Ndugai: Lishe duni ya wachezaji wetu imechangia Taifa Stars kufungwa

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema miongoni mwa sababu iliyochangia Stars kupoteza mchezo wa kwanza jana dhidi ya Senegal ni lishe duni ya wachezaji wetu.

Spika Ndugai ameyasema hayo muda mfupi baada ya kuwasili Dar es Salaam akitokea Misri aliposhuhudia mchezo wa kwanza wa Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Senegal na Tanzania uliomalizika kwa Taifa Stars kuchapwa 2-0.

Ndugai alisema ukiangalia kwa umakini utaona wale wachezaji wa timu pinzani walikuwa na miili mizuri ambayo inatokana na lishe nzuri.

"Kuna umuhimu wa kuwapa wachezaji wetu lishe nzuri ya kutosha ili kushindana na wapinzani wa aina ya Senegal," alisema Ndugai.

Katika hatua nyingine Ndugai alisema viongozi wengi wa soka na michezo mingine hapa nchini siyo watu sahihi wa kuongoza.
Ni sahihi alichokisema,ila mifumo ya vilabu vyetu hairuhusu hayo. Wachezaji wanaibuka tu kama majini, hawakulii kwenye academies, kila mtu anajua anachokula huko kwenye familia yake,wengine walevi, malaya hakuna must diet walizojiwekea, unategemea nini hapo?
 
Kwahiyo Kwa akili yako ilivyo fupi mh ndugai Senegal Wana miili mikubwa Kwa sababu wanakula vizuri??? What a waste! Imagine huyu ni spika wa Bunge!
Ndugu mlo mzuri unachangia kuwajenga wachezaji kimwili
 
Mambo ya udumavu unaosababishwa na lishe duni upo lakini pia ni species za kitanzania,waganda wana Vimo vya average ya John Boko lakini waliwamudu wakongo wenye miili dizaini ya Senegal urefu na unene
Ko sio sahihi moja kwa moja kusema hiyo ndio sababu,kwa mpira gani tuliocheza hadi hiyo iwe sababu? Species za West/Central and North Africa ni giants kuliko east Africa anbapo wengi ni moderate,wasukuma ni jamii ya west africa

East Africa Tanzania ndio kwenye udumavu mkuu, Kenya na Uganda asili yao ni miili mikubwa kwa maana ya vimo na maumbile..tuangalie aina lishe zetu tukiwa watoto na kipindi cha ujauzito wa wake zetu..

Special research inahitajika hapa ili kujenga generation ya watu wenye akili, nguvu, kujisimamia na kujielewa - tunakwama hapa.
 
Dah inasikitisha sana. Yaani tunashindana kuiponda timu yetu wenyewe? Kama Spika kasema haya kakosea sana.

Timu yetu ilijitahidi na hicho ndicho walichopata. Tuwatie moyo kwa michezo ijayo na tujifunze kwa wenzetu namna wanavyoweza
Ha ha ha kuna ukweli hapo ndugu
 
kama posho zao mmewadhulum hadi wakatishia kugoma watapata wapi lishe nzuri
 
..nilivyouangalia ule mchezo sikuona kama Wasenegali walituzidi kwasababu tuna maumbo madogo kulinganisha na wao.

..Kwa maoni yangu, wachezaji waliokuwa uwanjani wana miili inayowawezesha kushindana ktk mechi za kiwango chochote kile.
Hiyo ilichangia pia,wachezaji wetu walikuwa wanapoteza mipira sana aidha kwa kupiga pasi za hovyo au kuzidiwa ubavu na wasenegal wanapokuwa one to one
 
East Africa Tanzania ndio kwenye udumavu mkuu, Kenya na Uganda asili yao ni miili mikubwa kwa maana ya vimo na maumbile..tuangalie aina lishe zetu tukiwa watoto na kipindi cha ujauzito wa wake zetu..

Special research inahitajika hapa ili kujenga generation ya watu wenye akili, nguvu, kujisimamia na kujielewa - tunakwama hapa.
Uliona ya mechi ya Congo na Uganda? Nani alikuwa mrefu na mwenye miili mikubwa?
Ukiwachukua waganda na Tzn au wakenya utaona wao ni warefu hata hapa Tzn huko kaskazini wajaluo kurya etc ni warefu kwani huko hakuna utapia mlo?
Sikatai utapia mlo upo lakini sio kigezo pekee ishu ni specie mkuu,sio kila mfupi ni utapiamlo bali genes za hivyo ndo maana kwenye ulinganifu wa akili au IQ kimo sio ishu
 
No
Kwahiyo Spika Ndugai anasema kuwa viongozi wa michezo waliopo sasa ni DHAIFU? Aletwe na pingu hapa nilipo(utani wa Mngoni na Mgogo)!
[/QUOTE
East Africa Tanzania ndio kwenye udumavu mkuu, Kenya na Uganda asili yao ni miili mikubwa kwa maana ya vimo na maumbile..tuangalie aina lishe zetu tukiwa watoto na kipindi cha ujauzito wa wake zetu..

Special research inahitajika hapa ili kujenga generation ya watu wenye akili, nguvu, kujisimamia na kujielewa - tunakwama hapa.
mkuu ugali maharagwe ni Janga kwa Taifa ,vijana wa kitanzania wanapoanza kukuku wanatakiwa kwenda shule za secondary ,kwa miaka sita mtoto anakula wale maharagwe kwa kipindi chote ,hivi unategemea kuja kupata kijana mwenye nguvu hapo ,hata umpe vidonge hataweza kuwa na stamina inayotakiwa mchezoni ,mfano halisi ni hashim Thabeet ambae talent alikuwa nayo lakini alishindwa kuhimili mikiki ya mchezo husika
 
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema miongoni mwa sababu iliyochangia Stars kupoteza mchezo wa kwanza jana dhidi ya Senegal ni lishe duni ya wachezaji wetu.

Spika Ndugai ameyasema hayo muda mfupi baada ya kuwasili Dar es Salaam akitokea Misri aliposhuhudia mchezo wa kwanza wa Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Senegal na Tanzania uliomalizika kwa Taifa Stars kuchapwa 2-0.

Ndugai alisema ukiangalia kwa umakini utaona wale wachezaji wa timu pinzani walikuwa na miili mizuri ambayo inatokana na lishe nzuri.

"Kuna umuhimu wa kuwapa wachezaji wetu lishe nzuri ya kutosha ili kushindana na wapinzani wa aina ya Senegal," alisema Ndugai.

Katika hatua nyingine Ndugai alisema viongozi wengi wa soka na michezo mingine hapa nchini siyo watu sahihi wa kuongoza.
Apendekeze wawe wabunge wa viti maalum, watapata lishe ya kutosha na kuvimbiwa
 
..nilivyouangalia ule mchezo sikuona kama Wasenegali walituzidi kwasababu tuna maumbo madogo kulinganisha na wao.

..Kwa maoni yangu, wachezaji waliokuwa uwanjani wana miili inayowawezesha kushindana ktk mechi za kiwango chochote kile.
Mbona walikuwa wanashindwa kuwanyanganya mpira wachezaji wa Senegal kitaalam wanasema one to one battle Wachezaji wetu wialionekana dhahiri kushindwa
 
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema miongoni mwa sababu iliyochangia Stars kupoteza mchezo wa kwanza jana dhidi ya Senegal ni lishe duni ya wachezaji wetu.

Spika Ndugai ameyasema hayo muda mfupi baada ya kuwasili Dar es Salaam akitokea Misri aliposhuhudia mchezo wa kwanza wa Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Senegal na Tanzania uliomalizika kwa Taifa Stars kuchapwa 2-0.

Ndugai alisema ukiangalia kwa umakini utaona wale wachezaji wa timu pinzani walikuwa na miili mizuri ambayo inatokana na lishe nzuri.

"Kuna umuhimu wa kuwapa wachezaji wetu lishe nzuri ya kutosha ili kushindana na wapinzani wa aina ya Senegal," alisema Ndugai.

Katika hatua nyingine Ndugai alisema viongozi wengi wa soka na michezo mingine hapa nchini siyo watu sahihi wa kuongoza.
Tatizo hapo ni ccm
 
Ndugai alisema ukiangalia kwa umakini utaona wale wachezaji wa timu pinzani walikuwa na miili mizuri ambayo inatokana na lishe nzuri.
Lishe nzuri anamaana gani ............!!?

Hawapati lishe ya kutosha au wanapata lishe duni .............!!?
 
Back
Top Bottom