Ndugai yuko sahihi - hatutakiwi kukopa kujenga madarasa, vyoo, zahanati, madawati, hivi tufanye kwa tozo na kodi

Ndugai yuko sahihi - hatutakiwi kukopa kujenga madarasa, vyoo, zahanati, madawati, hivi tufanye kwa tozo na kodi

Ni kweli kabisa mkuu. Alichoongea spikani sahihi kabisa. Huwezi kukopa halafu unaenda kujenda madaras na vyoo. Investment hii ni ndogo sana haihitaji hela ya mkopo toka nchi za nje. Tatizo mwenyewe kagwaya halafu anaomba msamaha wakati aliongea ukweli kabisa. Wacha tu wamnange mgogo yule kama alivyojiita mwenyewe. Sisi tunamwona ni mtanzania halafu yeye anasema hapendwi kwa sababu ya ugogo wake!!!
Yuko sahihi, madarasa vyoo nk hivi vingejengwa na mapato ya ndani. Viongozi wetu hawana dira ya nini kifanyike cha kulete maendeleo. Nakumbuka nikisoma shule ya N/A mwaka 1958 kila kitu kilikuwepo kutokana na kodi za wananchi. Fedha za mkopo si za kujengea shule ni za kulete maendeleo .
 
Yuko sahihi, madarasa vyoo nk hivi vingejengwa na mapato ya ndani. Viongozi wetu hawana dira ya nini kifanyike cha kulete maendeleo. Nakumbuka nikisoma shule ya N/A mwaka 1958 kila kitu kilikuwepo kutokana na kodi za wananchi. Fedha za mkopo si za kujengea shule ni za kulete maendeleo .
Ulisoma 1958? Shikamoo mkuu.
 
Hata kama mkopo Una 0% interest?
Seems wengi humu si wafanyabiashara.
 
Ndani ya miaka 3 jinsi ya kuleta maendeleo na kumaliza tatizo la ajira nchini.

1.Ondoa futa kodi zote za kuingiza magari ya mizigo na abiria nchini kodi yake utaipata mara mbili yake kupitia indirect tax.Kwenye mafuta,leseni za udereva,fine za traffic, parking fee,ushuru wa stand,spare za magari,leseni na vibali mbalimbali.Gari moja uajiri si chini ya vijana 3.

2.Toa ruzuku kwenye viwanda vya kuzalisha matrekta wazalishe matreka mengi waje watuuzie wakulima kwa robo bei trekta moja uajiri zaidi ya watu wanne.

3.Jenga schemes za umwagaliaji KILA kijiji upitapo mto pande zote mbili watu walime mwaka mzima ni aibu sana kwa maji ya mito kumwaga maji yake baharini badala ya mashambani.Soko la mazao nje ya nchi lipo tele.

4.Jenga vyuo vya ujuzi kila kata kopesha vijana ujuzi baada ya kumaliza darasa la saba wakapate ujuzi wautakao. Kukopesha vijana waende chuo kikuu kisha warudi mtaani kuendesha bodaboda na kuwa machinga ni upotevu Mkubwa Sana wa kodi zetu na kuongeza idadi ya masikini nchini.

5.Fungua mipaka watu wauze watakapo nje ya nchi kuna masoko tele.Legeza masharti ya vibali Ili export ikue. Ni sekta mbili tu zingine takataka hazifikii kilimo na madini kwa kuajiri vijana wote nchini na kuongeza pato la taifa bila kutegemea kukopa na kukamua kodi wananchi.

6.Peleka KILA kijiji mashine za kutengeneza interlocking block na vigae Ili watz wote wajenge nyumba bora kwa gharama nafuu kabisa
Mjerumani kwa miaka 15 alituletea maendeleo makubwa Sana CCM imeshindwa nini.

Tukope kwa ajili ya uzalishaji na sio kujenga madarasa, wakishapata vyeti watakula vyeti?
 
Nimejaribu kufuatilia kinachoendelea mpaka nikashangaa watanzania walivyo mbumbumbu, nilivyomsikia ndugai sidhani kama alimaanisha watanzania tusikope kabisa bali ametizama matumizi ya mkopo wa trilioni...
Hotuba ya Ndugai itaishi miaka mingi sana na kama hawatachukua tahadhari alizosema Ndugai, basi itawaprove wrong.
 
Back
Top Bottom