Ndugai amezidi kumsemea Magufuli, unaweza kudhani yeye ndiye msemaji na mteteaji wa Rais Magufuli!

Kuna wakati niliwaambia watu wa CVM kuwa, kitendo cha Ndugai kumpiga mwanachama wa CCM mwenzake kwa fimbo hadi kuzimia, au hata mtu yeyote, ni kitendo cha ukosefu wa nidhamu wa hali ya juu kisichokubalika hata kidogo. Lakini kitendo cha CCM sio tu kutomchukulia hatua za kinidhamu kwa jambo hilo bali pia kumpitisha kuwa Spika wa Bunge la Tanzania, ni kitendo cha ukosefu wa nidhamu na maadili uliokithiri kwa CCM. Nikasema kwangu mimi Ndugai hana nidhamu, na CCM ni chama kisicho na nidhamu na maadili hata zaidi!

View attachment 1454042

Speaker Job Ndugai is a Killer and Murderer.....!!
 
Good
Hii tabia ya Ndugai kumsemea Magufuli kwa watu anaokuwa na bifu nao inakera sana. Mtu yeyote mwenye akili anaelewa wazi hii ni saikoloji Ndugai anatumia kuchochea moto kati ya Magufuli na watu ambao Ndugai ana tatizo nao, hasa baada ya kumjua Magufuli ana silka ya namna gani.

Mfano ni pale alipokuwa na issue na CAG aliyepita Prof. Assad ambapo kila wakati alitoa matamko ya kumsema GAG dhidi ya raisi katika namna ya kumpandisha mori Magufuli dhidi ya Prof. Assad. Pia amefanya hivyo dhidi ya watu fulani ndani ya CCM ambao hapatani nao.

Na sasa yuko kwa Mbowe, yale yale ya wewe Mbowe raisi akishatamka usijifanye una mamlaka zaidi ya raisi, usijipime ubavu na raisi, nk. Toka lini Spika umekuwa msemaji au mteteaji rasmi wa raisi? Wenye akili tunajua Ndugai anachofanya hapa - kwamba hii ni saikoloji ya mtu dhaifu kumgonganisha mtu aliye na ugomvi naye dhidi ya mtu mwenye nguvu zaidi kwa faida yake mwenyewe.

Ndugai kama una tatizo na watu kabiliana nao bila ya kujifanya wewe unajua sana kumsemea na kumtetetea raisi dhidi yao. Siyo kazi ya Spika kumsemea na kumtetea raisi. Kazi zako za kuwa Spika wa Bunge zinakushinda sasa unaingilia madaraka yasiyo yako. Kama Mbowe kama mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani anakiuka utaratibu wa protokali dhidi ya kauli za Raisi wapo wanaostahili kushughulikia hilo, sio Spika.

Na kumbuka kwamba Mbowe kama mwenyekiti wa chama cha siasa kama alivyo Magufuli, ana wigo unaomruhusu kukosoa hadharani kauli za raisi - ndio maana ya siasa za upinzani ambazo wewe Ndugai unaonekana huzifahamu sawasawa.

Na tafadhali, tumia lugha ya kistaarabu unapoongelea viongozi ukiwa kama spika. Kuna maneno ambayo yanakuonyesha kuwa huna staha na unayatamka ukiwa na mavazi ya uspika. Inatia aibu. Kwa mfano, suala la mbunge fulani kuwa mtu wa ovyo, au hatarudi bungeni, ni fedhaha sana Spika kufikia kiwango cha chini kiasi hicho katika heshima ya kiti cha Spika. Ukisema mbunge fulani ni wa ovyo unatukana hata waliomchagua. Sasa spika huna uwezo wa kuona hilo?

Ulisamehewa kwa kumpiga mtu wa chama chako fimbo kichwani hadi akazimia kwa sababu tu za ushindani wa kisiasa. Ule ulikuwa ni utovu mkubwa na nidhamu kuliko wowote ambao Mbowe amewahi kuonyesha kwa raisi. Sasa jaribu kujiendesha kwa namna ambayo itawaonyesha wale waliokupa second chance kwamba hawakukosea.

Hata kama viongozi au wabunge wanakosea, wawe upinzani au chama chako, kuna namna ya nidhamu ya uspika inayotakiwa katika kushughulikia mambo kama hayo badala ya wewe kutumia nafasi hizo kujipendekeza kwa Magufuli. Hii ni pamoja na kutowasema kama watoto wadogo - mfano eti wanatangaza ugonjwa wa wabunge wanaokufa. Acha kuongozwa na hisia (emotions) unapokalia kiti cha spika.
 
Mwenye hekima na busara ya kweli hawezi kujaribu 'kuua' mtu ( awe MKONGWA, mwanachama mwenzie au hata mwinginewe ...... ) ili tu kupata uteuzi.
Polisi na hata hao maCCM waliompitisha, pamoja na yote aliyofanya na kuhatarisha maisha Ndg Chilon....... nao busara zao zina mapengo.Mamlaka ya uteuzi nayo ikamliwaza kwa u DC, nae akanywea.
Ni kwetu tu hapa, kwingine mtu aina hii, asingeweza kufikiriwa hata kupata hata huo uteuzi wa mgombea wa jimbo la Kongwa, baki ya kupata huu uspika ambao nao tunaona jinsi anavyozidi kuutukanisha.

Mashetani ni mashetwani tu usitegemee kupata Malaika miongoni mwa mashetwani!! CCM Ni walewale wanalindana na hasa shetwani moja linapoonekana kuwa na roho mbaya na katili kuliko mashetwani wenzake.
 
Mbowe anawatetea wakenya badala ya kujenga nchi yake.

Leo kaumbuliwa wakenya wameomba radhi kwa yote!

Mbowe hakuwa anatetea Kenya,Uganda wala Rwanda. Kati ya nchi hizi 3 nchi ambayo haina kifo hata 1 cha Covid-19 ni Uganda. Mwenzako akifanya vizuri Kuna ubaya gani kupongeza? Tatizo la Rais na Spika wa sasa UKIPONGEZA AU KUSIFIA nchi yoyote HUO SI UZALENDO baali ni UBEBERU(Kwa tafsiri ya neno "BEBERU" Awamu hii)!
 
Mashetani ni mashetwani tu usitegemee kupata Malaika miongoni mwa mashetwani!! CCM Ni walewale wanalindana na hasa shetwani moja linapoonekana kuwa na roho mbaya na katili kuliko mashetwani wenzake.
Kuna shetani moja kubwa ndio chanzo cha yote haya.
 
Naona hili neno uzalendo linategemea na mahali linapotumika. Linataka kuwa kama mabeberu.
Unapokosoa wewe siyo mzalendo.
Ukisifu na kupongeza wewe ndiye mzalendo.
Mkuu ukimsifu na kumpongeza Museveni kuhusu kufanikiwa kudhibiti Corona wewe sio mzalendo pia!
 
Waziri Mkuu Ndugai Raisi Magufuli? Nitaukana uraia. Kuishi Tanzania itakuwa sawa na kuishi mtaa ambao kichaa kapewa rungu!
Ndo kilichopo Mkuu, maana fununu ni et Samia anaenda kushika zenji,Majaliwa atapanda kuwa vice,so watu wanapigana vikumbo kuchukua nafasi ya Majaliwa.

Anajipendekeza mpaka JPM anamshangaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uspika ni mtamu jamani na jamaa anajua fika kuwa kuupata tena baada ya uchaguzi ni ngumu sana sawa na ngamia kupita kwenye tundu la sindano
 
Hii tabia ya Ndugai kumsemea Magufuli kwa watu anaokuwa na bifu nao inakera sana. Mtu yeyote mwenye akili anaelewa wazi hii ni saikoloji Ndugai anatumia kuchochea moto kati ya Magufuli na watu ambao Ndugai ana tatizo nao, hasa baada ya kumjua Magufuli ana silka ya namna gani.

Mfano ni pale alipokuwa na issue na CAG aliyepita Prof. Assad ambapo kila wakati alitoa matamko ya kumsema GAG dhidi ya raisi katika namna ya kumpandisha mori Magufuli dhidi ya Prof. Assad. Pia amefanya hivyo dhidi ya watu fulani ndani ya CCM ambao hapatani nao.

Na sasa yuko kwa Mbowe, yale yale ya wewe Mbowe raisi akishatamka usijifanye una mamlaka zaidi ya raisi, usijipime ubavu na raisi, nk. Toka lini Spika umekuwa msemaji au mteteaji rasmi wa raisi? Wenye akili tunajua Ndugai anachofanya hapa - kwamba hii ni saikoloji ya mtu dhaifu kumgonganisha mtu aliye na ugomvi naye dhidi ya mtu mwenye nguvu zaidi kwa faida yake mwenyewe.

Ndugai kama una tatizo na watu kabiliana nao bila ya kujifanya wewe unajua sana kumsemea na kumtetetea raisi dhidi yao. Siyo kazi ya Spika kumsemea na kumtetea raisi. Kazi zako za kuwa Spika wa Bunge zinakushinda sasa unaingilia madaraka yasiyo yako. Kama Mbowe kama mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani anakiuka utaratibu wa protokali dhidi ya kauli za Raisi wapo wanaostahili kushughulikia hilo, sio Spika.

Na kumbuka kwamba Mbowe kama mwenyekiti wa chama cha siasa kama alivyo Magufuli, ana wigo unaomruhusu kukosoa hadharani kauli za raisi - ndio maana ya siasa za upinzani ambazo wewe Ndugai unaonekana huzifahamu sawasawa.

Na tafadhali, tumia lugha ya kistaarabu unapoongelea viongozi ukiwa kama spika. Kuna maneno ambayo yanakuonyesha kuwa huna staha na unayatamka ukiwa na mavazi ya uspika. Inatia aibu. Kwa mfano, suala la mbunge fulani kuwa mtu wa ovyo, au hatarudi bungeni, ni fedhaha sana Spika kufikia kiwango cha chini kiasi hicho katika heshima ya kiti cha Spika. Ukisema mbunge fulani ni wa ovyo unatukana hata waliomchagua. Sasa spika huna uwezo wa kuona hilo?

Ulisamehewa kwa kumpiga mtu wa chama chako fimbo kichwani hadi akazimia kwa sababu tu za ushindani wa kisiasa. Ule ulikuwa ni utovu mkubwa na nidhamu kuliko wowote ambao Mbowe amewahi kuonyesha kwa raisi. Sasa jaribu kujiendesha kwa namna ambayo itawaonyesha wale waliokupa second chance kwamba hawakukosea.

Hata kama viongozi au wabunge wanakosea, wawe upinzani au chama chako, kuna namna ya nidhamu ya uspika inayotakiwa katika kushughulikia mambo kama hayo badala ya wewe kutumia nafasi hizo kujipendekeza kwa Magufuli. Hii ni pamoja na kutowasema kama watoto wadogo - mfano eti wanatangaza ugonjwa wa wabunge wanaokufa. Acha kuongozwa na hisia (emotions) unapokalia kiti cha spika.
Amazing speaker, unheard for, and unseen. One of the wonders of the World.
 
Ndo kilichopo Mkuu, maana fununu ni et Samia anaenda kushika zenji,Majaliwa atapanda kuwa vice,so watu wanapigana vikumbo kuchukua nafasi ya Majaliwa.

Anajipendekeza mpaka JPM anamshangaa

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, Majaliwa hawezi kuwa vice wakati Magufuli ni president. Raisi akitoka bara lazima vice atoke visiwani, na raisi akitoka visiwani lazima vice atoke bara. Kwa hiyo hizo fununu zina kasoro.
 
Amcheki mwenzie Nancy pelosi na Trump wanavyoishi, kama paka na panya
 
Uspika ni mtamu jamani na jamaa anajua fika kuwa kuupata tena baada ya uchaguzi ni ngumu sana sawa na ngamia kupita kwenye tundu la sindano
Anajisahau sana kwamba Magufuli does not need Ndugai kwa suala la Prof Assad, Mbowe wala mtu mwingine!
 
Back
Top Bottom