Ndugai amezidi kumsemea Magufuli, unaweza kudhani yeye ndiye msemaji na mteteaji wa Rais Magufuli!

BAHATI MBAYA SANA SPIKA ANASEMA MBOWE ANAJUA HATARUDI BUNGENI, WAKATI HATA SPIKA MWENYEWE HANA UHAKIKA WALA HAJUI KAMA NA YEYE WANANCHI WAKE WATAMRUDISHA TENA BUNGENI.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli spika wa bunge letu ni shida tupu! Anajuwa kweli kuwachonganisha wapinzani na serikali! Sjaona shida yoyote kwa Mbowe kama Mwenyekiti wa CHADEMA taifa kutofautiana kimtazamo na mwenyekiti mwenzie wa CCM, Kikatiba hii ndio kazi ya upinzani kuleta mawazo mbadala katika masuala ya kitaifa! Ikumbukwe tulishaondokana na ule mfumo wa "ZIDUMU FIKRA ZA MKT WA CCM"! Kwa sasa siasa zetu tulishaziingiza katika uwanja mwingine kabisa ulio mpana kuliko inavyozaniwa, Lakini ni viongozi wsetu akiwemo spika kujaribu kuendelea kulazmisha watu waishi katika mfumo tulokwishaachana nao! Pia spika anapaswa kutambua kuwa mwingi anaoupoteza bungeni kwa kuzungumzia mambo yasiyohusiana kabisa na uendeshaji wa bunge, matumizi mabaya ya madaraka na ufujaji wa fedha za umma kuliko hata fedha miln. 2 alizoshikia bango kwa Mbowe! Kurusha kipindi cha TV live kwa saa moja ni zaid ya milion 5, lakini ukihesabu muda anaoutumia spika kuongedlea mambo yake binafsi ni mwingi mno, awaonee huruma walipa kodi! Pia tunataka spika ajitahidi kutumia hekima na busara za kiti chake, mbona yeye mshahara wake na posho zake hataji au kutangaza hadharani? ..Anawataja wabunge wa upinzani kuwa hawatarudi tena bungeni, ana maanisha nini, Utafanyika wizi wa kura au hujuma gani!...Na aendelee kushukuru Mungu kuwa wapinzani nchini mwetu ni wapole na wanajikita zaidi katika hoja na wako tayari kujishusha ili tu Taifa letu liendelee kuwa na Amani ndio kila wakati pamoja na kutendewa unyama lakini wamekuwa wakitangaza msamaha, kinyume na hapo hapa nchini kungekuwa na habari nyingine!..
 
Ukimpima muenendo wake ni dhahiri shahiri kuna upendeleo binafsi anaoutafuta kutoka huko ingawa njia aliyoitumia si njema hata kidogo. Spika amekuwa mbaguzi wa kiwango cha kutisha sana

Nina imani hatarudi
Yaani anafikiri watu hatuoni anachofanya. Na hata akirudi, CCM wakimpitisha tena kuwa soika basi wana tatizo kuliko hata yeye!
 
Kigogo ameonyesha Ndugai anavyomsaidia Jiwe kukwapua hela... kuna docs kibao twitter
 
Ndugai anatakiwa kufahamu kuwa yeye sie msemaji wa wapiga kura wa Hai.
Anatakiwa kufahamu kuwa yeye ni mchanga ktk siasa na hawezi hata chembe kujilinganisha na Mbowe.
Ongea ya Mbowe kwa hoja na kupanga uongeaji kwa mtiririrko wenye mvuto ni tofauti kabisa na ndugai ambae ongea yake imejaa kejeli na mihemko mitupu.
 
Huyu jamaa anafanya saikolojia za kitoto sana!
 
Anamhofu naibu spika anaungwa mkono na mkuu .so nafasi yake ipo hatari,anafanya Kila namna kujipendekeza ili mh rais amuunge mkono bunge lijalo

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu ni sawa kabisa, yaani Ndugai yuko kwenye ushindani wa kujipendekeza kwa Magufuli ili aonekane bora kuliko Naibu Spika. Na ndio maana amejiweka katika nafasi ya kuamriwa na kufiata maagizo ya Magufuli katika kuendesha spika - ili kujijengea sifa kwa Magufuli aone aendelee kwa Spika Bunge lijalo. Masikini hajui kuwa Tulia ndio wanampangia kuwa spika.

Ndugai ni aina ya mtu atafanyakampeni dhidi ya Tulia ili asipute ubunge kwa ajili tu ya kutaka yeye aendelee kuwa spika. Hatari sana mtu huyu.

Anamwambia Mbowe harudi Bungeni - na yeye anapaswa kujua harudi kuwa Spika!
 
Analitia aibu ya kikatiba Taifa lako bila sababu za msingi kisa upinzani. Nani alikwambia upinzani uadui? Bunge sio muhimili tena wagogo hawana historia ya ujasiri ila vibaraka tu ndio kazi wanaweza.
aya maneno haya yangelimua yana pimwa kwa mizani ya uzito basi yangekua na uzito wa......

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tangu nilipoona ile picha anamrabua mtu fimbo ya kichwa hadi akazimia, nakubaliana na wewe 100%

Hivi kuna watu hawajui kuwa Ayubu Ndugai ni mgonjwa? Mtu alikaa India zaidi ya nusu mwaka akitumia takribani 1 Bilioni kwa matibabu.
Fedha hiyo ilipohojiwa na CAG, Ayubu Ndugai akaanzisha bifu na CAG kwa kumchongea kwa Jiwe mpaka wakafanikiwa kumng'oa!!

Kwa sasa Ndugai ana bifu na Mbowe na kama kawaida yake anawachonganisha Mbowe na Magufuli ili aone Mwisho wa Mbowe utakuwaje! Spika huyu ameonekana kuwa dhaifu sana kuliko Watangulizi wake wote!

Ni aibu kwa Spika Ndugai tena mwanamme mzima anazidiwa hekima na busara za Kusimamia na Kuongoza Bunge na Spika mwanamke aliyemtangulia Bi. Anne Makinda! Hakika Ni aibu.
Ogopa sana mtu mwenye Tatizo la Afya ya Akili. Mtu anayeamua kuchukua FIMBO NA KUMPIGA NAYO MTU MPAKA AKAZIMIA NI SAWA NA MUUAJI! Spika Ndugai ashukru Mungu kuwa yule MPINZANI wake alikuwa vizuri Kiafya otherwise leo hii Ndugai angelikuwa anatumika KIFUNGO CHA MAUAJI AU HUKUMU YA KIFO.
Leo eti ndiye Spika wa JMT......Spika mbabe, mnoko,mbeya, Mnafiki na mwongo mkubwa!!!
 
Kuna wakati niliwaambia watu wa CVM kuwa, kitendo cha Ndugai kumpiga mwanachama wa CCM mwenzake kwa fimbo hadi kuzimia, au hata mtu yeyote, ni kitendo cha ukosefu wa nidhamu wa hali ya juu kisichokubalika hata kidogo. Lakini kitendo cha CCM sio tu kutomchukulia hatua za kinidhamu kwa jambo hilo bali pia kumpitisha kuwa Spika wa Bunge la Tanzania, ni kitendo cha ukosefu wa nidhamu na maadili uliokithiri kwa CCM. Nikasema kwangu mimi Ndugai hana nidhamu, na CCM ni chama kisicho na nidhamu na maadili hata zaidi!

 
Unajua tatizo la Ndugai ni kwamba anajiona ana busara sana. NI aina ya watu ambao wanajiona wana hekima katika macho yao wenyewe.
Mwenye hekima na busara ya kweli hawezi kujaribu 'kuua' mtu ( awe MKONGWA, mwanachama mwenzie au hata mwinginewe ...... ) ili tu kupata uteuzi.
Polisi na hata hao maCCM waliompitisha, pamoja na yote aliyofanya na kuhatarisha maisha Ndg Chilon....... nao busara zao zina mapengo.Mamlaka ya uteuzi nayo ikamliwaza kwa u DC, nae akanywea.
Ni kwetu tu hapa, kwingine mtu aina hii, asingeweza kufikiriwa hata kupata hata huo uteuzi wa mgombea wa jimbo la Kongwa, baki ya kupata huu uspika ambao nao tunaona jinsi anavyozidi kuutukanisha.
 
Ni sahihi,kasahau kuwa yeye ni spika anaongoza muhimili unaojitegemea. Kwa alivyo Ndugai anaongeza kasi ya madai ya katiba mpya, ndugai kaonesha ni aina gani ya spika tunamhitaji, kama kwa aina ya uspika wa ndugai akikaa miaka kumi basi hsdhi ya taasisi hii itapotea kabisa,kwa hakika ndugai hajaitendea haki kabisa nafasi ya uspika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…