Ndugai amezidi kumsemea Magufuli, unaweza kudhani yeye ndiye msemaji na mteteaji wa Rais Magufuli!

Ndugai amezidi kumsemea Magufuli, unaweza kudhani yeye ndiye msemaji na mteteaji wa Rais Magufuli!

Ngoja tusubiri,ila kujipendekeza huku Ni anatafuta kitu

Sent using Jamii Forums mobile app
Anatafuta kuchaguliwa tena kuwa Spika na Tulia aachwe, wakati Tulia alishaambiwa atakuwa Spika kamili akishinda Ubunge Mbeya!

Tulia akishindwa ubunge na Sugu Ndugai atafanya sherehe kubwa sana!

Hivi umeona Sugu akiwa anaongea Bungeni Ndugai hamkatishi wala kumkosoa? Anampa nafasi ya kuonekana bora ili ajinadi na amshinde Tulia. Ndugai ana saikoloji za kitoto sana. Wenye akili walishamgundua.

Sikiliza hii clip utaona Ndugai anavyojaribu kumchimba Tulia kwa kumsupport Sugu, utaona Ndugai huwa hamuingilii ingilii akiwa anaongea tofauti na wapinzani wengine

View attachment 1422499
 
Spika anatimiza majukumu yake Mkuu

Sema ushabiki na mihemuko ya kisiasa Ndio unawatia upofu vijana wachanga kisiasa
Hivi umemuelewa kweli mtoa mada wewe!! Yaani kama vile umedandia gari usilojua linapoenda. Jifunze kutoa maoni yako kwa hoja
 
Mkuu ni sawa kabisa, yaani Ndugai yuko kwenye ushindani wa kujipendekeza kwa Magufuli ili aonekane bora kuliko Naibu Spika. Na ndio maana amejiweka katika nafasi ya kuamriwa na kufiata maagizo ya Magufuli katika kuendesha spika - ili kujijengea sifa kwa Magufuli aone aendelee kwa Spika Bunge lijalo. Masikini hajui kuwa Tulia ndio wanampangia kuwa spika.

Ndugai ni aina ya mtu atafanyakampeni dhidi ya Tulia ili asipute ubunge kwa ajili tu ya kutaka yeye aendelee kuwa spika. Hatari sana mtu huyu.

Anamwambia Mbowe harudi Bungeni - na yeye anapaswa kujua harudi kuwa Spika!
Kimsingi naibu YUPO makini anaelewa anachokifanya hata Kama mbunge wa kuteuliwa lakini Ana balance.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo ku
Hii tabia ya Ndugai kumsemea Magufuli kwa watu anaokuwa na bifu nao inakera sana. Mtu yeyote mwenye akili anaelewa wazi hii ni saikoloji Ndugai anatumia kuchochea moto kati ya Magufuli na watu ambao Ndugai ana tatizo nao, hasa baada ya kumjua Magufuli ana silka ya namna gani.

Mfano ni pale alipokuwa na issue na CAG aliyepita Prof. Assad ambapo kila wakati alitoa matamko ya kumsema GAG dhidi ya raisi katika namna ya kumpandisha mori Magufuli dhidi ya Prof. Assad. Pia amefanya hivyo dhidi ya watu fulani ndani ya CCM ambao hapatani nao.

Na sasa yuko kwa Mbowe, yale yale ya wewe Mbowe raisi akishatamka usijifanye una mamlaka zaidi ya raisi, usijipime ubavu na raisi, nk. Toka lini Spika umekuwa msemaji au mteteaji rasmi wa raisi? Wenye akili tunajua Ndugai anachofanya hapa - kwamba hii ni saikoloji ya mtu dhaifu kumgonganisha mtu aliye na ugomvi naye dhidi ya mtu mwenye nguvu zaidi kwa faida yake mwenyewe.

Ndugai kama una tatizo na watu kabiliana nao bila ya kujifanya wewe unajua sana kumsemea na kumtetetea raisi dhidi yao. Siyo kazi ya Spika kumsemea na kumtetea raisi. Kazi zako za kuwa Spika wa Bunge zinakushinda sasa unaingilia madaraka yasiyo yako. Kama Mbowe kama mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani anakiuka utaratibu wa protokali dhidi ya kauli za Raisi wapo wanaostahili kushughulikia hilo, sio Spika.

Na kumbuka kwamba Mbowe kama mwenyekiti wa chama cha siasa kama alivyo Magufuli, ana wigo unaomruhusu kukosoa hadharani kauli za raisi - ndio maana ya siasa za upinzani ambazo wewe Ndugai unaonekana huzifahamu sawasawa.

Na tafadhali, tumia lugha ya kistaarabu unapoongelea viongozi ukiwa kama spika. Kuna maneno ambayo yanakuonyesha kuwa huna staha na unayatamka ukiwa na mavazi ya uspika. Inatia aibu. Kwa mfano, suala la mbunge fulani kuwa mtu wa ovyo, au hatarudi bungeni, ni fedhaha sana Spika kufikia kiwango cha chini kiasi hicho katika heshima ya kiti cha Spika. Ukisema mbunge fulani ni wa ovyo unatukana hata waliomchagua. Sasa spika huna uwezo wa kuona hilo?

Ulisamehewa kwa kumpiga mtu wa chama chako fimbo kichwani hadi akazimia kwa sababu tu za ushindani wa kisiasa. Ule ulikuwa ni utovu mkubwa na nidhamu kuliko wowote ambao Mbowe amewahi kuonyesha kwa raisi. Sasa jaribu kujiendesha kwa namna ambayo itawaonyesha wale waliokupa second chance kwamba hawakukosea.

Hata kama viongozi au wabunge wanakosea, wawe upinzani au chama chako, kuna namna ya nidhamu ya uspika inayotakiwa katika kushughulikia mambo kama hayo badala ya wewe kutumia nafasi hizo kujipendekeza kwa Magufuli. Hii ni pamoja na kutowasema kama watoto wadogo - mfano eti wanatangaza ugonjwa wa wabunge wanaokufa. Acha kuongozwa na hisia (emotions) unapokalia kiti cha spika.
Tatizo kubwa kila mtu ni msemaji.
 
Tatizo ku
Tatizo kubwa kila mtu ni msemaji.
Du, afadhali hata angekuwa msemaji. Mie naona ni mropokaji tu. Umesikia kauli zake bungeni juu ya Mbowe kuumia? Yaani utafikiri alikuwapo akishuhudia tukio na anajua fact zote. Jamaa kaharisha maneno, sio kuongea.
 
MAGOGONI MODERN TAARAB
wametoa Album Mpya ina Ngoma Sita zote Kali
1.Mtu na akili yako unahoji tozo na Mkopo
2.Stress za 2025
3.Serikali ya Mpito
4. Watakao kusumbua ni Shati ya Kijani wenzio
5.Kuna Mawaziri Mmeanza Makundi Makundi yenu
6.kuna watu nitawapumzisha Wakajiandae 2025

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo la Ndugai ni kwamba ana miss sana enzi za Magufuli alivyojipa madaraka na umwamba, sasa hana tena, na ana hasira nyingi sana
 
Back
Top Bottom