Uchaguzi 2020 Ndugai: Mimi ndio Spika wa Bunge, nawajua Wabunge wote. Hao wapinzani hawajawahi kuwatakia maendeleo watanzania maana wao kila kitu hupinga tu

Jobu ndio spika wa kwanza duniani kua na marukanga,yani anagharamiwa mabilioni ķununua mbolea ili afya ikae sawa
 
Kumbe Bado Ni speaker! Mpaka Hapo atakapoteuliwa mwingine!!...Au u speaker kapita Bila kupingwa!!!
 
Nasikia Kongwa inaizidi Tarime kwa maendeleo na huduma za jamii!!
 
Umeandika hoja gani hapa? Hewa tupu
 
 
Umeandika hoja gani hapa? Hewa tupu
Wilaya Kongwa kuna maendeleo gani katika kipindi chote ulichokuwa mbunge? Hufai kuwa mbunge hata umetuharibia heshima ya bunge lililoachwa na Anna Makinda.
 
 
Serikali imenunua ndege halafu inazikodisha kwa ATCL,imenunua ndege 16 kwa cash, hela zilizo tumika ni nyingi mno kiasi kwamba zimedidimiza uchumi wa watu.

ATCL ingeweza kukodi ndege kutoka kwenye mashirika mengine na akaendesha shughuli zake hela zinazo tumika kwenye ndege zingeweza kutumika katika shughuli zingine za maendeleo zenye tija zaidi na zinazo gusa watu wengi.

Sekta binafsi ingeweza kuwekeza kwenye sekta ya usafiri wa anga kama wanavyo fanya Precission Air,

Ndege zinaweza kununuliwa kwa mkopo na sio kwa cash na kwa mkupuo kama hivi sasa ilivyo.

Tunaumiza wananchi
 
Wewe ndiyo spika ila pia ni kada na mbunge wa CCM! Na CCM wapinzani wao wakuu ni Chadema, sawa na Yanga kuisifia Simba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…