Ndugai yuko sahihi - hatutakiwi kukopa kujenga madarasa, vyoo, zahanati, madawati, hivi tufanye kwa tozo na kodi

Ndugai yuko sahihi - hatutakiwi kukopa kujenga madarasa, vyoo, zahanati, madawati, hivi tufanye kwa tozo na kodi

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,407
Nimejaribu kufuatilia kinachoendelea mpaka nikashangaa watanzania walivyo mbumbumbu, nilivyomsikia ndugai sidhani kama alimaanisha watanzania tusikope kabisa bali ametizama matumizi ya mkopo wa trilioni 1.3 tuliokopa ili tujenge madarasa n.k akatazama kwenye bajeti yetu tulisema tunaweka tozo za miamala kwa ajili ya ujenzi wa madaarasa.

kweli binafsi namuunga mkono hatutakiwi kukopa mikopo nje kujenga madarasa, kujenga vyoo, kununua madawati, hivi ni vitu tufanye kwa fedha zetu za kodi na michango.

Sasa kama chama fulani wana utaratibu wa kutoshauriana, wanasapoti chochote ambacho serikali inafanya basi sisi watanzania tusio makada tutakuwa mbumbumbu tukibeba haya na kushangilia.

Kazi ya bunge ni kushauri serikali, hivyo spika kusema mtizamo wake ulio tofauti na msimamo wa serikali ni jambo la kupongeza
 
Je, ilifaa kukopa kununua mwewe, je vipi ilifaa kukopa kununua viwashio vya moto, na je ilifaa kukopa kuunda nyoka mrefu na je ilifaa kukopa kutengeneza madari?
 
Tumehama kwenye zama za uchochezi tupo kwenye zama za taharuki.

Likisemwa jambo lenye ukweli kwa sasa ni taharuki si uchochezi.

Watu wataporwa madaraka na vyeo sababu wataambiwa wameleta habari za taharuki kwa wananchi.
 
Nikiwa nimekaa hapa nikiota moto, imenijia akilini kuwa maadui wetu wa maendeleo TZ ni watatu tu.

• Uchawa ProMax wa Viongozi na Vijana wa UVCCM
• Kipaumbele Ni kwenye Next Election na sio Next Generation
• Presence of many Clueless Citizens

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ila watu huwa mnavichwa vizito kuelewa hivi hotuba ile ulifatilia yote mbn hilo lilifafanuliwa vizuri
 
Nimejaribu kufuatilia kinachoendelea mpaka nikashangaa watanzania walivyo mbumbumbu, nilivyomsikia ndugai sidhani kama alimaanisha watanzania tusikope kabisa bali ametizama matumizi ya mkopo wa trilioni 1.3 tuliokopa ili tujenge madarasa n.k akatazama kwenye bajeti yetu tulisema tunaweka tozo za miamala kwa ajili ya ujenzi wa madaarasa...
Ni kweli kabisa mkuu. Alichoongea spikani sahihi kabisa. Huwezi kukopa halafu unaenda kujenda madaras na vyoo. Investment hii ni ndogo sana haihitaji hela ya mkopo toka nchi za nje.

Tatizo mwenyewe kagwaya halafu anaomba msamaha wakati aliongea ukweli kabisa. Wacha tu wamnange mgogo yule kama alivyojiita mwenyewe. Sisi tunamwona ni mtanzania halafu yeye anasema hapendwi kwa sababu ya ugogo wake!!!
 
Nchi inayo ongeza kwa umbumbu mwingi ni tanzania .hoja hazijibiwi sasa kazi iliyobaki kimshambulia speaker ili wale teuzi
 
Nimejaribu kufuatilia kinachoendelea mpaka nikashangaa watanzania walivyo mbumbumbu, nilivyomsikia ndugai sidhani kama alimaanisha watanzania tusikope kabisa bali ametizama matumizi ya mkopo wa trilioni 1.3 tuliokopa ili tujenge madarasa n.k akatazama kwenye bajeti yetu tulisema tunaweka tozo za miamala kwa ajili ya ujenzi wa ma...
SGR gharama yake ni trilioni 14 yaani dola bilioni saba. Ni pesa nyingi sana huwezi kuzipata kwa kutegemea tozo zinazokatwa kupitia miamala ya simu.

Ni mradi mkubwa wenye gharama kubwa, na maji tumeshayavulia ngua hatuna budi kuyaoga.
 
SGR gharama yake ni trilioni 14 yaani dola bilioni saba. Ni pesa nyingi sana huwezi kuzipata kwa kutegemea tozo zinazokatwa kupitia miamala ya simu.

Ni mradi mkubwa wenye gharama kubwa, na maji tumeshayavulia ngua hatuna budi kuyaoga.
ndugu yangu achana na kuweka mambo yote kwenye kapu moja.

hakuna mtanzania anayepinga kukopa kujenga SGR, kukopa kujenga Bwawa wa maji, n.k

hawa wanasiasa wanatuchezea akili kwa kujitetea wakisimama kwenye haya.

hoja ni tumekopa trilioni 1.3 na tumezitumia kujenga madarasa, hiyo ndiyo mikopo ya kipuuzi.

hakuna anayepinga kukopa kujenga SGR au bwawa
 
Wanaokopa kujenga nyumba za kuishi? Inatia hasira kuona watu wanabwabwaja. Kwahiyo wanafunzi wasome wapi?
 
ndugu yangu achana na kuweka mambo yote kwenye kapu moja.

hakuna mtanzania anayepinga kukopa kujenga SGR, kukopa kujenga Bwawa wa maji...
Unasema ni ya kipuuzi kwa sababu wewe unaishi mjini na huna uhusiano wowote na huo mkopo. Pesa za mahitaji mengine zinatokana na tozo.

Tunachosahau ni kuwa kuijenga hii nchi kwa kasi kubwa alianza JPM huyu wa sasa anaendeleza tu.
 
Nimejaribu kufuatilia kinachoendelea mpaka nikashangaa watanzania walivyo mbumbumbu, nilivyomsikia ndugai sidhani kama alimaanisha watanzania tusikope kabisa bali ametizama matumizi....
Mwenyewe ashaomba radhi basi sasa mwambie afute basi naona toka jana kabana kimya huko aliko
 
Wanaokopa kujenga nyumba za kuishi? Inatia hasira kuona watu wanabwabwaja. Kwahiyo wanafunzi wasome wapi?
Haihitaji mkopo kujenga darasa labda ingekuwa shule.

Kila kata yenye upungufu wa madarasa wananchi wachangie.

Tatizo ni kufanya mambo kwa dharura/zimamoto
 
Tatizo zimeenda kulipa denI la vikoba,
 
Wamehujumu Shuler binafsi wakaenda kukopa pesa za matundu ya vyoo akili matope
 
figa moja limeenda kujiweka chini ya figa jingine, hilo sufuria liko salama?
 
Back
Top Bottom