Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kondoa kimezindua rasmi kampeni zake za Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kondoa Mji, Makoa Ally ambapo mgeni rasmi alikua Spika wa Bunge na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Job Ndugai.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Spika Ndugai amewaomba wananchi wa Kondoa wasifanye makosa katika kuchagua wawakilishi wanaojua kero zao na wenye kuweka mbele maslahi yao ili waweze kuwasemea.
" Ndugu zangu nyie wote mmejionea jinsi Dk Magufuli alivyoufanya mkoa wetu wa Dodoma kupanda chati, uchumi wetu sasa hivi umekua baada ya kuwa makao makuu ya serikali huku yeye mwenyewe akihamia hapa, nini cha kumpa zaidi ya kura za kishindo?
Mimi ndio Spika wa Bunge, nawajua wabunge wote, hao wapinzani hawajawahi kuwatakia maendeleo watanzania maana wao kila kitu hupinga tu, wanasema Rais anatumia hela hovyo kununua Ndege lakini kesho utawakuta wamezipanda, wanatumia barabara za lami kwenye kampeni zao lakini wanasema hakuna lililofanyika.
Kondoa ni wakati wa kuamka na kutoa kura nyingi za kuwafanya wapinzani wajute kwanini wameshiriki uchaguzi huu, niwahakikishieni mkimleta Makoa bungeni nitamsaidia sana katika kuwaletea maendeleo," Amesema Ndugai.
Kwa upande wake mgombea Ubunge wa Jimbo hilo la Kondoa Mji, Makoa Ally amesema anafahamu changamoto nyingi zinazowakabili wananchi wa Kondoa lakini kero ya Maji ndio kipaumbele chake cha kwanza.
" Najua kuna mambo mengi ya kufanya ila nyinyi wenyewe ni mashahidi kwamba hakuna jambo la muhimu Kondoa kwa sasa kama Maji, niwaombe nipeni ridhaa ya kuwa Mbunge wenu nikashughulike na maji ili dhana ya kumtua mwanamama ndoo kichwani iweze kutumia," Amesema Makoa.
Naye Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na msanii wa Bongo Fleva, Keisha amewaomba watanzania na wananchi wa Kondoa kuchagua mafiga matatu ya CCM ili yaweze kufanya kazi kwa ushirikiano na kusukuma gurudumu la maendeleo mbele.
" Chagueni Rais, Wabunge na Madiwani wetu, msipowachague wote kwa pamoja mnakwamisha maendeleo maana wapinzani wale ni kupinga tu sasa watu wanaopinga maendeleo ni ngumu kuikumbusha serikali iwajengee visima vya maji maana wao wanasubiri serikali ijenge ili wapinge, naombeni msifanye kosa Oktoba 28, kura zote kwa CCM," Amesema Keisha.