Ndugai avuliwe U-spika wa Bunge, kutokana na kuikanyaga Katiba ya nchi kwa kung'ang'ania kuwakumbatia wabunge wa viti maalum wa Chadema

Ndugai avuliwe U-spika wa Bunge, kutokana na kuikanyaga Katiba ya nchi kwa kung'ang'ania kuwakumbatia wabunge wa viti maalum wa Chadema

Yeye hawezi fuata katiba bali katiba itamfuata yeye.
 
Tunakemeaje mkuu Mystery?! Tunakemeaje?! Na sasa kuna wizara mpya ya kupambana na ‘freedom of speech’, Mawasiliano na Teknologia ya Habari!’ Hiki ‘kijiwe’ tu hapa, tutafutana, wee subiri tu!
santesandy
Ndiyo maana yake hao wanaowaita mabeberu wamegoma na tutazisikia kwenye bomba tu hizo shilingi trillion 2 zao kwa ajili ya kukuza Demokrasia nchini............

Hivi wazungu wanaleta hela zao kwa ajili ya kukuza Demokrasia, halafu wanagundua kuwa sisi tunaendelea kuiminya Demokrasia, hivi kweli hata kama pesa yao haina kazi, wataendelea kweli kutuletea hayo mapesa?
 
Ndugai anajivunjia heshima sana na kulidhalilisha bunge, kila mbunge anamizizi yake, mizizi imekatwa unashikiliaje huko juu,
Akifukuzwa wa CCM, kimya, cuf ya Lipumba kimya na unatekeleza taratibu, akifukuzwa wa chadema unajifanya unakingia kifua na ufuati taratibu, tabia hii hadi lini? Au kwa kuwa inampendeza jiwe, maana jiwe upenda uonevu na kuabudiwa!
 
t
Lakini kwa kuendelea kwa Spika Huyu, huoni kama Taifa tunapata aibu kubwa?

Hata Spika mstaafu katamka wazi kuwa, chama ambacho anadai kuwa ndicho kilichomdhamini kuja hapo Bungeni kikatamka tu kimeshamvua uanachama wake, automatically anaupoteza pia na huo ubunge wake..............

Hivi huyu Spika Ndugai anataka kutuambia kuwa hajui kusoma wala kuandika?
TATIZO LA KUPEANA "VYEO"! Ndugai hana sifa za kuwa "spika"(mkuu wa mhimili" wa nchi.Alitakiwa awe mkuu wa kitengo cha utafiti wa maumbile nyeti ya wanyama pori ktk chuo kinachotoa taaluma kiwango cha cheti! Alipo ni ngekewa ya ajabu sawa na jamaa aliyetajirika kwa kuangukiwa na jiwe la thamani ughaibuni!
 
Ndugai anajivunjia heshima sana na kulidhalilisha bunge, kila mbunge anamizizi yake, mizizi imekatwa unashikiliaje huko juu,
Akifukuzwa wa CCM, kimya, cuf ya Lipumba kimya na unatekeleza taratibu, akifukuzwa wa chadema unajifanya unakingia kifua na ufuati taratibu, tabia hii hadi lini? Au kwa kuwa inampendeza jiwe, maana jiwe upenda uonevu na kuabudiwa!
Hakika kwa kuwa anaicheza "tune" ya Jiwe ya kuvidhalilisha vyama vya upinzani, hususani Chadema, ndiyo hivyo tena Jiwe anachekelea hafi jino la mwisho............

Na huyo Spika anafuata nyayo za Bosi wake Jiwe kwa kuiona Katiba ya nchi kama takataka na hataki tena kuisimamia Katiba ya nchi aliyoapa kuitii na kuiheshimu...........

Lakini haya yote yana mwisho, hayataweza kudumu milele na milele
 
Mbona wakati CCM ilipowafukuza uanachama wao wa CCM, akina Sophia Simba, papo hapo walipoteza ubunge wao?

Mbona wakati chama cha CUF kimewavua uanachama wao, wabunge wake wa viti maalum, automatically walipoteza ubunge wao?

Iweje Leo wakati Chadema imewafukuza uanachama wabunge wao, kuwe na "double standard" ya utekelezaji wake?
Inategemea na mazingira na tafsiri ya sheria kwa mahitaji ya wakati huo. Huwezi kuitafsiri sheria kwa mrengo wa kumbeba adui.

Ndio maana hata Chadema wanapoogelea kutolewa kwa Hanje gerezani saa 1 usiku hawawaambii wanachama wao kuwa waliotolewa ni wengi akiwemo Twaha Mwaipaya. Usidhani ni wajinga, wanajua wanachokifanya.

Sasa hapa kuwa mpole kila mbuzi ale kwa urefu wa kamba yake.
 
Ebu mnijuze. Katiba ya Chadema inasemaje kama mwanachama atakiburuza chama mahakamani?
Hata kama inazuia mwanachama kwenda mahakamani bado mahakama itasikiliza na kutoa hukumu kwani ndio mhimili pekee unaoweza kutoa maamuzi katika mambo yanayohitaji tafsiri ya sheria kwa taasisi mbalimbali na watu binafsi. Ila katika kutoa maamuzi itajikita katika katiba, kanuni na utaratibu wa chama.

Kwa hiyo hakuna katiba inaweza kuzuia mwanachama wake kwenda mahakamani.
 
Tunajua kuwa sheria mama ya nchi hii ni Katiba ya Jamhuri wa Muungano, 1977, ambapo kila mwananchi anapaswa kuiheshimu na kuitii.

Viongozi wakuu wa serikali wanaapishwa kwa kuilinda Katiba hiyo kabla hatujawakabidhi madaraka hayo.

Katika kile tunachokiona watanzania kwa sasa kuona viongozi wetu wa serikaki kuidharau mno Katiba ya nchi na kuiona kama "toilet paper" Spika wa Bunge la nchi, Job Ndugai, amegoma kabisa kutambua mamlaka ya Chama cha Chadema, iliyoamua kuwavua uanachama wao wale wabunge 19 wa viti maalum katika kikao cha Kamati Kuu ya Chadema walichofanya hivi karibuni.

Katiba ya nchi ipo wazi katika suala hilo ambapo inatamka kuwa mbunge yeyote atapoteza ubunge wake pale chama kilichomdhamini mbunge huyo kabla ya kumvua uanachama wake.

Tunaomba Bunge la Jamhuri ya Muungano, ingawa tunajua kuwa ni la chama kimoja cha CCM, lakini katika suala hili inabidi wasimamie Katiba ya nchi na wasipepese macho na wamwambie Spika Ndugai kuwa kitendo chake cha kuisigina waziwazi Katiba ya nchi, ataipeleka nchi hii kwenye machafuko makubwa na wafanye maamuzi magumu kwa kumvua u-Spika wake wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Jambo jema ni kuwa hata aliyekuwa Spika mstaafu, Pius Msekwa, ambaye ni mwanaccm mwenzie amelifafanua suala hili kwa kutokuwa mnafiki kwa kueleza kuwa hao akina Halima na wenzie, ubunge wao umekoma pale Kikao cha Kamati Kuu kilipofanya uamuzi wa kuwavua uanachama wao.

Ninaloweza kumuuliza Spika Ndugai, hivi kwa kuendelea kuwang'ang'ania wabunge hao, watakuwa wa chama gani?

Kwa kuwa Katiba hairuhusu wabunge binafsi, hatujui hadi hivi sasa wabunge hao wanahesabika kuwa wa chama gani?

Kwa hiyo pamoja na kuelewa kuwa Spika Ndugai ana chuki kubwa na chama cha Chadema, lakini katika hili suala la wabunge wa viti maalum, inabidi akiri kuwa "amebugi step" kwa hiyo itamlazimu Spika Ndugai ajiuzulu wadhifa wake wa U- Spika ili kulirejeshea heshima iliyokuwa nayo Bunge letu na kama hataki basi wabunge wa CCM watende haki kwa kumfukuza Spika Ndugai mara moja, kwa kuwa ameliabisha sana Taifa hili ndani ya nchi na katika Jumuiya ya kimataifa, kwa kuona kuwa Spika wetu wa Bunge haitii na kuiheshimu kabisa Katiba ya nchi.

Kama kweli Taifa hili tunataka kuirejesha heshima yetu kama Taifa linaloheshimu sheria za nchi, Bunge linalazimika kumvua u-Spika Ndugai kwa manufaa mapana ya Taifa letu.

Hivi hilI bunge lilowekwa la kumwaga damu ni bunge halali ??
 
Muda wa kukata rufaa haujapita. Subirini wakate rufaa huenda maamuzi yakapinduliwa na baraza kuu. Wasipopata haki Baraza kuu wataenda mahakamani kuitafuta haki yao. Muda huo wote bado ni wabunge wenu kwa hiyo kuweni wapole.

Hata hivyo Chadema haina cha kupoteza hata kama wakiendelea kuwa wabunge kwani chenyewe hakina mpango wa kuteua wabunge[emoji1787].

Muda utaongea
Hadi hapo rufaa yao itakapokubaliwa wao si wanachama wa chama chochote cha siasa na kwa hiyo si wabunge. Rejea kesi ya Sophia Simba na wabunge wa CUF kambi ya Maalim za mwaka 2017 zilizoamuliwa na huyuhuyu Ndugai ambae leo anaamua kuisigina katiba.
 
Mkuu hebu rejea post yangu namba 26 hapo juu maana hicho unachosema nimeshakieleza.

Haijalishi nini, sheria ina tafsiri zake na ndio maana unaweza ukakuta Hakimu kamhukumu mtu lakini akikata rufaa anashinda.

Kwa hiyo sheria hutafsiriwa wakati mwingine kulingana na mazingira yaliyopo. Ndio maana hata wewe unarejea mazingira ya akina Sofia Simba na wale wa CUF.

Hata hivyo Chadema ikiwaacha wabunge 19 wakaendelea haina cha kupoteza kwani Chadema haina mpango wa kuteua wabunge Viti maalumu 🤣🤸‍♂️
 
Spika akili yake imeshaoza,ngoma imekimbilia kichwani.
 
Mkuu hebu rejea post yangu namba 26 hapo juu maana hicho unachosema nimeshakieleza.

Haijalishi nini, sheria ina tafsiri zake na ndio maana unaweza ukakuta Hakimu kamhukumu mtu lakini akikata rufaa anashinda.

Kwa hiyo sheria hutafsiriwa wakati mwingine kulingana na mazingira yaliyopo. Ndio maana hata wewe unarejea mazingira ya akina Sofia Simba na wale wa CUF.

Hata hivyo Chadema ikiwaacha wabunge 19 wakaendelea haina cha kupoteza kwani Chadema haina mpango wa kuteua wabunge Viti maalumu [emoji1787][emoji2223]
Suala siyo CHADEMA kupoteza ama kutopoteza bali ni kuheshimu katiba ambayo ni wajibu wa kila mtanzania.
 
Bunge limetokana na uchaguzi haramu na ndio maana kumesusiwa kupeleka majina ya viti maalum kwa sababu kuwa na wabunge katika hilo bunge ni sawa na kuhalalisha haramu. Ila hapo hapo kunalalamikiwa kwa kutofuatwa katiba katika bunge hilohilo lililo susiwa kwa sababu si halali.
 
Suala siyo CHADEMA kupoteza ama kutopoteza bali ni kuheshimu katiba ambayo ni wajibu wa kila mtanzania.
Katiba inasemaje?
Sheria na kanuni zilizoweka kutekeleza matakwa ya katiba zinasemaje?

Labda tuanzie hapo maana tunaweza kuwa tunabwabwaja tu katiba katiba kumbe hata kujua matakwa ya katiba hatujui.
 
Bunge limetokana na uchaguzi haramu na ndio maana kumesusiwa kupeleka majina ya viti maalum kwa sababu kuwa na wabunge katika hilo bunge ni sawa na kuhalalisha haramu. Ila hapo hapo kunalalamikiwa kwa kutofuatwa katiba katika bunge hilohilo lililo susiwa kwa sababu si halali.

Kipi kinaharamisha uchaguzi wa 2020.

Weka ushahidi, kama viongozi wenu hawaamini polisi na serikali ushahidi upelekwe jumuiya za kimataifa. Mnaleta porojo za unfunded claims on election fraud wakati mnajua kabisa wamepigwa kweupe. Mnaokoteza makaratasi mnayachoma. Mnatangaza mmekamata gari lina kura, gari lina usajili wa namba gani na mmiliki wake ni nani na kama mmelikamata ina maana lipo kwenye milki yenu, mmelipeleka wapi?

Hiki ni kichaa kama vichaa vingine unaletewa jambo unabeba tu hata hauongezi na za kwako.
 
Lakini kwa kuendelea kwa Spika Huyu, huoni kama Taifa tunapata aibu kubwa?

Hata Spika mstaafu katamka wazi kuwa, chama ambacho anadai kuwa ndicho kilichomdhamini kuja hapo Bungeni kikatamka tu kimeshamvua uanachama wake, automatically anaupoteza pia na huo ubunge wake..............

Hivi huyu Spika Ndugai anataka kutuambia kuwa hajui kusoma wala kuandika?
Mkuu mbona hili la wabunge wanawake 19 ni la kawaida sana. Kuna uwezekano CHADEMA bado hawajaandika barua ya kumfahamisha speaker kwamba wamewavua uanachama. Mimi naamini barua haijaandikwa ndio maana Mwenyekiti Mbowe kawafungulia milango na akawasihi waje waombe msamaha wayamalize

Jambo la ajabu kwangu ilikua ni yule Mbunge Mwambe ambaye mwenyewe alitangaza hadharani kuhama CHADEMA lakini spika akaendelea kumtambua kama mbunge halali
 
Ndizo hizo ninazosema "double standards" ambazo kama mhimili mmojawapo wa dola, Spika wa Bunge hapaswi ateleleze majukumu yake kiaona hiyo, kwa hiyo hakuna namna nyingine ya kulinda heshima yake na heshima ya Bunge la nchi, isipokuwa ni kujiuzulu tuuuuu
 
Kipi kinaharamisha uchaguzi wa 2020.

Weka ushahidi, kama viongozi wenu hawaamini polisi na serikali ushahidi upelekwe jumuiya za kimataifa. Mnaleta porojo za unfunded claims on election fraud wakati mnajua kabisa wamepigwa kweupe. Mnaokoteza makaratasi mnayachoma. Mnatangaza mmekamata gari lina kura, gari lina usajili wa namba gani na mmiliki wake ni nani na kama mmelikamata ina maana lipo kwenye milki yenu, mmelipeleka wapi?

Hiki ni kichaa kama vichaa vingine unaletewa jambo unabeba tu hata hauongezi na za kwako.
Hunijui sikujui,sasa nakushangaa unaongea kama unamungelea mtu unayemjua.

Mie sio hao unaowazungumzia hata hivyo pia huwezi kuwa na akili timamu ukasema et "mmepigwa kweupe" yani kwako wewe uchaguzi unaona ulikuwa sawa kabisa?
 
Tumpuuze huyu mtu kwani ni mwaharibifu wa kodi zetu huku akisigina katiba na sheria mbalimbali kiasi kwamba bunge limekuwa kijiwe cha porojo na umbea wakike kila kukicha! wabaki kama bunge la kamati ya ccm waamue watakavyo!
 
Back
Top Bottom