MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Hapa duniani nimeshawahi kuwa na ndoto nyingi. Kuna ambazo zimeshatimia, zilizofeli na zingine michakato inaendelea. Sasa jana ndoto yangu ya hivi karibuni imefikia mwisho bila mafanikio. Ni kuhusu kumpenda na kutaka kumuoa Mfalme Zumaridi.
Kiukweli kwa miaka kadhaa nimekuwa nikiteketea ndani kwa ndani kila nilipokuwa nikiona video za Mfalme Zumaridi na kujikuta nikilihitaji penzi lake tamu. Nikawa nimeweka nia kwamba ipo siku hili suala litatimia kwa kudhani kwamba huyu Baby Zuma atakuwa yuko single kwa jinsi anavyoishi.
Jana baada ya kutoka magereza akiwa anahojiwa ndo akasema yeye ana mume na watoto. Kiufupi ameolewa. Ni mtu pekee anayejiita Mungu huku akiwa kaolewa. Nimesikitika sana ila ndo hali halisi. Lile uno lake ndo ninalilia zaidi. Lakini sijakata tamaa nitapambana kupata mwingine kuliko kujiunga na wanaharakati wa KATAA NDOA.