Mtungi na utawala ni vitu viwili tofauti.
Kumbuka wananchi wanahitaji serikali ya ridhaa yao yenye kuwajibika kwao.
Iliyopo kasema mwenyewe ina majumba mabovu ya kumwaga ya kumwangukia mtu.
Ninakazia:
Sakata la Ndugai likifika mwisho kwa haki tutegemee:
1. Utawala na mihimili yenye uhuru kamili
2. Watawala kuwapo madarakani kwa ridhaa ya wananchi
3. Watawala kuwajibika kwa wananchi
4. Kuzaliwa kwa katiba mpya ya wananchi.
5. Kuzaliwa kwa Tanzania mpya.
Vita kwisha kwa haki haiwezi kuwa hisani bali kwa kupiganwa haswa!
Hii mbombo anapambana nayo Ndugai peke yake?
Wako wapi washirika?
Sakata la Ndugai: Mashabiki wako mkao wa Kula
Wewe uko upande gani mjomba?
Au umechagua kuwa shabiki (mpenzi mtazamaji) ukiwa mkao wa kula?