Ndugai: Tumshughulikie Zitto kama Bunge la Marekani linavyomshughulikia Rais Trump

Yanayomtokea Makonda si ajabu yakamtokea kiongozi mwingine wa muhimili mkuwa wa nchi hii.Endeeleni kufanya upuuzi wenu tu
 
Huyu ndie Spika wa bunge la Tanzania. Mhimili unao jitegemea.
Yaani tatizo za Rais Tramp ni tofauti kabisa na issue ya Zitto. Wabunge wa Marekani wana pinga usaliti wa Taifa.
Zitto ana pinga maamuzi ya serikali.. Hajawa na mtazamontofauti na Taifa. Kwanza Zitto ana tetea Taifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli bunge la Marekani linamshughulikia Raisi, lakini tuangalie, wanavyoitumia sheria na mwenendo wanaoufatualia.

Kuna wabunge wa chama atokacho Raisi, ambao kura zao zinampinga raisi wa chama chao, jee kwetu inawezekana???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Spika awaandikie WB barua awaambie hayo niawaxo yake na sio msimamo wa bunge inatosha
 
Ni heri kuwa masikini wa kipato, umasikini wa fikra ni ugonjwa.
 
Kwa kitendo alichokifanya Zitto Kabwe kwa Wamarekani kwao angenyongwa na kuvifuta vizalio vyake. Lakini utaona Wamarekani wanamkumbatia kwasababu anawewezesha kutaka Tanzania isitawalike.
Huyu Zigo ni adui namba 1 wa Watanzania .
Kwa Waliosoma Zamani watanielewa
 
Kama suala ni kumshughulikia Rais Trump, mbona Ndugai anakaa kimya JPM anapovunja katiba?

Na yeye ashughulikiwe pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mlimshughulikia Sugu mpaka kipaza sauti kikang'olewa wakati hakuwa na kosa lolote kama ilivyothibitishwa na mahakama zaidi ya kosa kuwa mbunge wa Chadema, bunge ni lenu CCM mnyang'anyeni ubunge kama mlivyomnyang'anya Lissu.
 

Hivi chenji zimeeisha za kununulia ndege cash [emoji383]? Kwa nini musijenge shule na madawati kwa cash kama ununuzi wa ndege?
 
Zitt ni mhaini na Mhujumu namba 1 wa Tanzania, nitaanza si muda mrefu kupost uchafu wa Anti Zigo
 
Nimeusikiliza huu mjadala, kiukweli baadhi ya wabunge wametoa kauli kali na hatarishi, ikiwemo kauli ya kifo kwa Mhe. Zitto Kabwe.

Naendelea kusisitiza kuhusu kauli huumba, kauli kama hii ilitolewa kumhusu Lissu na mara ikatekelezwa, sasa ni kumhusu Zitto, bahati nzuri Zitto ni mtu wa Kigoma, mwisho wa reli, na kule kwao, kaaga!, likimtokea la kutokea, kwa mujibu wa Zitto mwenyewe, hawa waliochangia adhuriwe, kule majumbani kwao, hakuta salia hata panya alive!.

P
 
Acha kwanza mambo ya kauli huumba, twende kwenye heshima ya bunge letu na umoja wake.
Nani sasa hivi anaweza kuliona tena hili bunge kama chombo chenye heshima na muhimu katika uendeshaji wa nchi?
Na aibu kubwa ni kuwa mpuuzi anaye ropoka maneno kama hayo sio mbunge wa kuchaguliwa na wananchi bali wa kuteuliwa na Rais, jee Rais kwa nini katika nafasi zake adimu kabisa alizopewa kweli anaweza kuliletea bunge mshenzi kama huyu? Naita mshenzi maana mtu anayemtakia kifo mwakilishi wa wananchi ndani ya bunge anastahili kuitwa nani zaidi ya mshenzi?
Na kwa nini ndani ya bunge zikija hoja za kipumbavu huoni wakipewa wawakilishi wenye heshima zao na akili kuxungumza zaidi ya watu wa dizaini ya Bulembo, Kessy, Lusinde , Msukuma, Goodluck nk? Ndugai kwake anaona mpangilio huo ndio unamsaidia lakini wenye akili ndani ya bunge kimya?
Bora hata mijadala yetu bar inaweza kuwa na hoja kuliko bungeni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi hii hela wanayoitoa serikali kuwezesha elimu bure, kwa nini isingetumika kufanya maboresho kwanza ya miundo mbinu ya elimu kama kununua madawati ya kutosha, kujenga madarasa ya kutosha, kuboresha ofisi za waalimu, kusambaza umeme kwenye mashule nchi nzima, kujenga computer lab na kununua vifaa. Wakati wananchi wakiendelea kulipa iyo ada ya 75,000 kwa mwaka. Tatizo letu hatuna mipango mizuri ndio maana hadi leo tuna matatizo ya msingi kama elimu,ujinga na maradhi. Hivi kuna siku itafika na sisi tutengeneze silaha za nuklia au tutume wanasayansi mwezini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…