Ndugai Aanze na "Waheshimiwa" Wabunge kabla ya "Wasomi" Mawakili

Ndugai Aanze na "Waheshimiwa" Wabunge kabla ya "Wasomi" Mawakili

Mindi

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2008
Posts
3,523
Reaction score
4,992
Spika wa Bunge, Job Ndugai, ameeleza "kukerwa" kwake na kada nne kwamba wanajiona ni bora kuliko wengine. Kwa mfano Mawakili, ambao wana utaratibu wa kuitwa "Wakili Msomi" kabla ya kutaja jina. Hoja ya Ndugai ni kwamba iweje Mawakili waitane "Msomi" ambapo wasomi wako wengi tu, siyo Mawakili peke yao?

Binafsi sioni shida kama kada fulani wanakuwa na utaratibu fulani wa kuitana, kama ambavyo Watanzania hawana tatizo kimsingi, na kitendo cha Wabunge wa Bunge letu kuamua kuanzia miaka ya 90 kama sikosei, kujiita "Mheshimiwa" kabla ya kutaja jina la Mbunge husika.

Huko nyuma, enzi za Ujamaa na Kujitegemea, Watanzania tuliitana "ndugu". Na kwa hiyo ilikuwa kawaida kabisa kusikia kauli kama "Ndugu Rais", "Ndugu Waziri", "Ndugu Mbunge", "Ndugu Mwenyekiti", "Ndugu Spika", nk.

Lakini kwa hekima zao nyingi, Wabunge wetu waliamua kuachana na neno "Ndugu" na kutumia neno "Mheshimiwa". Hii ni pamoja na kwamba CCM inaamini kwamba "binadamu wote wanastahili Heshima", na kwa hiyo kwa kweli title ya "Mheshimiwa" inastahili kwa kila binadamu.

Sina hakika kama Job Ndugai ameishia kwa kada hizo tu, yaani Mawakili, Mainjinia, Madaktari. Sijui kama hana tatizo na Kardinali kuitwa "Mwadhama", Askofu kuitwa "Mhashamu", nk.

Ninachojua ni mambo mawili. Kwanza kitendo cha Ndugai kuanza kutafakari hayo mambo ya Titles, ni wazi Spika wetu amekosa kazi muhimu ya kufanya. Huenda ni kutokana na Bunge letu kukosa changamoto, hasa ambazo zingeletwa na Bunge kamili, halali, la vyama vingi. Bunge hili la Chama Kimoja linamboa Spika, halimpi changamoto za kumfanya hata akiongea, aongee kwa makini.

Pili, nimshauri Spika, kama kweli anakerwa na Title za Mawakili na hao wengine, basi aoneshe mfano. Ehee, maana Charity begins at home ati! Aje na pendekezo la kuachana na title ya "Mheshimiwa" kwa Wabunge. Baada ya hapo, ndio aanze hizo njozi zake.
 
Usilaumu kila kitu, hizo ni Stimu za Chanjo si unajua nayeye alizamishiwa sindano yote akamwagiwa chanjo?
 
Back
Top Bottom