Ndugai awaponda wana Mwanza kwa kuezeka nyumba zao na Mabati ya kizamani, Masufuria

Ndugai awaponda wana Mwanza kwa kuezeka nyumba zao na Mabati ya kizamani, Masufuria

Alimaanisha waweke mabati yenye rangi ya CCM kiutani na siyo kwamba wameweka ya kizamani.
 
Rais hawezi kuongeza mshahara mwaka wa majonzi kama huu!! Tumuenzi Magufuli kwa vitendo apeleke fedha zote kwenye Miradi ya maji.
unampangia rais cha kufanya.? Muda wa maombolezo umeisha kitaifa.

Kumuenzi magufuli kusifanye wengine wanyimwe haki zao za kikatiba.
 
Nadhani kaamua kumjibu shigongo maana naye alimpiga dongo Bungeni hivi majuzi.
 
Simpendi Ndugai ila katika hili namtetea. Huo ni utani wa wagogo na wasukuma, ndomana hakuwa serious kipindi anaongea.. kwahyo hizo ni tamaduni za kawaida
 
Rais hawezi kuongeza mshahara mwaka wa majonzi kama huu!! Tumuenzi Magufuli kwa vitendo apeleke fedha zote kwenye Miradi ya maji.
Majonzi ni kwako wengine ni mwanzo wa miaka ya neema
 
Simpendi job ila huo ni utani kwa watani zake
Ni utani tu kama alivyotangulia kusema. Ila ukimsoma between the lines anajaribu kutuma ujumbe serious kwa kutumia utani. Kuna ujinga mwingi unaendelea kwenye sekta isiyo rasmi ya ujenzi wa nyumba za makazi. Ukiachilia aina ya mabati (mi sina shida sana na aina ya mabati, nyumba yangu mwenyewe nimejengea "masufuria" na najenga kajumba kengine nako nitapaulia hayo mabati wanayoita masufuria). Shida niliyo nayo ni hii style ta kunyanyua paa hadi mawinguni. Yaani style hii ya upauaji ni ya kishamba sana na inaharibu kweli kweli shoo ya nyumba na makazi. Hakuna hata sababu zozote za taaluma ya usanifu majengo kuweka paa za dizaini hiyo, ni madaha tu yasiyo na sababu zaidi ya kuongeza gharama.
 
Akitoa salamu zake mbele ya raisi samia kwenye sherehe za wafanyakazi, spika wa bunge job ndugai amesema mwanza ingependeza kama wangeacha kuezeka nyumba zao kwa masufuria, akisema

"mwanza kunapendeza lakinni kwanini mnafunika nyumba zenu na masufuria? ,Ingependeza kama mngeezeka nyumba zenu na mabati ya kijani".

Hii ni dharau kubwa sana kwa mtu mkubwa kama spika kutoa dharau kwa watu ambao kipato chao ni kidogo na ndiyo maana nyumba zao wameezeka na mabati ya sufuria. Kweli viingozi wetu wakipata uwezo mkubwa wa fedha wanasahau kabisa kwamba kuna wengine hawana uwezo kama wa kwao .
MLETA HOJA utumie ubongo wako kutoa tafsiri sahihi.
#NDUGAI ni mgogo,kabila ambalo lina utani wa jadi na #WASUKUMA.

Pia alilitamka jambo hilo bayana kabla!

Na alichokimaanisha ilikuwa waondowe aluminium colour na waweke green colour ya #CCM.

Wewe umekirupuka toka huko na kuleta uchonganishi huku ﹰﹰJF.
FB_IMG_1619726835884.jpg
 
Back
Top Bottom