Behaviourist
JF-Expert Member
- Apr 8, 2016
- 39,926
- 95,626
😁😁😁
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mimi na CCM ni pete na kidole.swali mnamkumbuka au ndo mnacheza kila ngoma wanayopiga CCM?
Kuna haja gani upinzani kuingilia ugomvi wa Samia na ndugai?
mtadai lini haki zenu?
Inawezekana hata hana nia ya kugombea ila Mimi naona kilichomuuma nikwanini madarasa yajengwe kwa wingi Sasa hapo inawezekana kala mshiko wa shule binafsi anaogopa shule zisiendelee kustawishwa na kuongezeka iwapo mikopo itaendelea kujenga shule na kuchukua wanafunzi wengi waliofaulu kitendo kitachowapunguzia wanafunzi shule binafsi maana angekuwa na uchungu kweli na Nchi huko nyuma tungeshamuona akisimama pamoja na wananchi.kama angelikuwa na nia njema
Si angelipendekeza wabunge basi wapunguziwe mishahara minono na kukata maposho ili kuisaidia Seriali kupata pesa za ziada!
naona huko kubanana kwenyewe kunatuhusu zaidi sisi walala hoi tuu ambao wengi wetu mapato yetu ni duni sana vijisenti vichavhe tunavyotumiana kwenye mitandao ni ili kupunguziana makali ya maisha. SasaTozo ni janga kwa wanyonge.
Ndungai anatukejeli sisi Wanyonge na kutaka tubanwe zaidi.
Suala la kukopa linasababishwa na ongezeko la mahitaji ya Huduma za nchi kwa raia na wakati Mapato ni duni ,hayaendani na ukuaji wa mahitaji yetu kama Taifa. Hapo ndio kuoneha kuwa Serikali Ya ccm imeendelea Kushindwa kuleta uwiano wa Mapato na Matumizi.
Ndungai ni wale wale ,Walo shindwa Kuongoza Taifa Kufika kwenye Neema bila ya Madeni.
Mbona TZ ilishauzwa zamani? Mumesahau Enzi za Mkapa?
Mimi bila kujali usahihi wa chochote alichokizungumza Ndugai mbele ya wagogo wenzie, nafurahia sana matokeo yake na kinachoendelea sasa kwani jamaa ni mnafiki sana na Mungu hamfichi mnafiki.Mkuu we hukuwepo kwenye kile kikao kwa ufupi ndugai aliponda mkopo wa 1.3 bila chenga tena mkopo ilikuwa zuga tu hisia zake unaona kabisa anamdisi maza spana alizopewa ni haki yake kabisa.
Ushauri wako kwake (Ndugai) ni mzuri sana. Principally, hivyo ndivyo ilivyo, kwamba, mtu lazima asimame na kukutetea daima kile anachokiamini bila kujali matokeo yake...
Yesu Kristo Bwana na Mwokozi wa ulimwengu alisimamia kweli aliyoamini hata kama iligharimu UHAI wake...
LAKINI MIMI NAONGEZEA HAYA KWA AJILI YA WATU WA AINA YA CCM WENYE MAMLAKA NA MADARAKA YA KISERIKALI:
Kwamba, kwa mujibu wa mfumo wa utawala wetu "Rais" ni kila kitu. Obviously, Ndugai alipigwa upofu na ujinga wa kifikra hata akajikuta haoni nguvu ya mhimili wa "EXECUTIVE/U-RAIS" dhidi yake kiasi cha kuropoka na mdomo wake unamponza sasa...
Kina Ndugai hawa wana nafasi ya kutumia fursa hii waliyonayo kwa sasa kuleta usawazisho wa mfumo wetu wa utawala kwa kuhakikisha tuna katiba inayolinda na kuweka UHURU WA KWELI wa mihimili ya utawala (Bunge, Mahakama na Serikali/Executive)
Tungekuwa na uhuru wala kusingekuwa na mjadala wa maoni tu ya mtu tena ktk nafasi ya U - SPIKA aliyoyatoa kuhusu utendaji wa serikali...
Kwa kuwa hata Bunge/Spika hayuko huru, yupo pale kwa hisani ya Executive (Rais), alikuwa MJINGA SANA kupanua mdomo wake kukosoa mkono unaokupa kula...!!
Hii kazi alitakiwa awaachie kina Tundu Lissu, Freeman Mbowe na wengine kina sisi huku...
LABDA sasa akili zao hawa kina Ndugai zitaanza kuona na kuelewa kwanini watu wanataka KATIBA MPYA YA WANANCHI....
Tafadhari rudia bandiko hili kwa herufi kubwa nahitaji kuprint nikali laminateOgapa kitu kinaitwa "Karma"
Spika alichoongea siyo kitu kibaya hakutakiwa kuomba msamaha lakini naye alimuonea CAG Assad kwani naye hakuzungumza kitu kibaya kwahiyo muosha huoshwa.!
Hapana polepole hana mfano wa hili, polepole ni takataka tu maneno yk tumeweka kwa dustbin shida yetu ilikuwa ni huu muhimili ambao tunafanya nao kazi kwa upande mwengine vipi anageuka geuka halaf akagusia uchaguz wa 2025? Mama samia pasina shaka alimjua shida yake ni madaraka ya rais, Kwaiyo wacha yamkuteKwema wakuu!
Katika duru za kisiasa, kinachoendelea ni sakata la Mhe. Spika na Mkuu wa nchi, Mhe. Rais Samia.
Nimesikiliza pande zote mbili nikaona nami nitoe maoni yangu.
Kama mimi ndio ningekuwa Spika nisingeomba Msamaha, ningeweza kufafanua kauli zangu kwa namna ya kutetea kile nilichokuwa nakiamini.
Kitendo alichokifanya Ndugai ni kujisaliti yeye mwenyewe, kushindwa kutetea kile alichokiamini. Na hapa ndipo alipozidiwa na Ndugu Humphrey Polepole.
Sikuona sababu ya Spika kuomba msamaha wakati aliyoyasema yalikuwa ni dhahiri, kuhusu kukopa kaongea vizuri kabisa kuwa tusiwe taifa la kukopa kopa ingawaje hajakataza kukopa. Ndugai kwa upande wake kajaribu kutoa maoni yake kuwa yeye aliona bora kuminyana sisi kwa sisi kwa kutozana kodi kuliko kukopa kopa, huo ni mtazamo wake na ambao nafahamu wapo wengi watakaoungana na yeye kimtazamo na wapo watakaompinga vilevile.
Kitendo cha mtu kuomba msamaha kwa jambo alilolitenda kwa makusudi na ndicho anachokiamini ni kutia kitanzi mwenyewe na kutoa kibali cha upande wa pili kumshambulia atakavyo.
Kuomba msamaha sio ishara ya kukubaliwa isipokuwa kutangaza umeshindwa.
Kuomba msamaha kuna mata zaidi kama Mkubwa akimuomba mdogo msamaha lakini sio mdogo akimuomba mkubwa msamaha.
Mdogo akimuomba mkubwa msamaha huwa na mambo mawili, mosi; Unafiki kutokana na hofu kwa kuwa hana ubavu wa kupambana na mkubwa wake, mbili toba ya kweli ambayo hii wengi ni 10% lakini 90% ni unafiki
Lazima tujifunze kuwa Mtu mzima unapokosea kwa makusudi hata uombe msamaha haitabadilisha lolote upande wa pili, yaani tayari ushaondoa Uaminifu na kamwe huwezi kuurejesha.
Ndugai hakupaswa kuomba msamaha, angetulia na kuendelea na mambo mengine hii ingewapa kazi upande wa pili, lakini kujisalimisha ni kurahisisha kupigwa.
Ndugai pia kapoteza bara na pwani, wale waliokuwa wanamuunga mkono kwa mtazamo wake sasa wanamuona mnafiki, na wale aliowaponda wanakopa kopa pia wanamuona mnafiki hata angeomba msamaha kwa machozi ya damu.
Bora Polepole kabakiza uaminifu kwa wafuasi wake, wanamuona shujaa, na wanaweza kumsikiliza. Lakini sasa hivi nani atamsikiliza tena Ndugai, maana hata yeye mwenyewe hawezi kujisikiliza,
Hii inatupa fundisho sisi wengine wachanga namna ya kufanya maamuzi.
Kama utashindwa basi kwa nini uingie kwenye vita ambayo ulijua tangu mwanzo utashindwa na kudhalilika?
Wito; Kama Ndugai aliongea hayo akiwa na agenda ya siri kama ilivyotanabaishwa na Mhe. Rais basi awajibike au kuwajibishwa, lakini kama ni maoni yake binafsi na hakuna nguvu kutoka nje basi msamaha wake upokelewe.
Hata hivyo nafasi ya Urais sio ya mtu mmoja, hivyo yeyote anayetaka kuwania asionekane ni adui wa nchi.
Tuache demokrasia ichukue mkondo wake. Kutaka Urais 2025 sio dhambi wala sio kosa la jinai. Labda wanaotaka wawe wanahujumu utendaji kazi wa Serikali iliyopo madarakani lakini kama ni kuikosoa kwenye mapungufu yake ili ionekane haina sifa ya kuendelea 2025 hilo sio kosa kimsingi.
Tujenge nchi
Hapana polepole hana mfano wa hili, polepole ni takataka tu maneno yk tumeweka kwa dustbin shida yetu ilikuwa ni huu muhimili ambao tunafanya nao kazi kwa upande mwengine vipi anageuka geuka halaf akagusia uchaguz wa 2025? Mama samia pasina shaka alimjua shida yake ni madaraka ya rais, Kwaiyo wacha yamkute
Alipofeli ndugai ni kwamba hakuweka hakiba juu ya mtu aliye juu yake kimadaraka., apo tuu
Should go., atafanya vipi kazi mazingira yalivyo sasa na mamaSo mpaka sasa hakuna tumaini kwa spika?