Ndugai: TANESCO ni kikwazo kikuu kwa maendeleo ya Watanzania

Wakiwa nnje ndio wanajifanya kuongea ukwel na akili kuwarudi.
 
Kikwazo kikuu kwa maendeleo ya taifa la Tanzania ni Ccm, na yeye ni mmojawapo wa Wana ccm walio endeleza hicho kikwazo, atoe kelele tuu asubirie siku ya hukumu akamuonyshe yesu mke wake
 
Duuh, Ila wafanyakazi wa TANESCO wameshindwa kabisa kuendesha kampuni hii kwa faida na matokeo mazuri

Kwani si walibinafsishe hili Shirika?

Hovyo kabisa.
Uwajibikaji haupo,
Innovation inapigwa vita,
Rafiki yangu mmoja ambaye ni mfanyakazi wa hapo katika Project yake moja alikuja na Project fulani ambayo ni vital kwenye baadhi ya technicality za Umeme.

The guy came na idea ya kutambua katizo la umeme ambalo badala ya kutafuta manually kungekuwa na program maalum ya Computer ambayo ingekuwa inaonesha exactly tatizo la kukatika kwa umeme lipo wapi hasa kwa maeneo ambayo nguzo zimepita Porini.

kwa namna alivyonieleezea ilikuwa ni ku-code nguzo zote then faulty ikitokea system inaonesha kuwa umeme umeishia Pole X hivyo hauvuki kwenda Pole Y hivyo mafundi straight wanaenda pointi hizo na kukagua hitilafu inaweza kuwa imesababishwa na nini. of coz huu ulikuwa mwanzo mzuri i expected over time ingeweza kueleewa exactly nini tatizo o mafundi wakitoka ofisni they direct collect entire spares na kuelekea kwenye eneo lenye hitilafu ( Kumbuka hii kitu imefanywa sana Manually nakumbuka hawa jamaa walikuwa wanaweza poteza 18 hours kutafuta faulty iko wapi hasa kwa ameneo ambayo nguzo zimepita porini au maeneo complex)

Aliingia gharama kuangiza devices nje ili kufanya simulation, na ilifanikiwa kupita pale chuoni kwake, ilipofika Govt ndipo ilianza kukwamishwa na watu ambao wamewekwa kutatua changamoto za watanzania. From there jamaa hakutaka tena kuendelea anafanya issue zake na maisha yanasonga mbele.

Ninachotaka kusema ni kuwa baadhi ya watoa maamuzi they only tends to support mambo ambayo wana maslahi nayo, kwa hali kama hii tusitegemee kama tutakuja kusonga mbele. Mchawi wa maendeleo yetu ni hawa watoa maamuzi wenye maslahi binafsi!
 
Duuh, Ila wafanyakazi wa TANESCO wameshindwa kabisa kuendesha kampuni hii kwa faida na matokeo mazuri

Kwani si walibinafsishe hili Shirika?

Hovyo kabisa.
Ni shirika gani lililo chini ya Serikali.liliwahi kuendeshwa kwa ufanisi? Tatizo ni Serikali.

Mashirika ya umma yamekuwa mahali pa kutunzia ndugu, marafiki na chawa wa watawala, bila ya kujali uwezo wa hao watu. Wameshindwa kuendesha bandari, utegemee wamudu umeme?
 
Ameongea jambo la maana ila halina maana kwa sasa.
Ilitakiwa mambo km hayo angeyasema kipindi amekalia kile kiti pale bungeni ingeeleweka.
 
Spika aliyeondolewa kwa uonevu ndugu Job Yustus Ndugai amelitupia lawama Shirika la umeme la Tanzania kwa kuwa ndilo hasa linalo kwamisha maendeleo ya Watanzania kwa desturi yake ya kukata umeme hovyo hovyo.

-----
View attachment 2815240

Spika wa Bunge Mstaafu Job Ndugai, ameitaka Serikali kuboresha taratibu zake katika kuwahudumia wananchi ikiwemo kutenga fedha za kutosha kutekeleza miradi, huku akionyesha kukerwa na kukatika kwa umeme.

Ndugai ambaye pia ni Mbunge wa Kongwa, ameyasema hayo wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, iliyotembea na kukagua miradi mbalimbali ambapo amesema kukatika umeme kunarudisha nyuma nyuma jitihada za wananchi katika kujiletea maendeleo kupitia viwanda mbalimbali vya uzalishaji.

"Tanesco (Shirika la Umeme Tanzania) ni lazima mwende na nia aliyonayo Mheshimiwa Rais, baadhi ya desturi zenu lazima zibadilike ili muepushe kero hizi kwa wananchi," ameonya Spika huyo Mstaafu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kongwa, mkoani Dodoma.

Aidha kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumatano Novemba 15, 2023 na kitengo cha mawasiliano cha mkoa wa Dodoma, Ndugai amesema ni jambo muhimu kwa serikali kutenga fedha zinazotosheleza kutakidhi mahitaji ya wananchi.

“Tunashukuru jitihada za Serikali za kuwaletea Wananchi Maendeleo. Wito wangu kwa Serikali Kuboresha taratibu zake katika kuhudumia Wananchi ikiwemo kutenga fedha zinazojitosheleza kutekeleza miradi mbalimbali ili kukidhi mahitaji ya wananchi,” amesema.

Naye Katibu wa CCCM Mkoa wa Dodoma, Pilli Mbaga amepongeza wilaya hiyo kwa kutekeleza Ilani ya CCM ya mwaka 2020 hadi 2025 na kuwataka wananchi kuendelea kuiamini Serikali ya Awamu ya Sita.

“Tunawapongeza kwa kazi nzuri iliyofanyika. Wananchi tuendelee kuiamini Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais wake Samia Suluhu Hassan, kwani imedhamiria kutatua kero zinazowakabili wananchi,” amesema.

Aidha, Mbaga amewataka madaktari na wauguzi kuwa na kauli nzuri kwa wagonjwa ili kutimiza dhamira nzuri ya Serikali ya kutoa huduma bora kwa wananchi wake.

Katika ziara hiyo, kamati ya Siasa ya Mkoa imetembelea na kukagua miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa barabara ya kiwango Cha lami ya Mwalimu Nyerere yenye urefu wa Kilometa moha ambayo imejengwa kwa tamani ya Sh487.19 milioni.

Miradi mingine ni ujenzi wa Miundombinu katika Hospitali ya Wilaya wenye thamani ya Sh4.64 bilioni unaohusisha wodi tatu za wagonjwa na jengo la mama na mtoto na kisima cha maji katika Kijiji Cha Laikala "B" wenye thamani ya Sh780.56 milioni, Shule ya Msingi Moleti iliyojengwa kwa thamani ya Sh318.8 milioni.

Mradi mwingine ni kuboresha umeme kwa ajili ya kutatua kero ya umeme hafifu kwa Wilaya za Kongwa, Mpwapwa mkoani Dodoma na Gairo iliyopo mkoani Morogoro.

Ujenzi huo unaohusisha njia ya msongo wa Kilovoti 33 kutokea kituo kidogo cha Zuzu hadi Mbande wenye thamani ya Sh5.1 bilioni.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi
Hii nguchiro kumbe bado ipo duniani
 
Duuh, Ila wafanyakazi wa TANESCO wameshindwa kabisa kuendesha kampuni hii kwa faida na matokeo mazuri

Kwani si walibinafsishe hili Shirika?

Hovyo kabisa.
Sikumbuki vizuri ila makamba alishawahi kuliombea trioni kadhaa .sina uhakuka alifanya nini
 
ni speaker alieponzwa na ulimi kuteleza na kuropokea muhimili mkuu kwa upotoshaji
 
Back
Top Bottom