Wanao mlahumu Spika wanamuonea - JPM alikuwa ni binadamu ambaye hashauriki - sasa ulitegemea Spika angefanya nini au mlitaka yamkute yaliyo mkumba Profesa Asaad?
Kama nakumbuka vizuri, mwaka jana Mh. Ndugai aligusia kuhusu alivyo kwenda Uchina,akabahatika kukutana na lika la Uongozi wa China ambalo lilikuwa karibu na Mao na Nyerere ingawa wengi wao wamekwisha aga Dunia,walio baki walimshauri Mh.Ndugai kwamba ingekuwa vema kama Serikali ya Tanzania ingefanya juu chini kushirikiana na China kwenye nyanja za viwanda,kilimo na ujenzi wa infrastructure nyingine za kuendeleza Tanzania,nadhani waligusia hata ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo - mwishowe wakamkumbusha Mh. Ndugai kwamba Tanzania ifanye hima kabla kizazi cha Uongozi wa Mao hakija toweka kabisa - kwa kuwa kizazi hicho ndio wanajua vizuri uhusiano mzuri uliyo kuwepo baina ya Tanzania na China wakati wa utawala wa Mao na Nyerer, bado wana influence kwenye utawala wa sasa wa Serikali ya China - kizazi kipya mahusiano mazuri ya zamani baina ya China na Tanzania hilo hawalijui ie tilia maanani hata kidogo. Mh.Ndugai is right,tukiwatumia Wachina kwa weledi watatufikisha mbali sana kimaendeleo.
Namshukuru sana Mh. Ndugai kuwa na ujasiri wa kumkumbusha Mama Samia kuhusu umuhimu wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo - mradi huo utatuinuwa sana kama Taifa Sceptics notwithstanding. Msikilizeni Mh. Ndugai kama alifanikiwa kupewe copy ya mkataba wa ujenzi na uendeshaji wa bandari ya B'moyo basi aubandike hapa ili kuwakata ngebe wale wote walio kuwa wamepania kuhujumu ujenzi wa Bandari ya B'moyo.