzike!

‘We wee wee! Ni Nani Wewe unaingia kwenye nyumba yangu halafu huna wasiwasi kabisa unazama tu, hebu njoo hapa haraka!”

Ilikuwa ni sauti ya Baba iliyomfanya asimame make ilikuwa Kama inamfokea, aligeuka ili amjibu lakini alikumbuka Kuna Maneno alikuwa akimwambia mamake.

“” Hupaswi kuzungumza na wakubwa pale wanapokukosea angalia kwanza chanzo ni Nini ndio ufungue kinywa chako.”
 
SEHEMU YA NNE – 04



“” Baba! Huyu anaitwa Gorii” ni Dada yetu kaletwa na Mama aje kuishi hapa!

Doreen aliongea na kumfanya Babake amtizame Kisha alimwangalia tena Gorii”

“” Basi nenda nitaongea na mama yenu, ataniambia ukweli!”

Gorii aliingia Chumbani Kwake yeye muda wote alikuwa akimuwazia mamake atakuwa wapi! Hata Yale maneno ya Baba alichukulia kawaida tu!

Majira ya usiku akiwa amelala mamake mlezi alifika kumgongea Ilibidi afungue.

“” Mama mbona usiku Sana upo hapa?

Gorii” Alihoji lakini mama aliishia kumshika kichwani akimtoa wasiwasi.

“” Kama utaendelea kukaa hapa! Hutampata mamako kwa uharaka, nimepanga kesho utaenda kukaa kwa rafiki yangu huwa anaishi yeye na binti yake mmoja watoto wengine huwa wapo shule! Nishamweleza Kila kitu nahisi atakusaidia kumtafuta Mamako hata Mimi nitakuwa muda wote nipo na wewe!”

“” Lakini Mama… Mimi Yule sijamzoea nimezoea familia hii, sijajua hata atanichukuliaje kwa hizi akili zangu!”

Mama aliishia kucheka kwanza, kweli binti yake akili yake anaijua vizuri anae wenge la nguvu aliamua kuondoka tu.

Gorii alikuwa na akili nyingi Sana alianza kuhoji kimya kimya mbona imekuwa ghafra Sana aambiwe ahame, alijiongeza Huku akijua chanzo ni mapokezi ya Baba mwenye nyumba ndiyo kaamua vile, aliplan siku ya kesho yake ataenda kuongea nae ili asiondoke tu.

Asubuhi kulipopambazuka Gorii” aliamka asubuhi Sana, alifanya kazi zote Kisha aliweka chai mezani, ile familia inakuja kuamka asubuhi wanashangaa kazi zote zimefanyika na chai ipo mezani.

Mama Ilibidi aingie Chumbani kwa Gorii” angalau ampongeze, baada ya kuchungulia kwanza Ilibidi abaki akimtizama Gorii anavyofanya maigizo akitembea tembea chumba kizima.

“” Aaa! Hapana, hapo nimekosea.. nitamsalimia kwanza Kisha nitamletea jusi anywe,,, aaa… Hapana! Nitamsalimia Kisha nitamwambia, “” Baba I’m sorry! Jana nilikuwa na mawazo nilipokuwa napita sikukuona vizuri! Ndio maana nikakupita pasi pasipo kukuongelesha! Kwahiyo nisamehe sitarudia halafu nipe adhabu yeyote na sio nikakakae kwingine! Nivumilie nimpate mama kwanza!”

Goryanah alimaliza kuongea Kisha alijipigia makofi akiamini mtihani kaufaulu! Lakini alisikia upande wa pili Mama akimpigia makofi, upande mwingine tena ni Doreen alikuwa akichungulia dirishani alicheka na yeye, Kisha alizunguka akaingia ndani.

“” Mama lakini kwanini usimuache Gorii” akae tu hapa Nyumbani unajua tumemzoea Sana! Halafu leo kafanya kazi zote mwenyewe, nyumba inavutia ujue! Si baba ndio kasema Gorii” hamuamini lakini sisi tunamwamini mama, acha akae tu.”

Kwa maelezo ya Doreen ndio yalimfungua macho Gorii” alijua kabisa kumbe shida ni kutokumuamini tu, kwanza alishuka kitandani kama karushwa na remote, huyo nduki Hadi sebuleni baada ya kufika alimuakia Babake kwa heshima, muda huo alikuwa ananyanyua kikombe anywe chai, Gorii” alimsitopisha kwanza Kisha alichukua kile kikombe akanywa chai iliyokuwemo, baada ya Hapo alishusha tenaa huku akimpatia Mzee anywe..

“” Samahani Baba! Wewe kunywa tu! Najua huniamini ndio maana nimefanya kunywa chai yako kabla usije ukanisema nimeweka sumu!”

Doreen na mamake walibaki kucheka tu, make vituko vya Gorii” Kila kukicha vilikuwa haviishi.

Lakini Baba Yule alibaki akikitizama kile kikombe, kwa roho mbaya alikitamiza chini Kisha alisimama aondoke lakini Gorii” aliwahi akamshika mkono huku wakimtizama jicho kwa jicho.

“” Lakini Baba!! Nimekosea Mimi na sio kikombe hiki! Hata kyenyewe kimeumia ndio maana kimepasuka! Halafu ulipokitupia sio sehemu salama muda wote kinaweza kukuchoma wewe kwa hasira kilichonacho.”

Baba alimtiza tena Gorii” Kisha alimtoa mkono uliokuwa umeshikilia mkono wake, alimpatia ishara huku akimsontea kichwa chake kwamba hamnemo.

Gorii hakujali, aliinama akawa ameokota vile vipande vilivonjika na kwenda kuvitupa kwenye ndoo ya uchafu!

Mama alimuonea huruma Sana huenda anapitia wakati mgumu, kuliko hata yeye lakini binti wa watu hajali kuhusu hilo, Ilibidi amfuate Kisha aongee nae.

“” Gorii jiandae basi tukamtafute mamako! Kuna taarifa zimetoka Kuna wamama wajane wanahitaji msaada!

Gorii kwa mamake tena! Dakika tano ni nyingi alienda kubadilisha nguo siku hiyo alivaa gauni lake Zuri kweli Kisha waliondoka.

“” Huenda Mamangu anapitia wakati mgumu kwasasa! Atakuwa kaenda kuomba msaada kwa watu wenye roho nzuri!” Gorii alimuuliza Ma Doreen!

“” Usijali siku tukimpata ataishi vizuri!”

Walielekea sehemu Kunae tajiri mmoja alikuwa maarufu Sana, alijitolea kugawa msaada kwa watu wasiojiweza! Gorii baada ya kufika pale aliuliza wale walinzi Kama Kuna usajili wa jina la mamake.

“” Mamako anaitwa Nani?

“” Nelisha Magai!”

Muda kidogo mlinzi alimwangalizia kwenye orodha Kisha alirudi na majibu kwamba hakunae jina hilo.

Gorii alivunjika moyo Alibaki amekaa huku akijawa na wasiwasi Sana huenda hata mamake alikufa muda mrefu! Ma Doreen alimfuata Kisha alimshika mkono huku akimpeleka kwenye gari, siku hiyo hakutaka kumpeleka nyumbani make nako hakukaliki. Aliondoa gari yake kuelekea kwa huyo rafiki yake( Mama Rich ) angalau wapate chakula kule.

Baada ya kufika Gorii” alibaki kwenye gari akiamini mamake anaenda kuonana na mtu Kisha angemkuta kwenye gari, lakini mama alimuomba ashuke kwenye gari Kisha waondoke wote!

Baada ya kushuka Gorii” alibaki akitizama jumba lilivokuwa kubwa halafu linae wafanyakazi wengi alibaki kushangaa, walipitiliza moja kwa moja Hadi sebuleni.

Kuna mama aliingia sebuleni, kwa muonekano ilionesha ndie mama mwenye nyumba, lakini alikuja ameambatana na Bibi mmoja akiongozana nae walikaa kwa pamoja, Gorii ilibidi awasalimie Kisha alikaa kimya, waliletewa kinywaji huku msosi ukizidi kuandaliwa.

Kwa Gorii muda wote alikuwa akimtizama Yule Bibi Kisha anampatia ishara kupitia mkono baadae anacheka, Ma Doreen alimuona Bibi anacheka ilibidi amtizame anaecheka nae, ile kumtizama Gorii” akavunga Kama hakuna kinachoendelea.

Ghafra Kuna kijana aliingia huku akipiga makofi kuelekea kwa Bibi yake aliongea.

“” Naona Bibi amepata mjukuu wa kufanana nae! Muda wote anacheka nae!”

Wote walimtizama Bibi lakini Bibi alibaki kufurahia zaidi, Gorii” ndio akauchuna maziwa.

“” Rich wamaanisha Nini? Mjukuu yupi huyo!?”

Mama Rich ndio Alihoji, make Rich pia ni mwanae.

Rich alifanya kumsonta Gorii” kwa kidole.

“” Yule pale mjukuu!”

wote waligeuka kumtizama Gorii”

“” Hapana sio Mimi! “Mjukuu wa Bibi kakosea”

Ilibidi wacheke kwa pamoja huku wakizidi kumtizama Gorii”.

“” Mama Rich.. nilikwambia Gorii” ninaekaa nae ndio huyu! Yaani muda wote haishiwii vituko! Huwa ni mcheshi Sanaa!”

“” A aaa!! Lakini mama Mimi sitakaa hapa! Lazima turudi wote Nyumbani!”

“” Gorii” familia niliyokwambia utakaa nayo ndio hii, huoni wanavyokupenda!”

“” Haikuwa makubaliano yetu..! Uliniambia ninae mama mmoja na binti mmoja mbona ni wengi hivyoo!?”

“” Nilikwambia vilee lakini nilitaka kukuondolea hofu ila ndio hii!”

Bibi Alisimama huku akimfuata Gorii aseme nae, ile kusimama mguu wake ulikuwa umekufa ganzi, alitaka kuaanguka lakini Gorii” aliwahi kumdaka, mpaka watu wote wakabaki kushangaa, “” mbona ni binti wa ajabu Sana!”

“” Sorry Bibi!!” Huku akimkalisha taratibu kwenye kiti.

“” Mama twaweza kuondoka sahii! Itakuwa Doreen anatuulizia Sana!

“” Lakini Wewe mjukuu wa Bibi! Si ubaki tu! Tulisikia Kuna binti ataletwa hapa! Angalau awe anakaa na Bibi kumliwaza make Bibi yangu ni mgonjwa.

Rich aliongea, alimfanya Gorii” amtizame kwanza huku akifikilia.

“” Kumbe kukaa hapa ni kwaajili ya Bibi na si kumtafuta Mamangu!? Wanaleta utani hawa.

“” Gorii” mwelewe Basi kakako! Hii familia ndio itakusaidia kuitafuta familia yako pamoja na Mama.

Gorii” Alisimama kwanza Kisha alizunguka huku akitizama mazingira ya pale Kama Kuna usalama kwanza, Kisha alimsogelea Mamake Rich akamuuliza.

“” Je, utanichukulia Kama Mtoto wako Kama Ma Doreen anavyonichukulia Mimi!?”

Mama Rich aliishia kumshika shavu Kisha alimkumbatia.

“” Ninajua thamani ya kuwa mama!”

Aliongea maneno machache tu, lakini ndani yake yalikuwa na maana nzito.

“” Kwahiyo utabaki na familia hii? Familia yetu inajulikana Kama familia ya Mishoki house! Je upo tayari kuishi na hii familia?”

Gorii alikuwa Kama haelewi alimtizama Bibi upande wa pili muda wote alikuwa akimpatia ishara akubali, akikataa atajiua.

Kabla hajakubali alimsogelea Bibi kwanza Kisha alimshika mkono huku akipaza sauti.

“” Kwaajili ya Bibi nitakaa hapa!”

Wote walipiga makofi kumpongeza kwa maamuzi aliyochukua.

Mama Doreen ilibidi akae nae pembeni angalau amuachie maneno kadhaa yatakayomjenga.

“” Gorii! Najua Wewe huwa una moyo safi, naimani kupitia Wewe familia hii utaifanya iwe na furaha Kama ulivyotufanyia sisi! Sina maneno mengi ya kuongea make najua nidhamu huwa unayo! Pia ni mtu wa kujiongeza! Kuhusu mama tutampata tu, kikubwa makazi kwanza ndio kitu muhimu, hata mama naamini yupo anatafuta makazi ya kukaa, kana Wewe umepata hifadhi hata mama nae kashapata hifadhi amebakiza jambo moja tu, nikukutafuta Wewe!”

Gorii” alibaki akidondosha chozi Kisha alimkumbatia mamake kwa furaha kabisa! Ni mama mwenye upendo wa dhati, alihisi hata huo moyo utakuwa ni Mamake.

Baada ya kumaliza maongezi walirudi sebuleni, Gorii” alitembezwa nyumba nzima ajue mazingira pia alipatiwa chumba chake kwaaajili ya mapumnziko.

Mwisho kabisa walikaa mezani wapate chakula Cha pamoja. Mama Doreen aliomba kuondoka huku akimwahidi Gorii atamletea nguo zake.
 
SEHEMU YA TANO

Ilipita Kama wiki mbili Gorii” tayari alikuwa amezoea mazingira, tangu akae pale hakuona dalili yoyote ya kutengwa zaidi familia ya Mzee Mishoki ilizidi kumpenda hasa katika uwajibikaji wa kazi, pamoja na kalama aliyojaliwa ni uchesi na utoto mwingi uliojaa akili.

Leo Mrs Mishoki alimkuta Gorii” akiwa chumbani Kwake akiwa na picha ya Mamake, baada ya kumuona Mama ilibidi aifiche ile picha ila mama alikuwa amemuona muda, alimua kukaa kimya kama hajaona

“” Gorii” Unajua leo tunao wageni! Kaka zako wawili wanakuja likizo! Naomba twende wote sokoni tukatafute mboga!”

“” Na Bibi je?”

“” Unavompenda Bibi yako! Kwani wamkimbia?”

“” Gorii alitabasamu huku akisimama waondoke.”

“” Wapi tenaa waenda!?”

“” Ngoja nimchungulie Bibi kwanza! Huenda anataka zawadi ya kutoka nje!?”

Muda huo Rich nae alitokea huku akimuita Gorii”.

“” Gorynah”.. muda bhana! Leo hujui kakazangu wanakuja! Humu ndani sikuzote Mimi ndie dume pekee! Sahii nitakuwa situmwi ovyo! Kina Kaka nao watawajibika.

“” Aaa..! Na wewe Ka Rich..!! Nilikuwa namuaga Bibi kwanza! Halafu kumbe na Wewe waenda!?”

“” Unaweza kubeba mizigo yote mkihemea!?”

Mama ilibidi awakatishe make wakianza kuhojiana huwa hawamalizi.

“” Nyie watoto tuondoke bhanaa!”

Wakiwa sokoni walihemea vitu vingi, Gorii” na Rich ndio walikuwa wakusaidiana kubeba na kuweka kwenye gari.



Baada ya Kumaliza ilibidi waanze kurudi. Wakiwa njiani Goryanah ” alimuuliza Mamake Rich.

“” Mama mbona vitu vingi hivyo umenunua si vitaharibika? “” Yaani huko kwetu huwa twaenda na mfuko wa magufuri wa mia mbili vitu vyote vyatoshea, siku nyingine huwa nakimbia gengeni bila mfuko naleta nyanya, kitunguu, ndio kwisha hapo!

“” Hi ni familia kubwa, kukaa twaenda kuhemea kila siku sio vizuri! Huwa twahemea vitu vyakukaa navyo siku nyingi! Muda mwingine ni mazingira tu ndio unachagua kipi ufanye!”

“” Aaah!! Ndoo… maaana!” ” Kule kwetu unajua hata tukipika mboga huwa ni moja tu! Huku Sasa yaani vitu vingi mpka huwa nashidwa nianzie wapi!? Ila Mimi vyote huwa naonja!”

Mama ilibidi acheke tu… Mtoto hajui kuvunga.. Rich nae aliamua kumvuta nywele kwa nyuma huku akimcheka.

“” Halafu Rich umenikumbusha! Utampitisha dadako saluni leo mpendeze, si unamjua Jolvin huwa hapendi uchafu ataanza kuwasema huyoo!”

“” Jolvin… Itakuwa ni huyu mjukuu wa Bibi muda wote huwa anamuongelea Sana! Jolvin, Jolvin… Oooh! Kwani yeye msafi?

Gorii Alihoji, lakini Rich aliwahi kumjibu.

“” Ni msafi huyo! Itabidi leo nitaenda kukuonesha chumba chake ukijue! Yaani kila kitu cheupe pee!”

“” Haaaa! Atakuwa na majini huyo, kijijini kwetu mtu akiwa msafi zaidi! Itakuwa anakaa na jini Safi.”

“” Wewe Gorii” tulia Basi akikusikia hivyo kakako atakuuliza!? Acha niwaache saluni muwahi kurudi Sasa

Mama aliwashusha pale, Kisha aliwaachia pesa kidogo watumie. Ile kushushwa tu! Gorii” alijinyosha huku akitizama mji ulivyojaa majengo mazuri alicheka kwanza Kisha alishusha pumzi ndefu!



“” Unajua Nini Rich… Afadhari leo tutembee tembee,, yaani kwenu kila ukitoka ni kwenye gari! Twende Tandale kwanza..! Huko Kuna saluni za bei nafuu!”

“” Goryanah umeanza… Mama kasema tuwahi kurudi! Mimi huko uswahilini sitoenda!”

“” Hutoenda wakati pesa nimekabithiwa Mimi! “” Ayaa hiace hiyo hapo ya Tandale mi napanda ka unabaki.. we baki”

Rich hakuwa mjanja tena ilibidi akubali! Make hata pesa ya nauli hana Walifika Tandale wakawa wameshuka.

“” Twende kwenye hio saluni.. huenda wanae bei nzuri.

Baada ya kufika Gorii” aliulizia….

“” kusuka yebo bunda tatu shi ngapi?”

“” Elfu kumi na tano tu!”

“” Hapana hela nyingi mno hiyo!! Nikajua elfu nane!!”

“” Dada.. nenda kwenye saluni yako uliyoizoea naona umekosea saluni.

Msusi mmoja alimjibu, make Kama anamletea mazoea kwenye kazi yake.

Huku kwa Rich yeye hana mbavu, make alikuwa akisikiliza jinsi wanavyoelewana bei.

“” Vipi mbona unacheka.. Ndio umefurahi!? Ila wana bei kubwa mno!

“” Gorii” nacheka kwasababu unaulizia kusuka yebo,, nywele ya kishamba hiyo hata demu wangu hawezi suka hiyoo..!”

“” Ooh! Kumbe Rich huwa unafanya tabia mbaya! Kumaliza form four tayari unae dem?”

“” Wewe unashangaa Mimi!!?’ ” wakati ninae rafiki yangu anae Mtoto!?”

“” Itakuwa huyo ndie kakufundisha tabia mbaya! Ndio maana upo kwenye mahusiano ukiwa na umri mdogo!”



“” Kwani Wewe bado!!?”



“” Bado Nini!? ” Mimi Sina tabia Kama zako!”

Rich alibaki kumcheka kwanza Kisha alimshika sikio.

“” Wewe si una miaka Kama yangu..? ” ushakuwa mbona!!”

“” Twende bhana Saluni nyingine naona wataka kuongea!!”

“” Nijibu kwanza…. ndio twende.. Ukipata mchumba huwezi olewa! Make tunalingana kila kitu!.

“” Unafurahisha Sana Rich, Mimi nawaza nipate pesa! Mamangu nimjengee nyumba nzuri! Wewe wazani siku zote Mimi nitaendelea kuishi kwenu?”

Rich ilibidi akae kimya kwanza, Huku akimfikilia Gorii” atakuwa ni muongeaji Sana lakini kutimiza malengo yake ni changamoto kwa mtazamo ule hata hiyo pesa ataitoa wapi?

Walielekea kwenye saluni moja ilibidi akubali kutumia gharama ya ishirini na tano, Rich alimshawishi abadilishe mawazo ya kusuka na sio yebo tenaa!

Baadae walirudi Nyumbani huku wakiwa wamenunua vyakula vya mtaani, Goryanah alipitiliza moja kwa moja Chumbani kwa Bibi, alitoa vile vyakula akaviweka mezani.

“” Bibi! Leo nilienda kuzurura huko nje! Nimepata vyakula vya mtaani kwetu! Nikaona nikuletee wewe kama unavipenda Karibu tule!”

Rich aliingia, Kisha alikaa mezani nakuanza kushambulia ile mihogo, Bibi nae akasema awee!! Sio ya kukosa alianza kula huku wakifurahia kwa pamoja.

“” Wewe Rich! Mbona unaivuta vuta hivyoo!?”

‘” wewe nifate kwanza! Si nilikwambia nitakuonesha chumba Cha Jolvin.”

“” Ooh! Nipeleke kwa huyo Kaka mwenye vitu vyeupe!”

Waliongozana hadi kwenye hicho chumba baada ya kufika, Rich alifungua mlango! Kweli chumba kilikuwa kinavutia, kitanda kilitandikwa vizuri!

“”Waoo!! Chumba kizuri sana

Goryanah aliongea huku akijitupia kitandani.

“” We wee!! Dada wa kazi kamaliza kufanya usafi sahii tu halafu Wewe wavurugua kitanda! Hivi kumbe wajua kingeleza!?”

“” Na ningesoma Wewe huniwezi kwa kuongea kingeleza!”

“”Ayaa tandika vizuri tuondoke! nimesikia wamefika Airport! Tusikutwe humu.

Walifika sebuleni huku Gorii” aliingia jikoni kuwasaidia wapishi, baada ya kumaliza walileta mezani!

Muda huo Jolvin alikuwa akiingia huku akiwa na wenzake wawili wakipiga stori!

“” Hodi humu Ndanii!!!”

Jolvin alibisha hodi Kisha akafatia Esau na Joely.

“” Daaah! Wanangu mmependeza kweli..!”

Mama alifika kuwapokea huku akifatia Rich, Kakake walimpenda Sana hutaamini wote walimkumbatia huku wakielekea sebuleni.

“” Bibi yupo wapi maama!?”

Jolvin Alihoji huku akijaribu kumuita Bibi yake.

“” Atakuwa bafuni, si unamjua Bibi yako anataka arudi ujana Kama wewe!”

“” Goryanah… Chakula bado tu! Mje msalimie wageni kwanza.

Mama Aliita.

Neno Gorii” lilikuwa jina geni kwa Jolvin, Esau na Joely ilibidi watoe macho kutizama Gorii” mwenyewe anaeitwa.

Wakati wakiwa jikoni wadada wa kazi wote walishadadia Gorii” apeleke kinywaji kwanza kwani wote wanamuogopa Jolvin, muda wote ni kusodoa, wakati mama anaita Goriii ndio alikuwa akimimina Juice kwenye Grass baadae alifika sebuleni na kuweka mezani.
 
SEHEMU YA SITA



Baadae aliinua kichwa kumtizama Rich make alimkanyanga mguuni, muda huo alikuwa amewekwa kati na kaka zake.

Goriii ilibidi amtizame kwanza, Kisha alimaliza kuwatizama na wale wengine Kisha aliongea..

“” Wajukuu wa Bibi wanamfanana Bibi yao kweli! “” Oooh sorry Sijawasalimia… Shikamoni wajukuu wa Bibi!””

Jolvin aliishia kumtizama Gorii” huku akimshangaa, lakini Esau na Joely wao waliitikia huku wakimtizama Gorii” alivyomcheshi.

Muda huo Gorii ndio anagawa juisi kwa Kila mtu alipofikia kwa Jolvin Alibaki kutizama ule mkono ulivyoshika Glass, Kisha alipokea ile Glass akaiweka chini huku akimtizama Gorii”.

‘” Your name is…!!!!?”

“” Gorii” Goryanah!!”

Rich ilibidi aingilie kati make Kaka anakoendelea sio kuzuri!

“” Gorii” nenda Basi ukasaidiane na wadada wa kazi mlete chakula!”

Gorii” alivyoondoka, Jolvin nae alimfuata njia ile ile anakoelekea, kumbe alikuwa akiishia chumbani kwa Bibi.

“” Wewe Kaka White! Mbona unatembea nyuma yangu!?”

Jolvin hakujibu zaidi alikata Kona kuingia mlango wa pili ambao ni chumba Cha Bibi.

‘” Bibi! Hutaki kumuona mmeo leo!? Ndo umejifungia.

Chumba kilionekana kuwa kimya, Jolvin ilibidi akae kwanza lakini kwa pembeni aliona Kuna mihogo ya kukaagwa, aliangalia upande wa pili hamna mtu alichukua mhongo mmoja akaula kwa uharaka Kisha alitulia.



Katika pita pita za Gorii” alikuwa akija ndani kumkalibisha Bibi yake chakula, aliingia kimya kimya bila kupiga hodi ndio anamkuta Jolvin akimalizia mhogo wa pili! Ilibidi kwanza acheke huku akichukua sahani ili kuhakikisha Kama bado Kuna mihogo.

“” Ooh!! Wewe ndie umekataa juisi nilokuletea halafu unakuja kula mihogo ya Bibi, Ngoja nikamwambie Bibi umekula mihogo yake!”

Gorii” alitoka haraka ili akaseme lakini Jolvin alimuwahi! Kisha alimsogelea Karibu huku akimziba mdomo.

“” Wewe ni Nani kwanza katika nyumba hii? Umeleta vyakula vya huko nje hata havijachunguzwa! Wataka Bibi yangu ale! Hujui anae magonjwa ya moyo!””

“” Oooh! Wewe Bibi yako anae magonjwa ya moyo! Vipi kuhusu mama yangu make nahisi anae magonjwa mengi Sana! Mimi najitahidi kumuweka sehemu nzuri Bibi yako! Sijui hata Mamangu huko aliko anaishi katika mazingira gani tu?”

Wakati wakiendelea kuongea kumbe Bibi alikuwa ametoka kidogo, muda ule anarudi anawakuta wapo kwenye position tofauti kabisa, aliaanza kuwatizama make muda huo kila mtu alikuwa akimtizama mwenzake kulingana na uzito wa maneno aliyoyatoa, Jolvin aliamua kumuachilia baada ya kuhisi Kuna mtu.

“” Bibi nakusubili Wewe tu! Nataka uniambie ulienda wapi kwanza! Au ushapata mwingine!?”

Jolvin aliongea huku akivuta kiti akae. Gorii” yeye aliamua kuwapisha!”

Bibi Alibaki akimtizama Gorii” jinsi anavyoondoka! Mpaka aliingiwa na wasiwasi hata Mjukuu wake alilitambua Hilo.

“” Bibi! Kwani Gorii” ni mtoto wa Nani!?”

“” Masikini Gorii” Unajua Sipendi kumuona anakosa furaha Mjukuu wangu! Yaani muda wote huwa anapenda kukaa Karibu na Mimi! Hata Kama akiwa na huzuni hufanyia chumbani Kwake ila akirudi huku ni furaha tu!”



Jolvin aliamua asimhoji kwanza kuhusu Gorii” make hata akili yake ilikuwa mbali!”



Huku kwa Gorii” aliingia jikoni kuandaa Juisi ya Bibi, baada ya kumaliza aliweka kwenye Grass alipeleka chumbani kwa Bibi, alimkuta Jolvin yupo kwenye sitori nzito na Bibi! Aliwaza arudi lakinii aliangalia saa iliyokuwa ukutani! Alijua ni muda wa Dawa.

“” Kaka White! Nipe nafasi kwanza nimpatie Bibi Dawa!”

Jolvin ilibidi akae pembeni akiangalia nesi anavyomhudumia mgonjwa!

Gorii” alimaliza kumpatia dawa Kisha alimsogelea Bibi yake sikioni akamnong’oneza.

“” Kaka White! Kapita na mihogo yako!”

Bibi ilibidi amurudishe kwanza Gorii” chini Kisha alimuuliza Jolvin.

“” Ile tabia yako ya kula mihogo kumbe bado unayo!?”

“” Mhu mhuu… Mi miimi!!?”

Goryanah ndio alicheka huku akichukua sahani ilokuwa na mihogo akimuonesha Jolvin.

“” Ni wewe Ndio! Halafu umenitishia nisiseme kwa Bibi!”

Bibi ilibididi acheke tu, Kisha alimvuta masikio Jolvin akimuomba aombe msamaha kwa Gorii” kwa kumtishia.

“” Bibi kabla sijaomba msamaha! Nayeye anitake radhi! Kwanini ananiita Kaka White na si Jolvin!?”

Gorii” ilibidi acheke kwanza Kisha alijibu.

“” Mfano Mimi naitwa “Gorii” “Goryanah” Ila Wewe nimeona waitwa Jolvin huna jina jingine, ukiwa kaka White itapendeza Sana, kwanza wewe msafi, chumbani kwako kumejaa nguo nyeupe! Namimi nimekuita “Kaka White” kwasababu unapenda nguo nyeupe!”

“” Gorii” chumbani kwangu tenaa!? ” Inamaana umeingia…? “Hivi Wewe ni Nani kwanza katika Nyumba ya Mishoki!?”

Rich aliamua kuwafuata chumbani baada ya kuwasubili muda mrefu mezani!

“” Kaka, Bibi.. tunawangoja mezani, chakula kinapoa!

Maada iliishia hapo! Ilibidi waelekee mezani, lakini Jolvin swala la Gorii” kuingia chumbani Kwake alikuwa akiendelea kulitafakari! Mpaka anamaliza kula.

Baada ya kumaliza kula ilibidi Maama awaite wanae kwa pamoja alifanya kuwatambulisha vizuri kuhusu Gorii” make walikuwa hawajamuelewa kwa undani! Baada ya utambulisho kila mtu alikuwa kawa mwenyezi hata Gorii” alitambulishwa kuwa wale ndio Kaka zake! Make mama alikuwa anao watoto wa kiume tu na wao ni watatu Rich ndio wa mwisho halafu Esau, Jolvin wamefatana! Na Joely ni mtoto wa ba mkubwa! Wote wapo chuo wanasoma.

Asubuhi kulipopambazuka Kama kawaida Goryanah aliamka asubuhi kufanya kazi za ndani akishilikiana na wadada! Baada ya kumaliza waliweka chai mezani huku kila mtu ni kujisevia.

Majira ya mchana Gorii” alikaa bustanini akipunga upepo! Mwisho kabisa aliamua kujilaza kwenye nyasi, usingizi nao ukawa umemchukua! Ile anakuja kuamka anamkuta Rich kakaa pembeni yake huku akiwa na note book ya Gorii” muda mwingi alizoea kumchora mamake huku akiandika maneno mengi, mama nimekumisi, mama hivi uwapi? Lini nitakuona?”

Gorii” ndio anaamka huku nywele zake zimejaa majani alianza kujitengeneza huku akitumia kioo Cha Simu ya Rich. Rich ilibidi amsaidie kumtolea.

“” Nishakwambia umefikia muda wa kuwa na mchumba ili awe anakutolea Kama hivi na sio Mimi kakako!?”

“” Wewe nae! Kunitolea tu Hadi niwe mchumba wako! Sa mbona unanitolea Sasa na si mchumba wangu!?”



“” Kuna siku nitakuoa! Kama utakosa mtu wa kukuoa!”

Goryanah ilibidi amsine mguuni kwanza Kisha walianza kurushiana majani wakikimbizana, lakini kwa bahati mbaya wakati Gorii” anarusha yalimuangukia Jolvin kichwani na mengine usoni.

Jolvin ilibidi asimame kwanza make alikuwa haoni, alinyanyua mkono wake kwanza ili afute kwa bahati mbaya tenaa Simu yake ilianguka chini, Rich baada ya kuona vile ilibidi akimbie huku msala ukibakia kwa Gorii’‘
 
SEHEMU YA SABA

Gorii” alitizama pembeni alimuona Esau, Joely wapo busy kusoma, yeye akazani hawajaona kumbe walivunga ili waone kinachoendelea pale.

“” I’m sorry Kaka White! Ni mis understanding tu! Hata hivyo Simu haijapasuka.

Jolvin alikaa kimya huku akiwa amefura hasira! Akifikilia mambo anavyoyafanya kitoto kitoto halafu analeta kuongea kingeleza.

Gorii” hata hakujali alinyanyua mkono ili aendelee kumfuta lakini Jolvin aliurudisha ule mkono akiukunja. Gorii” ambavyo hasikiagi alirudia tena kuweka huku akimtolea, Kisha mkono wake wa pili alimshika akimsogeza sehemu nzuri amkalishe huku akiendelea kumtolea majani, baada ya kumaliza alijipigia makofi huku akimuomba afungue macho.

“” Kaka White! Ila Mimi ni Bora kuliko hata Rich aliyesababisha matatizo, halafu sahii kakukimbia!

Huku kwa Esau na Joely! Walibaki wakicheka kimya kimya, Rich nae hakuwa mbali alikuja kuungana nao.

“” Yaani leo nilikuwa nakula Kofi moja mpaka kuanguka! Najua Gorii” akitoka hapo atakuwa na hasira na Mimi! Lakini angalau kalisovu hilo!”

Esau na Joely walicheka Kisha walimpatia Ishara Rich ajifiche make Jolvin anamuangaza muda wote!

“” Daaah! Nimekwisha kumbe bado natafutwa tu!?”

Jolvin alimuona Rich anavokimbia alimuita kwa sauti Kali arudi.



Ilibidi Rich aje taratibu huku mikono kaiweka nyuma alikuwa mnyonge kweli, Gorii” alimtizama akawa amegundua hilo! Jolvin alinyanyua mkono wake ampatie Kofi lakini Gorii” aliudaka Kisha aliuelekeza shavuni kwake.

“” Kaka White…!! Wewe huwa hujui bahati mbaya!? Unazani Mimi na Rich tulipanga tuje tukumwagie majani usoni? Tulikuwa kwenye michezo wewe Ndio ukatokea ukapita mbele yetu! Hiyo si bahati mbaya tu!? Basi nipige Mimi make mikono yangu ndio ilikumwagia nyasi!”

Jolvin ilibidi atoe mkono Kisha alishusha pumzi ndefu akiwa ameshikilia meza waliokuwa wakiitumia Rich na Gorii”

Esau na Joely baada ya kuona imekuwa msala ilibidi wasogee karibu, walimruhusu Rich na Gorii” waondoke Kisha wao walibakia na Jolvin.

“” Hapana amezidi huyu Mjukuu wa Bibi! Muda wote hasira! Sijui Nani kumuuzisha kiasi hicho!

Gorii” alikuwa akilalamika huku akiwa na Rich, ilibidi kila mtu aingie chumbani Kwake!

Kitendo Cha Rich kukoswa Kofi na kakake kilimuuma Sana! Aliamua kuchukua nguo zake akapaki kwenye begi dogo la mgongoni Kisha alilala.

Asubuhi kulipokucha alienda kumgongea mamake chumbani Kisha alimuaga, huku akiaga kuwa anaenda kwa rafiki yake anae birthday! Mama alimruhusu.

Huku Chumbani kwa Jolvin alikuwa akichungulia dirishani! Kwa mbali alimuona Gorii” akiruka kamba ilibidi acheke kwanza.

“” Zoezi la kuruka kamba ndio uuzuie mkono wangu kweli! Ayaa… Ngoja tuone Hadi mwisho, Nani mshindi?”

“” Ooyo Jolvin..!!”

Esau alibisha hodi.

“” Wewe ingia bhana!



“” Tunaogopa kuingia kiholela humu chumbani, make hupendagi mtu aingie.. !”



“” Wewe sema wataka Nini!?”

“” Sabuni.. naona nimeishiwa kwangu!”

“” Huwa si shei..!”. Au Ngoja kwanza kumbe Kuna hii mpya sijaitumia! Usinirudishie.”

Esau aliondoka, lakini Jolvin aliendelea kukumbuka siku ya Jana kidogo amshushie Kofi mdogo wake! Asingekuwa Gorii” lingemfika.

Alitoka ndani huku akiwa amevaa pensi na singled akielekea chumbani kwa Rich! Alifika akagonga mlango lakini kimya aliamua kuingia huku akikagua chumba chote kilikuwa kimya! Mwisho kabisa aliingia bafuni kumuangalia hakukuwa na mtu pia.

Huku kwa Gorii” baada ya kumaliza kazi aliamua kuja chumbani kwa Rich! Make kwenye mazoezi hakumuona! Alijua itakuwa kaumizwa na hasira za kakake, akaona budi amjulie khari yake.

Alifika Mlangoni akaita kimya mwisho kabisa aliingia ili ajidhihilishie Kama hamnae mtu ndani! Muda huo Jolvin anatoka bafuni huku kaweka singled yake nyeupe begani, nahii ni baada yakugusa uchafu toka bafuni akaamua kuivua kabisa make alihisi Kama inazidi kumchafua.

Ile anafungua anamuona Gorii” yupo busy na kioo akijitizama huku akibana nywele yake, Jolvin ilibidi amsogelee Hadi Karibu na mgongoni Kisha alishika mkono mmoja ukutani.

“” Hivi ndivyo ulivyosifiwa kuwa Gorii” ana nidhamu, ana akili, ana heshima! “” Sijui hii kuingia kwenye chumba Cha wanaume bila ridhaa yao hii tuiweke upande ganii!?”

Gorii” ndio anageuka vizuri amtizame huenda alihisi, kile kioo ukijitizama Sana kinakuvua nguo ilibidi ahakikishe kwanza make Kuna taswira ya mtu, na mtu kamili!

Ile anageuka ndio wanakutana uso kwa uso na Jolvin! Alichofanya ni kufunga macho yake na mikono huku akimwambia avae ndio afungue.

Jolvin alimwangalia Kisha alicheka Sana, akaona ili kumkomesha nikumchezesha akili yake ili awaogope wanaume hasa upande wake! Make kamzoe kweli hata hamuogopi!

“” Nipe Dakika tano nivae! Ndio ufungue macho yako!!”



Alirudi Hadi kunako mlango Kisha aliurudishia ndio akarudi Hadi kwa Gorii”

“” Fanya ukae kwanza! Make ukifunga macho muda mrefu utaanza ona kizunguzungu! Ukaanguka!

Alimshika mkono Kisha alimkalisha kwenye sofa!

“” Kaka White! Bado tu..! Mama ananitafuta niende jikoni sahiii!”

Muda huo alisikia sauti ikimuita kweli alikuwa ni Dada wa kazi akimuita! Gorii” alitaka kuitika lakini Jolvin alimuonya Kisha yeye alijibu.

“” Mbona kelele! Asubuhi asubuhi watu wamepumzika kamtizame garden!”

Dada ilibidi aondoke japo aliona Kama Gorii” kaelekea kwenye hiko chumba, akahisi ni wenge lake tu.

Gorii” baada ya kushiba tu, alianza maneno yake.

“” Hivi Rich wewe ndie umesema nisiende kusema kuwa ulikuwa out na mwanamke! Vipi lakini anaitwa Nani? Na unae mpango wa kumuoa!? Isiwe unamchezea tu.

“” Ushaanza maneno yako ee! Anaitwa Sophia! tuna malengo ya kuoana!”

Gorii” ilibidi acheke kwanza Kisha alimsogelea kwa ukaribu.

“” Hapo ulipo upo mnadanganya Dada wa watu unamuoa! Hivi inakuja kweli hiyoo! Bado hujaenda chuo, huna kazi na pesa hujapata bado! Hivi itawezekanaje kwanza!!?”

“” Wee! Kama anakupenda kweli lazima akusubili! Siku zote kwenye upendo wa kweli, kusikilizana, kuaminiana, kuvumiliana hiki ndio kiunganishi!”

“” Sawa’ mwalimu wa Mahusiano japo bado mdogo Sana!”

“” Hivi Gorii” wewe huwa unanichukuliaje Mimi! Mimi sahii naweza kuwa na familia! Hata Wewe naweza kukuoa na kukuzalisha pia!”””

“” Basi… Basi… Make unaleta maada za kijinga hapa!



Wakati wakiwa wamekaa Kuna vijana watatu walifika pale! Ile Gorii” anatizama vizuri alimuona Hammad ilibidi ashituke kwanza.

“” Hammad! Wewe tenaa!!?”

“” Yaah! Mimi Ndio! Umenikimbia kule kijijini! Nilikuulizia kwao Muddy, na ndie kanambia upo mjini! Kuna siku nilikuona ukiwa na familia ya Mishoki nikajua kabisa waishi pale! Ila umepiga hatua kuondokana na umaskini.”

Gorii” alishusha pumzi kwanza hakuna kitu kinamuuma kusikia kakaa kwa mtu ili aepuke umaskini na hiki ndio kitu kinampatia ujasiri wa kupambana zaidi.

“” Kipi wakitaka kwangu!!?”

“” Mamako anadeni kwetu, alikuwa akikopa pesaa kwaaajili ya mtaji! Hapa katoweka kijijini akiwa na deni! Kama tumekupata wewe Basi utalilipa, na ukishidwa kulilipa kubali nikufanye mke wangu Ili tuishane.”

“” Mama alikopa lini tenaa!? Wakati hakuwa na Deni au alirudi tena kijijini kukopa!?”

“” Mamako alirudi Kijijini Kama wiki moja baada ya kuondoka, alichukua laki mbili akidai ni pesa ya matibabu! Baba akamuonea huruma kutokana na khari yake aliokuja nayo! Na Mimi nilimpigia debe apewe kwasababu yako tu, Nakupenda”

Neno Nakupenda likamfanya Rich acheke kwanza, kumbe Gorii” huwa anavunga kumbe anae bwana.

“” Nawewe unacheka Nini!!? Wazani huyu ni Bwanangu’ make akili yako na yeye ni kitu kimoja!”

“” Ushaanza kunilinganisha na hii level ya poli Mimi! Ila nimeamini Mungu humpa wakufanana nae! Ila kwasasa haufanani nae make wewe kwasasa ni familia ya Mishoki! Ndio maana upo na Mimi!”

Rich alimtetea mpaka Gorii” alifurahia na kujipa kiburi,

“atafanya Nini huyo Hammad?”



Alimsogelea Karibu Kisha alimnong’oneza sikioni.

“” Ukinigusa Mimi ndio umegusa familia nzima ya Mishoki! Kwahiyo kuwa makini!”

Hammad alisogea nyuma kidogo Kisha aliwapatia Ishara wenzake kilichofuata hapo ni kelele tupu huku wakipeana vipigo vya kufa mtu, baadae Hammad aliwanong’oneza wenzake wakatoka haraka haraka .
 
SEHEMU YA NANE



Huku barabarani Jolvin alikuwa na Anelisa wakiendelea kula bata, siku hiyo walizungukia mitaa mingi, Kama bahati nzuri walifika sehemu Kunae kelele ilibidi wachungulie kwa pembeni alimuona Kama Rich amelala ilibidi ashuke, pembeni kidogo alimuona Gorii” katapakaa tope mwili mzima huku akizidi kumlalamikia Hammad ambae nae alikuwa hoi, alikuwa amelala chali huku akimtizama Gorii” kwa pembeni akiongea nae.

“” Kwanini nisikuoe tu Gorii” tukaachana na mambo haya ya kuaibishana mtaani!?”

“” Kwanza hufai kuwa mme! Mara hii tu nimenusurika kumwaga ubongo! Hio nguvu ya kuitwa mke wa Hammad itatoka wapi!?”

Huku kwa Rich ndio alizidi kulalamika, ukiangalia mwili wake laini laini alipigwa rungu moja tu hoi akiugumia maumivu. Alimtizama Gorii” ambae nae yupo hoi.

“” Sasa Gorii” hapa tunaondoka vipi!? Mimi mwenyewe hata nguvu Sina za kusimama! Ee Mungu saidia Kaka White asituone tulivyofanana na ardhi make atatuongezea fimbo tenaa!”

Gorii” ilibidi ajikaze alisogea Hadi kwa Rich Kisha alifanya kumuinua, akimkalisha.

“” Yaani leo tumekuwa Kama watu wa mazingaombwe si sura zetu , nguo zetu! Hivi na Mimi nipo Kama Wewe usoni!?”

“” Wewe ndo kabisa!! Yaani hiyo nywele kung’aa labda ukadumbukie ziwani!”



Walicheka kwa pamoja, Hammad nae aliamka ilibidi avute Simu huku akiwapigia rafiki zake, kumbe muda ule aliwarusu wakaandae mazingira Nyumbani! Alijua lazima Gorii” akubali kuongozana nae, make ile pesa hawezi kuilipa.



Muda huo Jolvin alikuwa akiwatizama vizuri! Hakuelewa kipi kilikuwa kinaendelea pale! Muda huo kumbe alikuwa amewapigia Simu kina Esau na Joely wakawa wamefika pale!

Walishuka kwenye gari haraka, hutaamini wote walikimbilia kumuona Rich, halafu Gorii yeye walimtenga. Gorii” hakujali walaa!” alibaki akijitengeneza vizuri ili ainuke lakini mguu wake ulikuwa umeteguka ilibidi akae chini huku akijaribu kuunyosha!

Muda huo Jolvin alikuwa akimtizama, Kisha alitingisha kichwa huku akiongea mwenyewe.

“” Sijui lini ataipata familia yake akaepukana na kudhalilisha familia ya Mishoki! “

Huku kwa Hammad baada ya kuiona ile familia imetia timu pale ilibidi akimbie, lakini Jolvin alikuwa amekalili prate namba ya gari iliyomchukua, swala la kuanza kupigishana kelele na mtu mchafu haina maana Kwake!”

Rich aliinuliwa na ndugu zake wawili huku kwa Gorii” alijua leo ndio siku ya kuwa mbali na familia ya Mishoki, alibidi aanze kuandaa mazingira ya kuwa mwenyewe.

Alishangaa Kuna mtu kamnyoshea mkono anataka kumsaidia, alimtizama kwanza asiamini Jolvin ndie yupo pole, alitazama kwanza mikono yake ilivyochafuka na tope! Ikabidi atikise kichwa kukataa, lakini Jolvin aliendelea kumnyoshea mkono.

Ilibidi atoe mkono wake huku akiangalia jinsi Jolvin anavyomshika mkono, japo alimshika kwa kinyaa Sana ila ndio ulikuwa msaada Kwake.

Alimkokota taratibu kuelekea kwenye gari ya Kina Esau make yeye alikuwa na usafiri wake na Anelisa, alimkabizisha kisha alirudi kwenye gari yake! Ile anafika tu Anelisa alikuwa ameandaa maji ya chupa aliamua kumnawisha kwanza huku akimuuliza.

“” Huyo binti ni Nani katika familia ya Mishoki!? Imekuwaje ukubali uchafuke kwaaajili yake!?”

“” Achana nae kwanza! Hakili yake haipo sawa’ ndio maana nimemsaidia! “” Muda nao umeenda kweli Ngoja nikupitishe Nyumbani kwanza.”



“” Hutaki kuwasalimia wazazi!!?”

“” Ni usiku sahiii! Nitakuja mchana, Ngoja nikawawahi kwanza hawa wapuuzi!”

Huku Njiani Esau ndio alikuwa akiendesha gari! Joely yeye alikuwa Hana mbavu! Muda wote alikuwa akiwapiga picha Kama kumbukumbu.

“” Hapana Kaka! Usiipost… Nitaabika ujue!”

“” Hivi bado unae Sophia! Nataka picha hizi nimuoneshe!”

Gorii” muda huo yeye alikuwa katulia huku akimfikilia Hammad anavyozidi kumfatilia, zaidi alimuwazia mamake alichukua pesa nyingi kwa matibabu gani? Alijikuta akianza kulia mpka wenzake wakashituka..

“” Gorii” Nini tenaa!? Mmepigana kule, ulikuwa hulii sahii ndio walia, au umeumizwa Sana!?”

“” Mamangu kachukua pesa ya matibabu! Ile ni pesa ndefu nawaza atakuwa kazidiwa Sana! Sijui hata anatibiwa wapi!? Kesho itabidi nirudi kumtafuta Hammad huenda anajua wapi mama alipo!”

Wote walibaki kumtizama kwa makini.

“” Lakini Gorii” usiwaze mama atakuwa salama tu! Nimeona machapisho yako mengi yamejaa mtaani! Lazima yatamfikia tu!

Walifika Hadi Nyumbani kilichofuata, Gorii” na Rich walishuka wakawa wamekaa nje kwanza.

“” Vipi mbona hutoki Mimi nataka kuoga kwanza!”

Rich aliongea Huku akitaka kuingia kwenye maji, Gorii” ilibidi akakae getini kwa walinzi akingoja Rich aoge kwanza!.

Muda huo huo Jolvin ndio anaingia, alifika getini kwanza Kisha alishusha kioo kumtizama Gorii”. Aliamua kupaki gari pembeni Kisha aliingia ndani kubadilisha nguo baadae alirudi akiwa na Bibi.

“” Umemuona Mjukuu wako wa kufikia alivyofananania na ardhi!?”



Gorii” alipomuona Bibi yake alikimbia kwenye swimming pool! Alijitupia ili kuepuka aibu! Ile Bibi anakuja kutizama aliona maji ndio yanaruka ilibidi wote wabaki wakishangaa.

Huku kwa Rich baada ya kumuona Gorii kaingia ilibidi apige kelele make alikuwa na nguo ya ndani tu!

“” Wewe hebu tulia bhana! Mi hata sikuchungulii!? Si ukae pembeni na Mimi nikae hii pembe!”

Bibi Alibaki kucheka aliamua kurudi ndani.

Jolvin yeye aliamua kusogea Karibu Ili azidi kuwakagua Kama wanatakata kweli.

“” Ayaa! Wewe binti mwenye nywele ndefu inuka tukuone!!”

Gorii” aliinua kichwa.

“” Bado kabisa hujatakata! Sogea hapa uchukue sabuni!

“” Sasa nasogea vipi wakati Rich yupo sehemu hiyo!?”

“” Rich zama chini mwenzako asogee!!”

“” Hapo sawa’ umeanza kutakata!”

Baada ya kumaliza kuoga, kazi ikabaki kwa Gorii” atatoka vipi wakati tayari nguo zimeloweka.

“” Kaka White!! Zima Basi taa mi nikimbie ndani kubadilisha mavazi!”

“” Sahii unaogopa! Wakati mpaka Sasa upo na mwanaume kwenye maji Kama ni kuchunguliwa tu! Ushaonwa!?”

“” Kaka White! Niitie Basi Dada” aende chumbani kuniangalizia nguo!” Nahisi baridi et..!”

Jolvin alipiga Simu, nguo zikaletwa ilibidi waondoke wamuache mwenyewe!

Gorii” ndio akapata muda wa kwenda chumbani kubadilisha hata hivo ni usiku Tayari.

Baada ya kumaliza Bibi alimuita chumbani Kwake! Alimsaidia kumnyoosha nywele huku akimuulizia kipi kiliwakuta ilibidi amwelezee, hata hivyo huwa hamfichi.

“” Kwahiyo ni laki mbili tu ndio inatakiwa!?”

“” Ni hiyo tu! Halafu Bibi naomba umuombe mama aniruhusu nifanye kazi ili niweze kumlipa Hammad pesa yake!”

“” Hio ni pesa ndogo Sana! Nitakulipia mjukuu wangu!”

“” Bibi unazo hizo pesaa!!?”

Bibi alicheka Kisha alimuaga akalale kwanza, kesho ataongea nae. Ile ametoka tu! Bibi alimpigia Simu Jolvin alipofika akaanza kumuelezea kuhusu Gorii”.

“” Usijali Bibi! Mimi nitaenda kuilipa hiyo pesa! Kuhusu Hammad nitaongea nae! Na hatomgusa tena Gorii”.

Siku iliyofuata! Majira ya mchana Gorii” alikuwa kajipumnzisha chumbani Kwake huku akimfikilia Mamake atakuwa wapi!

Jolvin Aligonga mlango kwa Gorii” akawa amefungua. Ilibidi kwanza akusanye zile karatasi akaziweka vizuri.

“” Sa mbona unakubali kuchafuka tope! Wakati chumbani kwako unapangilia vizuri!”

“” Kaka White!! Leo umeingia chumbani kwangu! Itakuwa Kuna shida ee!”

Jolvin alisogea karibu mezani Kisha alichukua picha ya Mamake Gorii” akaitizama, huku akichukua karatasi alizokuwa kachapisha.

Gorii” alibaki amesimama Karibu na mlango, Jolvin alimuuliza.

“” Kwanini hukai! Au waniogopa!?”

“” Ni Juzi tu umenifungia chumbani! Leo tena tupo wote chumbani Mimi sikuamini!”

Jolvin alifanya kupotezea, aliinyanyua Simu yake akawa amempigia Hammad Kisha alimpatia Simu Gorii” aongee nae!



“” Gorii” naomba unisamehe kwa kile kitu kilichotokea Jana! Pia kuhusu Hilo Deni la mamako tayari Bibi yako kalipia! Kwasasa upo huru!”

Jolvin aliidaka ile Simu Kisha alimalizia kuongea.

“” Usajili wa Prate namba yako tayari upo kituoni! Kama unafanya tukio baya kumbuka maovu yako yametangulia kituoni.”

Kisha alikata Simu.

“” Kaka White! Thank you!”

Jolvin alimwangalia Kwanza Kisha alicheka make anapenda kingeleza huyu.

“” Sorry lakini, elimu yako umesoma Hadi ngazi ipi!?”

“” Ngazi tenaa? Au Unamaanisha Darasa la ngapi? Mi nimeishia Darasa la Saba! Nikawa nimefaulu kujiunga kidato Cha kwanza, sema shule ilikuwa mbali ilikuwa inanilazimu nikakae huko! Na Mimi kumuacha mama pekee siwezi, ilibidi nisiendelee na masomo! Japo niliahidi kuwa Karibu na mama muda wote nimlinde lakini sinae tenaa!”

Gorii” aliongea maneno mazito, kweli alimpenda Mamake hata kupambana kote ilikuwa ni kwaajili ya Mamake.

“” Pole Sana! Mama atarudi tu! Hata Mimi nitakusaidia kumtafuta! Vipi lakini mbona Kama unashinika uso unae maumivu kwenye bega!?”

Gorii” ilibidi akatae japo alikuwa ameumia kwa kupigana na Hammad.

“” Najua unanificha Basi niruhusu nijilizishe Kama kweli hujaumia!?”

Jolvin alimsogelea Karibu Kisha alishusha shifoni alokuwa kavaa, aliona ni kidonda kibichi bado kinatoa damu kutokana na ile nguo alokuwa kavaa ilikuwa imeshika kwenye kidonda.

“” Naomba utoe hio nguo ya juu Kisha jifunge kanga! Nakuja mara moja na dawa!”

Alienda Hadi chumbani Kwake akarudi na boksi la huduma ya kwanza! Joely akawa amemuona ilibidi amfuate mpaka anafika!



“” Upo tayari niingie?”

Gorii” alimruhusu muda huo alikuwa kajifunga kanga kifuani.

“” Najua itauma ila jikaze ili upone haraka!”

Joely nae aliingia, akifatia na Rich.

“” Gorii” kumbe wewe uliumia hivo Jana! Mbona ulijikaza tu! Uwe unasema kwanza! Utakuja kuoza eti..!!”

Jolvin, Esuu walibaki kumtizama Rich, mpaka walicheka.

Jolvin alimwangalia Joely Huku akimpatia ishara ampake dawa make yeye ashaanza kumuonea huruma kwa ile dawa ni Kali sana, ilikuwa ni ” iodine solution”

Joely alichukua pamba akainoweka kidogo kwenye dawa Kisha alifanya Kama anamfuta, Kelele ya maumivu ya dawa ilisika nyumba nzima!
 
Back
Top Bottom