Ndugai: Lishe duni ya wachezaji wetu imechangia Taifa Stars kufungwa

Ndugai: Lishe duni ya wachezaji wetu imechangia Taifa Stars kufungwa

Hivi hao wachezaji wakisema nchi yetu inayumba kwasababu bunge ni dhaifu, wataitwa mbele ya kamati ya maadili?
 
Mambo ya udumavu unaosababishwa na lishe duni upo lakini pia ni species za kitanzania,waganda wana Vimo vya average ya John Boko lakini waliwamudu wakongo wenye miili dizaini ya Senegal urefu na unene
Ko sio sahihi moja kwa moja kusema hiyo ndio sababu,kwa mpira gani tuliocheza hadi hiyo iwe sababu? Species za West/Central and North Africa ni giants kuliko east Africa anbapo wengi ni moderate,wasukuma ni jamii ya west africa

Kwa hiyo Jiwe wa West????!!! Sasa hiyo 9 spika mwenyewe mdumavu na anamjua Diego, Mesi au Salah??? Mengine yaacheni yapite tu
 
Kwa hiyo Jiwe wa West????!!! Sasa hiyo 9 spika mwenyewe mdumavu na anamjua Diego, Mesi au Salah??? Mengine yaacheni yapite tu
Jiwe awe wa west kwani mrefu? Si ndio common type za kibongo?
Nachokataa ufupi kwa wabongo iko related na specie na genes kuliko lishe duni,ingekuwa ni lishe basi warefu wote wangekuwa smart kichwani na wafupi wote wangekuwa dungaembe sasa haiko hivyo
Kingine hata utumwa ulikuwa zaidi West Africa ambako kuna giants people kuliko east Afrika ambako waarabu waliiga tu,kule watu ni wakubwa ila hawana akili ile miili ni kukabiliana na harsh conditions
 
Jiwe awe wa west kwani mrefu? Si ndio common type za kibongo?
Nachokataa ufupi kwa wabongo iko related na specie na genes kuliko lishe duni,ingekuwa ni lishe basi warefu wote wangekuwa smart kichwani na wafupi wote wangekuwa dungaembe sasa haiko hivyo
Kingine hata utumwa ulikuwa zaidi West Africa ambako kuna giants people kuliko east Afrika ambako waarabu waliiga tu,kule watu ni wakubwa ila hawana akili ile miili ni kukabiliana na harsh conditions

Namaanisha tumefungwa na timu bora kuliko sisi sasa sababu za kijinga ndio hatutaki. Timu yetu na maandalizi yetu bado yanafanya tusiwe washindani wazuri sie tunawekeza katika maombi na zari sasa sababu za Ndugai ndio kaongea ujinga.
 
Acha upimbi kuwa na mwili ambao umeshiba sio lazima uwe na kitambi wewe.Umemuona Samatta alivyo na nguvu kuliko hata john Bocco ambae mwili mkubwa tu lakini nguvu hana.
Nawe unaungana na sabufa?
 
..nilivyouangalia ule mchezo sikuona kama Wasenegali walituzidi kwasababu tuna maumbo madogo kulinganisha na wao.

..Kwa maoni yangu, wachezaji waliokuwa uwanjani wana miili inayowawezesha kushindana ktk mechi za kiwango chochote kile.

Kweli kbs najaribu kuwatafakari wachina wana umbo dogo lkn wapo World Cup
 
Dar es Salaam. Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema miongoni mwa sababu iliyochangia Stars kupoteza mchezo wa kwanza jana dhidi ya Senegal ni lishe duni ya wachezaji wetu.

Spika Ndugai ameyasema hayo muda mfupi baada ya kuwasili Dar es Salaam akitokea Misri aliposhuhudia mchezo wa kwanza wa Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Senegal na Tanzania uliomalizika kwa Taifa Stars kuchapwa 2-0.

Ndugai alisema ukiangalia kwa umakini utaona wale wachezaji wa timu pinzani walikuwa na miili mizuri ambayo inatokana na lishe nzuri.

"Kuna umuhimu wa kuwapa wachezaji wetu lishe nzuri ya kutosha ili kushindana na wapinzani wa aina ya Senegal," alisema Ndugai.

Katika hatua nyingine Ndugai alisema viongozi wengi wa soka na michezo mingine hapa nchini siyo watu sahihi wa kuongoza.

Source : Mwananchi
Wachezaji wetu hawajapitia misingi ya mpira wamejikuza wenyewe tu,tukiwekeza ndiyo tulaumu saizi hakuna mtu wa kumnyoshea kidole mwenzake
 
Ni Kweli.
Wachezaji wetu wana tatizo la Lishe Duni.
Mishahara wanayopata haikidhi kupata chakula kinacho kidhi kwa mchezaji wa Soka.
Pia hawali kutokana na maagizo ya wataalamu wa afya ya Soka.
 
Spika wa bunge kwa hili umekosea sana. Huwezi kuwa kiongozi wa Serikali ukatumia kodi yetu vibaya kwamba unaenda kuwapa support wachezaji, matokeo yake wewe unaanza kuwaponda. Eti tumefungwa kwa sababu hatuli.

Hivi ni kweli hatuli au ni maumbo yetu? Hivi kessy hata akila usiku na mchana kama mchwa atarefuka ili apambane na Senegal.

Jambo la pili unasema tumefungwa kwa sababu ya viongozi wabaya wa mpira. Pale viongozi ulitaka wafanyeje? Au ulitaka wamwingile kocha majukumu yake kama unavyofanya mara zote.

Nimekusikia tena unasema kuna kiongozi mdogo hajitambui bila shaka huyu ni makonda kutokana na alichomwambia Rais.

Makonda yuko sahihi ndiyo maana umeona watanzania hawawalalamikii wachezaji bali kocha maaana yeye alipaswa kufanya zaidi ya hicho alichofanya kama fiziki hiyo ni kazi ya kocha.

Mheshimiwa tambua wewe ni kiongozi hupaswi kuwa na maoni binafsi kwa namna yoyote ile unapoongea na public.

Maoni tuachie sisi wadau wengine. Inabidi kama kiongozi ujitafakali. Naona utaanza kupambana na huyo kiongozi kijana kwa sababu amekuchallange na kukonyesha wazi ulichokosea.
 
Back
Top Bottom