Ndugai avuliwe U-spika wa Bunge, kutokana na kuikanyaga Katiba ya nchi kwa kung'ang'ania kuwakumbatia wabunge wa viti maalum wa Chadema

Tunajua kuwa sheria mama ya nchi hii ni Katiba ya Jamhuri wa Muungano, 1977, ambapo kila mwananchi anapaswa kuiheshimu na kuitii.

Viongozi wakuu wa serikali wanaapishwa kwa kuilinda Katiba hiyo kabla hatujawakabidhi madaraka hayo.

Katika kile tunachokiona watanzania kwa sasa kuona viongozi wetu wa serikaki kuidharau mno Katiba ya nchi na kuiona kama "toilet paper" Spika wa Bunge la nchi, Job Ndugai, amegoma kabisa kutambua mamlaka ya Chama cha Chadema, iliyoamua kuwavua uanachama wao wale wabunge 19 wa viti maalum katika kikao cha Kamati Kuu ya Chadema walichofanya hivi karibuni.

Katiba ya nchi ipo wazi katika suala hilo ambapo inatamka kuwa mbunge yeyote atapoteza ubunge wake pale chama kilichomdhamini mbunge huyo kabla ya kumvua uanachama wake.

Tunaomba Bunge la Jamhuri ya Muungano, ingawa tunajua kuwa ni la chama kimoja cha CCM, lakini katika suala hili inabidi wasimamie Katiba ya nchi na wasipepese macho na wamwambie Spika Ndugai kuwa kitendo chake cha kuisigina waziwazi Katiba ya nchi, ataipeleka nchi hii kwenye machafuko makubwa na wafanye maamuzi magumu kwa kumvua u-Spika wake wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Jambo jema ni kuwa hata aliyekuwa Spika mstaafu, Pius Msekwa, ambaye ni mwanaccm mwenzie amelifafanua suala hili kwa kutokuwa mnafiki kwa kueleza kuwa hao akina Halima na wenzie, ubunge wao umekoma pale Kikao cha Kamati Kuu kilipofanya uamuzi wa kuwavua uanachama wao.

Ninaloweza kumuuliza Spika Ndugai, hivi kwa kuendelea kuwang'ang'ania wabunge hao, watakuwa wa chama gani?

Kwa kuwa Katiba hairuhusu wabunge binafsi, hatujui hadi hivi sasa wabunge hao wanahesabika kuwa wa chama gani?

Kwa hiyo pamoja na kuelewa kuwa Spika Ndugai ana chuki kubwa na chama cha Chadema, lakini katika hili suala la wabunge wa viti maalum, inabidi akiri kuwa "amebugi step" kwa hiyo itamlazimu Spika Ndugai ajiuzulu wadhifa wake wa U- Spika ili kulirejeshea heshima iliyokuwa nayo Bunge letu na kama hataki basi wabunge wa CCM watende haki kwa kumfukuza Spika Ndugai mara moja, kwa kuwa ameliabisha sana Taifa hili ndani ya nchi na katika Jumuiya ya kimataifa, kwa kuona kuwa Spika wetu wa Bunge haitii na kuiheshimu kabisa Katiba ya nchi.

Kama kweli Taifa hili tunataka kuirejesha heshima yetu kama Taifa linaloheshimu sheria za nchi, Bunge linalazimika kumvua u-Spika Ndugai kwa manufaa mapana ya Taifa letu.
Uongozi wote ccm ni wa hovyo mno!
 
Jaji Mkuu anasemaje?
 
santesandy
Ndiyo maana yake hao wanaowaita mabeberu wamegoma na tutazisikia kwenye bomba tu hizo shilingi trillion 2 zao kwa ajili ya kukuza Demokrasia nchini............

Hivi wazungu wanaleta hela zao kwa ajili ya kukuza Demokrasia, halafu wanagundua kuwa sisi tunaendelea kuiminya Demokrasia, hivi kweli hata kama pesa yao haina kazi, wataendelea kweli kutuletea hayo mapesa?
“Sisi ni matajiri, tuna pesa za ndani!” Ukweli ni kwamba ‘Mabeberu’ wapya ni mimi na wewe, tutatoa tu pesa!
 
Hiyo hiyo katiba ndio imempa kinga ya kutokushtakiwa popote
 
Naunga mkono hoja! Yaani tukisema hoja hii ipigiwe kura hope inaweza vuna kura za wananchi wote wenye umri wa kupiga kura!
 
Back
Top Bottom