Ndoto yatimia: Serikali kupitia TPA kuanza ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo kuanzia mwaka huu wa 2023/24

Ndoto yatimia: Serikali kupitia TPA kuanza ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo kuanzia mwaka huu wa 2023/24

The Sunk Cost Fallacy 2

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2022
Posts
9,436
Reaction score
10,944
Habari ndugu Wadau..

Baada ya siasa na saga nyingi ,hatimaye Serikali ya awamu ya 6 imesema itaanza ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo mwaka huu wa Fedha wa 2023/24 ambapo ujenzi wake utasimamiwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA..

Ile ndoto Sasa inaenda kuwa kweli ambapo Tanzania itapata Bandari kubwa kabisa Kwa Ajili ya kukuza Uchumi.

Ushauri wangu napenda,chonde chinde Serikali itafute mbia wa kujenga nae sio kama pale awali kwamba Kila kitu kifanywe na pesa za ndani, ni hatari Kwa Uchumi Wetu tusije kurudi kule kule Kwa Jiwenomics.

Hongera sana SSH na Serikali Kwa Ujumla.
===
Serikali imeamua mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo unaotarajiwa kuanza katika Mwaka wa Fedha wa 2023/24 utekelezwe na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Juma Kijavara amesema katika mahojiano ya kipindi cha Bandari Zetu kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

Alisema matayarisho ya mradi huo yameanza, lakini ujenzi unatarajiwa kuanza katika mwaka wa fedha unaoanza Julai. “Huu ni moja ya miradi mikubwa utakaobadilisha na kukuza kabisa uchumi wa nchi yetu kwa sababu sisi kama mamlaka tutaweka miundombinu ya kibandari na wapo pia watu wengine walio tayari kuwekeza vitu vingine vya kiuchumi.

Kwa mfano viwanda, hospitali na majengo mengine,” alisema Kijavara. Alisema TPA inataka mradi huo uwe mfano na ubadili mwenendo wa bandari Afrika Mashariki nzima.

“Kwa mfano sisi tukisema ile mizigo tunayoihudumia kwa uchache kutokana na miundombinu yetu ukilinganisha na nchi nyingine wanazosema zimetuzidi kihuduma, lakini ukilinganisha na nchi ambazo kweli zinategemea uchumi wa bandari, mizigo ya nchi zetu zote za Afrika Mashariki hatufikii zile nchi,” alisema.

Aliongeza: “Nchi ya Malaysia inahudumia tani zaidi ya milioni 20 kwa mwaka sisi hata kontena milioni moja au wenzetu kontena milioni tano bado ni chache sana.” Alisema kupitia mradi huo, TPA inalenga kuhakikisha Bandari ya Bagamoyo inahudumia kontena zaidi ya milioni 10 kwa mwaka.

Alisema TPA inapokwenda kuijenga bandari hiyo ya Bagamoyo maana yake inataka kwenda kuhudumia kontena zaidi ya milioni 10 kwa mwaka.
 
Tuombe waarabu wawekeze hiyo bandari nikiangalia naona kuna mambo tutafeli tukitumia fedha za ndani our revenue collections barely suffices our Recurrent expenditure
Kabisa,hii tabia ya Kila kitu kutumia pesa za ndani ni mbaya sana Kwa uchumi..

Ndio inasababisha financial inclusion iwe ngumu na kuleta umaskini
 
Wachina out, hatutaki uwizi ni bora tujenge sisi na mradi uwe wetu 100%

JPM aliona mbali sana

Kwa hiyo amekosekana wa kuusaini ule mkataba wa kijinga?

Tehe. Tehe. Tehe JPM bhana!

Umenifunza mengi na kunifanya niwe jasiri zaidi hata kwa yale makubwa zaidi

Shule ni nzuri tusiidharau
 
Tuombe waarabu wawekeze hiyo bandari nikiangalia naona kuna mambo tutafeli tukitumia fedha za ndani our revenue collections barely suffices our Recurrent expenditure
Kwann tuferi
Tukiamua tunaweza
Mm nataka serikali ionyeshe inaweza
Na itawezekana
Kama alovyoonyesha magufuri anaweza
Leo hii reli ya standard gauge tunaenda kuimaliza
Bwawa tunaenda kulimaliza

Usione lile bwawa mabeberu kulipigia kelele sijui tutaharibu mazingira maneno kobao
7bu mojawapo na kuu hasa hawakufaidika
Ingekuwa tumeingia UBIA na kampuni la kimarekani au ulaya wakatengeneza kisha waliendeshe bwawa miaka 50 kurudisha pesa ndio watuachie likiwa na cracks kibao
Usingeona KELELE zozote
Beberu/mchina akupi msaada bure msaada akikupa leo utaanza kuulipia wewe na atakuja kuulipia mpk MJUKUU wako

MAGUFURI alivyowakataa WACHINA kwa mashart yao ya KIWAKI usidhani alikuwa mjinga aliona mbali
 
Habari ndugu Wadau..

Baada ya siasa na saga nyingi ,hatimaye Serikali ya awamu ya 6 imesema itaanza ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo mwaka huu wa Fedha wa 2023/24 ambapo ujenzi wake utasimamiwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA..

Ile ndoto Sasa inaenda kuwa kweli ambapo Tanzania itapata Bandari kubwa kabisa Kwa Ajili ya kukuza Uchumi.

Ushauri wangu napenda,chonde chinde Serikali itafute mbia wa kujenga nae sio kama pale awali kwamba Kila kitu kifanywe na pesa za ndani, ni hatari Kwa Uchumi Wetu tusije kurudi kule kule Kwa Jiwenomics.

Hongera sana SSH na Serikali Kwa Ujumla.

hivi hiyo bandari inajengwa bagamoyo sehemu gani
 
Back
Top Bottom