Ndoto zangu za kujiunga JF zimetia

Mkuu princemikazo karibu jukwaani.

Bila shaka ukiwa kama mgeni unaweza kujua ama kusikia maneno hayo uliotaja kama avatar,Pm, mods na kadharika pia waweza ukawajua members kama uliowataja kwa kuwa ni wazoefu na wanamuda mrefu humu.

Swali langu wewe mgeni, umejuaje jinsi ya ku quote thread au comment ya mtu humu ndani? Au nayo umejifunza ukiwa mgeni
Huko nje?

Nijibu tu hili.

Pili, Wanaume Tumezoea Lawama - JamiiForums tangu rais wako anaapishwa ulikuwa unasoma!!! dalasa la ngapi embu nikumbushe tena lakin mkuu sasa yapata miaka mitatu umeshapata mke na beki tatu juu? . Kweli una speed ya supersonic. Eehh KA'BINTI KA BABA MWENYE NYUMBA - JamiiForums na huyu mtoto wa mwenye nyumba bila shaka ume mdowload humu jf.


Bajaji mpya injini ya fekoni. Karibu mdogo wake @beiraboy

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swali zuri sana mkuu,,Kuanzisha thread pamoja na ku-quote nimefundishwa na member wa humu,,Hiyo thread ya Mke sijui house girl pamoja na binti wa Mwenye nyumba angalia hiyo thread iko jukwaa gan mkuu??Iko jukwaa la Utani/jokes+Udaku,Unataka kusema Red scorpion anachokipost kwenye ilo jukwaa au Numbisa ni maisha yake kweli??Kuhusu shule 2015 nilikua Form4 saiv niko chuo,,Sijui nitakua nimekujibu vizuri mkuu?
 
Lakini pia Suala la Ku-quote mbona kwenye coment ya mtu kuna option kabisa pale kuna like na Reply..!!
 
Hi inawahusu malegendary wacha wengine tupite hivi👣👣👣👣👣
 
Mkuu princemikazo umejitahidi lakini maelezo yako bado siyo concrete naona bado una tu- blindfold kuhusu ugeni wako.

Sasa mkuu mbona unatufumbua macho kwa maelezo yako maana mtu ukipost kuna mda mwingne unaweza hata usijue umepost jukwaa lipi Lakini wewe umejua hadi post ilipowekwa na jukwaa kabisa from general to specific hii haijawahi tokea(in Lisu's voice).

Pili, umefundishwa na memba gani na kwa njia gani maana ku-quote umeanza kwenye thread yako ya kwanza wakati pm hujaijua sasa huyo memba mmekutana wapi hadi akufundishe ku- quote?

Tatu, Umeingia na kujua kabisa unaanzia wapi kutu fake na story zako. Maana mgeni huja.hujitambulisha.hupokewa na mengine hufuata.sasa ghafla bin vuu unakuja na uzi wa mke,house girl,mtoto mwenyenyumba. Kiukweli kutoka moyoni kwa sisi tulio wazoefu humu hatuta kuamini hata kidogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alienifundisha kanielekaza live yaani practically coz nilikutana nae kabisa tukakaa akaingia jf akaanza kunielekeza,Pia kuhusu kuchagua jukwaa kila jukwaa pale juu kuna Title thread na sehem ya kupost,so ukipost pale direct unakua umepost kwenye jukwaa husika mkuu..Ushanifahamu vyedi?(In Mussa Husein's voice)
 
(Costful ,succes, succsesful, mamber) angalia makosa yako--- dogo wewe unajitahidi katika lugha ya kiingereza, lakini bado unatakiwa uongeze bidii zaidi ndipo ulete "posts" zako humu kwa kiingereza. Soma "grammar" zaidi.
Unaweza kuwa na ushauri au maoni mazuri ila ukashindwa namna ya kuwasilisha, unawezaje kuniita dogo kwa mfano? Kwa kigezo kipi?
but all in all your advice is good in case of grammar...
Be blessed.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaweza kuwa na ushauri au maoni mazuri ila ukashindwa namna ya kuwasilisha, unawezaje kuniita dogo kwa mfano? Kwa kigezo kipi?
but all in all your advice is good in case of grammar...
Be blessed.


Sent using Jamii Forums mobile app


Samahani, mimi ninakumbuka nilipokuwa darasa la saba nilikuwa naandika kiingereza kama chako, basi nikikumbuka umri wangu wakati huo kama miaka 16 hivi, nikaona labda na wewe unao umri huo pia, kama nimekosea samahani.

But never give up .
 
Samahani, mimi ninakumbuka nilipokuwa darasa la saba nilikuwa naandika kiingereza kama chako, basi nikikumbuka umri wangu wakati huo kama miaka 16 hivi, nikaona labda na wewe unao umri huo pia, kama nimekosea samahani.

But never give up .
Haina shida mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…