Ndugu Bashe, ulimaanisha nini uliposema Mashamba ya kulima miwa yabadilishwe yawe ya mpunga?

Ndugu Bashe, ulimaanisha nini uliposema Mashamba ya kulima miwa yabadilishwe yawe ya mpunga?

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
21,625
Reaction score
33,688
Salaam, Shalom!!

Ulipokuwa mbunge kabla ya kupewa Uwaziri ulionekana kama mzalendo wa Kweli Kwa HOJA ulizojenga!!

Ulimaanisha nini?

1. Kwamba, mpunga unaweza kuwa mbadala wa sukari?

2. Kwamba Ajira ambazo zinatolewa na viwanda vya sukari, zikipotea, Watanzania hao waende wapi?

3. Hiyo chain ya billion of shillings inayotengezwa na wakulima,vwasafirishaji, wafanyabiashara, ushuru na Kodi vikipotea, utafaidika na nini?

4. Kwamba kiafya sukari fake ya GMO ya Bei Chee Toka Thailand, Brazil na Dubai Ina ubora sawa na sukari yetu ya Kagera na Morogoro?

5. Kwamba tufunge viwanda vya sukari vinavyoexport sukari nje ya Nchi na kuleta dollar, Kisha Serikali ipate wapi pesa za kigeni kuagizia sukari?

6. Kwamba uliagizwa kuwa waziri wa KILIMO Ili kuua kabisa viwanda vya kuzalisha sukari Badala ya kuvikuza na kuviongeza?

Unasuburi nini Ofisini Hadi sasa, unataka Hadi ufukuzwe sio?

Basi endelea kusubiri!!!

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿.

Karibuni 🙏
 
Sijui ni mara nagapi CCM watuonyeshe kwamba hawastahili kushika madaraka. Kuna mambo anaongea waziri tena mwenye elimu nzuri tu unabaki kujiuliza mbona katema chenga tu na wananchi wa jimbo lake watamrudisha tena madarakani wakipewa kanga na kofia.
 
sijui ni mara nagapi ccm watuonyeshe kwamba hawastahili kushika madaraka.... kuna mambo anaongea waziri tena mwenye elimu nzuri tu unabaki kujiuliza mbona katema chenga tu.... na wananchi wa jimbo lake watamrudisha tena madarakani wakipewa kanga na kofia
Sijui nini kimempata Bashe!!

Ni shinikizo, au ufahamu wake umetekwa!!

Na hatumii kilevi kusema kwamba labda alitamka hayo sababu ya ulevi wa pombe!!
 
Hiyo kauli ya Bashe kwamba mashamba ya miwa hata yakigeuzwa kuwa ya mpunga ni sawa tu, ni kauli ya kifedhuri, kibri, jeuri, na dharau kubwa sana.

Badala ya kuinua sekta, yeye anaweka mipango ya kuua sekta na kuhujumu nchi.

That is beyond repair!

-Kaveli-
 
Badala ya kuishauri Mifumo ya JAMII kuzidi kuwekeza katika KILIMO Cha miwa na viwanda vya sukari,

Yeye anataka vifungwe,

Kwani Huwa anapata commission yoyote vikitokewa vibali vya kuagiza sukari nje?
 
Sijui nini kimempata Bashe!!

Ni shinikizo, au ufahamu wake umetekwa!!

Na hatumii kilevi kusema kwamba labda alitamka hayo sababu ya ulevi wa pombe!!
Entitlement/umwamba, wamesifiwa sana. Na ni tabia ya wanasiasa kuona wao ndio wenye akili na mawazo ya kipekee uliko wengine. Na ukiwakosoa ndio utajua kiwango cha viburi vyao.

Kifupi tunajisahaulisha kwamba mawaziri, wabunge, DC, DED wote ni wanasiasa, hakuna cha maana toka kwao isipokuwa ajenda za kisiasa(ulaghai).
 
Entitlement/umwamba, wamesifiwa sana. Na ni tabia ya wanasiasa kuona waonndio wenye akili na mawazo ya kipekee uliko wengine. Na ukiwakosoa ndio utajua kiwango cha viburi vyao.

Kifupi tunajisahaulisha kwamba mawaziri, wabunge, DC, DED wote ni wanasiasa, hakuna cha maana toka kwao isipokuwa ajenda za kisiasa(ulaghai).
Si wote, mbona Jerry Slaa hayuko hivyo?
 
Back
Top Bottom