Clark boots
JF-Expert Member
- Jun 5, 2017
- 6,770
- 6,202
Nasema haya yote kutokana na mienendo yake mbalimbali na matatizo yanayomkuta huyu Spika wa bunge hasa toka afariki JPM. Nadiriki Kusema anachukiwa na watu tena wengi kwa sababu, Huyu ni Spika ambaye hata akifanya au kuongea Jambo dogo tu lazima watu wamnange. Kunangwa huku kunadhihirisha kabisa kuwa huyu Spika ana damu ya kunguni na hapendwi na watu tena wanatamani hata leo hii ajiuzulu.
Rejea Ile hotuba yake siku Ile anasema kuwa watu wanamsema sana na kumchafua huko mitandaoni sio kwamba ana baya lolote au mapungufu yoyote hapana Ila kwa kuwa yeye ni MGOGO na akadhihirisha kuwa hii ni DHARAU. Binafsi siwezi kukubali kuwa anasimangwa na kuandikwa vibaya kwa kuwa yeye ni Mgogo kwani wagogo wamefanya nini, mbona wako wengi tena wenye nafasi kubwa Serikalini Ila hawasemwi kama yeye?
Sasa basi huu ni wakati wa kujitafakari kabisa kwake, awe mpole, mtulivu, mnyenyekevu, aache kiburi na majigambo hasa kwenye vikao vyake afikirie sana maneno ya kuzungumza.
Nimpe pole sana Mhe: Spika Ndugai kwa kipindi hiki kigumu anachopitia naamini fika kuwa mwaka aliumaliza vibaya na bado yupo Frustrated and Stressed Ila hamna namna apambane kiume maisha ya kuongoza watu yanahitaji uvumilivu sana na ushujaa wa hali ya juu asipokuwa makini kile kitu atakiona kichungu sana na atatamani 2025 iwe hata kesho kutwa ili angoke chap.