Ndoto yatimia: Serikali kupitia TPA kuanza ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo kuanzia mwaka huu wa 2023/24

Ndoto yatimia: Serikali kupitia TPA kuanza ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo kuanzia mwaka huu wa 2023/24

Pesa za kuajiri hata walimu tu ni mtihani hadi elimu ya watoto imebaki kituko, kazi kutafuta miradi ya kuwapa ten percent utafikiri nchi ina tatizo critical la bandari.
Bandari ni muhimu, kama una mtoto jiongeze
 
.
JamiiForums1490063517.jpg
 
Habari ndugu Wadau..

Baada ya siasa na saga nyingi ,hatimaye Serikali ya awamu ya 6 imesema itaanza ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo mwaka huu wa Fedha wa 2023/24 ambapo ujenzi wake utasimamiwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA..

Ile ndoto Sasa inaenda kuwa kweli ambapo Tanzania itapata Bandari kubwa kabisa Kwa Ajili ya kukuza Uchumi.

Ushauri wangu napenda,chonde chinde Serikali itafute mbia wa kujenga nae sio kama pale awali kwamba Kila kitu kifanywe na pesa za ndani, ni hatari Kwa Uchumi Wetu tusije kurudi kule kule Kwa Jiwenomics.

Hongera sana SSH na Serikali Kwa Ujumla.

Basi, wenye akili tumeelewa. Baadae TPA itaingia makubaliano na wachina ambao nao wata subcontract waOmani. Yaleyale
 
Watu wengi wanaamini Magufuli alikuwa mkali, binafsi nilikuwa namuona bado soft yaani ukali wake aufikii hata nchi za ulaya zinazo hubiri democracy kwenye kunyooshana huo ndio ukweli wenyewe.

Huko kwa mabeberu kama uelewi kwa maelezo na sheria basi utaelewa siku ukiingia kwenye 18 zao na utatia akili, ndio maana kila mtu yupo kwenye mstari mwenyewe.

Sasa watanzania (and this is unique to us only in the world), yaani watu wengi wana akili zao au mtazamo wao juu ya jambo fulani ata waeleweshwe vipi awataki kuelewa wakishajijengea premise ya ukweli wao wanao utaka ni ivyo tu.

Ndio kama hili sakata la bandari yaani Kakoko kalielezea kweli walipokwama na wachina. Kaelezea bandari ya Bagamoyo aina mjadala with or without wachina lazima ijengwe Dar ishafikia saturation point aiwezi kuwa expanded zaidi na mizigo ya nchi inayoitumia inazidi kuongezeka na itazidi kuongezeka.

Sasa unashangaa anaingia raisi mwingine anaanza na kuropoka majukwaani as if wenzake walizuia kwa makusudi wakati wametumia nguvu nyingi kwenye kuelimisha umma walipokwama na kusubiri hatma ya majadiliano kama vipi wajenge wenyewe huo ndio ulikuwa mkakati wa TPA.

Kwenye LNG ivyo ivyo kama ulisoma ile MoU iliyowahi kuwekwa hapa unaona kwanini J.K akutaka lawama za baadae ziwe zake ilikuwa mbovu mno.

Magufuli nae akutaka kuugusa kwa sababu wawekezaji awakuwa tayari kuubadilisha terms za kwenye MoU na ulikuwa na ‘stabilisation clause’ kumbuka hawa tayari wana exclusive right ya ku-exploit vitalu walivyofanyia exploration kukabaki na stalement kwenye majadiliano.

Kaingia Samia anaanza kupayuka nataka majadiliano yaishe soon, niliposikia tu nikajua hana facts, walisema December majadiliano yatakuwa yameisha kiko wapi.

Uzuri wa haya mambo Binafsi sasa hivi naanza kupata imani kuna watu wapo well trained kwenye maswala ya mikataba siku wakikutana na ‘bi Tozo’ wakimuelezea wanachogawa kama namuona akistuka “mtume ebu subirini kwanza, kabla amjasaini”.

Msingi wa upotoshaji ni mijitu ya ovyo kama Zitto na waropokaji au niite wadandiaji wa mambo wenye upeo mdogo kama waziri wa nishati yaani akianza kuongelea maswala ya mikataba his ignorance halafu mwenyewe anajiona wa maana kweli kweli kumbe bogus full of ujinga.

Ndio maana mimi siku nikiwa ata mwenyekiti wa mtaa nikikuta mtu katupa taka kiholela mtaani ntamuamsha ata usiku wa manane akaziokote yaani tuna tabia fulani za ujinga unique to us only bila ya kunyooshana kwa adhabu atuendi.
 
Ndoto yako au ya mwenye ndoto yake? Usijishaue !! Wenye ndoto za hilo wanajulukana !!!
 
Habari ndugu Wadau..

Baada ya siasa na saga nyingi ,hatimaye Serikali ya awamu ya 6 imesema itaanza ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo mwaka huu wa Fedha wa 2023/24 ambapo ujenzi wake utasimamiwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA..

Ile ndoto Sasa inaenda kuwa kweli ambapo Tanzania itapata Bandari kubwa kabisa Kwa Ajili ya kukuza Uchumi.

Ushauri wangu napenda,chonde chinde Serikali itafute mbia wa kujenga nae sio kama pale awali kwamba Kila kitu kifanywe na pesa za ndani, ni hatari Kwa Uchumi Wetu tusije kurudi kule kule Kwa Jiwenomics.

Hongera sana SSH na Serikali Kwa Ujumla.

Na wewe kwa akili yako ulikua unaamini kweli ni fedha za ndani zinatumika?
 
Lile la mwekezaji ambaye angehodhi ardhi yetu kwa masharti ya kiwendawazimu ndio tulilikataa chini ya jpm. Kama tunajenga wenyewe itakua ndio mradi mkubwa wa mama wa kwanza bila shaka. Tutatumia hela za ndani na nje za kukopa bila shaka. Kuna wale wanajidai wachumi eti miradi mikubwa ya jpm ni white elepants. Sasa waseme tena ujenzi wa bagamoyo kutumia TPA itakua white elephant.
Kwenye miradi mikubwa mama awe makini kwani gharama inaweza kuwekwa kubwa kwa ufisadi watu wakiweka cha juu
Watu wa ccm hawachelewi kuweka 100 % chap,wezi kabisa
 
Habari ndugu Wadau..

Baada ya siasa na saga nyingi ,hatimaye Serikali ya awamu ya 6 imesema itaanza ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo mwaka huu wa Fedha wa 2023/24 ambapo ujenzi wake utasimamiwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA..

Ile ndoto Sasa inaenda kuwa kweli ambapo Tanzania itapata Bandari kubwa kabisa Kwa Ajili ya kukuza Uchumi.

Ushauri wangu napenda,chonde chinde Serikali itafute mbia wa kujenga nae sio kama pale awali kwamba Kila kitu kifanywe na pesa za ndani, ni hatari Kwa Uchumi Wetu tusije kurudi kule kule Kwa Jiwenomics.

Hongera sana SSH na Serikali Kwa Ujumla.

'Irony' ni kwamba unajiamini sana kama 'economist' katika uwezo wa kupanga mipango ya maendeleo ya nchi hii, lakini inapokuja kwenye maswala ya kujijengea uwezo katika nyanja mbalimbali, ili tuweze kupunguza utegemezi wa nje, hapo kila kitu kinakutoka kabisa akilini!

Hili ni jambo la kushangaza sana, na sielewi linatoka wapi.

Nchi hii inashindwa kupata dola 200 kwa mwaka au chini ya hapo kuendesha ujenzi wa bandari? Pesa zinazovurugwa tu na kodi zisolipwa ni sawa tu, mradi tutembeze bakuli tusaidiwe kila jambo?
Hii ndiyo elimu ya uchumi inavyotuelekeza?
 
Si wakati ule ulikuwa unashangilia huo upuuzi?ghafla umegeuka,chawa kazini
Nashangalia nini? Wachina walikua na masharti ya hovyo ni mwendawazimu tu ndio angekubali. Magufuli hakukataa bandari bali alikataa masharti ya mwekezaji huyo mchina.
Mama Samia alipoingia madarakani Kuna watu wakamshika masikio afufue majadiliano na mchina, mama akafufua Ila mwisho wa siku kajionea na imeshindikana. Ndio hapo TPA wakaamua wajenge wenyewe
 
Why bagamoyo?
Pazuri kuwa Bandari:
1. Pana kina kirefu kwa meli kubwa.
2. Pana eneo kubwa la ardhi kwa kupakua na kupakia mizigo.
3. Ni rahisi kupaunga kwa reli ili kukutana na reli zilizopo (tazara, reli ya kati na SGR)
4. Ni jirani na EPZ ya viwanda Bagamoyo
 
Tuwakatae Wachina
Unapeleka tatizo kusikokuwa na tatizo.

Tatizo lipo hapa hapa kwenye viongozi wetu, lakini hatuamini, inakuwa rahisi zaidi kuhamishia lawama kwingine.

Mchina atakutandika, kwa sababu mmatumbi mwenzio ndiye anayemsaidia akutandike.

Mkataba mbovu ulitengenezwa wachina wakijua watakaoukubali hawana wajualo; au wanaruhusu iwe hivyo kwa maksudi mazima.

Wahenga walisema ukila na kipofu usimguse mkono tu basi. Wachina wanatumia upofu wetu kwa faida yao.
 
Habari ndugu Wadau..

Baada ya siasa na saga nyingi ,hatimaye Serikali ya awamu ya 6 imesema itaanza ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo mwaka huu wa Fedha wa 2023/24 ambapo ujenzi wake utasimamiwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA..

Ile ndoto Sasa inaenda kuwa kweli ambapo Tanzania itapata Bandari kubwa kabisa Kwa Ajili ya kukuza Uchumi.

Ushauri wangu napenda,chonde chinde Serikali itafute mbia wa kujenga nae sio kama pale awali kwamba Kila kitu kifanywe na pesa za ndani, ni hatari Kwa Uchumi Wetu tusije kurudi kule kule Kwa Jiwenomics.

Hongera sana SSH na Serikali Kwa Ujumla.

Mchina kavalishwa koti la Tanzania ili asionekane kwa uchina wake, daah salale ....
 
Back
Top Bottom