shibela
JF-Expert Member
- Jul 3, 2018
- 1,068
- 3,507
Ilikuwa ni asubuhi na mapema mwezi uliopita, nimeamka ili niende kwenye mihangaiko yangu,ghafla nikasikia tumbo kama linakatwa na kisu Ile shwaaaa!
Nikashtuka nini hiki,nikajikaza hapo nikaendelea kujiandaa,kadri muda ulivyokua unasogea na maumivu nayo yanazidi!
Nikawa sielewielewi shida nini, kadri muda ulivyozidi kusogea maumivu nayo yakawa makali sana upande wa kushoto wa tumbo.
Mtoto wa mama mkwe akaniambia anipeleke hospital nikamwambia hapana aende tu kwenye mishe zake mimi nitaenda mwenyewe (alikua na safari ya kikazi na Mimi sikuchukulia yale maumivu serious kiviiile)aisee ni kama nimejiloga!
Nikatoka ndani vizuri nikawasha ka baby walker huyo hospital, jiani maumivu yakazidi kuwa makali Sana Sana Sana!ikabidi nikatize kwenye kituo kimoja cha afya kiko njiani (hapa nilifanya mistake kubwa).
kufika pale wakanichoma sindano ya kupunguza maumivu,ndo Kwanza yanazidi nikapelekwa ultrasound kwenda kucheck hamna tatizo, nikarudishwa chumba cha mapumziko!
Mle ndani nikawa peke yangu hali ikazidi kuwa mbaya sana, maumivu yakawa ni makali mno,
NIkawa sijiwezi kwa lolote, siwezi ku shout Ile niwaite,siwezi kujisogeza,ghafla nikaanza kupoteza fahamu, nikawa napoteza fahamu baada ya muda nazinduka,muda kidogo nazimia tena, hapo hakuna hata nesi/ daktari anayekuja kuchungulia! Nikajua siku zangu zimeisha! Nilijiona kabisa nakufa peke yangu ndani ya kile chumba!
Baadae nikapoteza fahamu tena nilipozinduka nikaona wamenizingira! Nikawatajia password ya simu,wakampigia mtoto wa mama mkwe alikua safarini, ikabidi ageuze,wakawapigia pia watu wa kazini kwangu,mtoto wa mama mkwe yeye akampigia rafiki Yake aje kutoa Msada akaja!
Kwahiyo akaja rafiki Yake na wafanyakazi wenzangu, wakatafuta Mtu mwingine wa kusoma ultrasound ikaonesha Nina ectopic pregnancy na imeshakua ruptured!
Wakafanya utaratibu hapo,nikahamishwa hospitali Kwa matibabu zaidi!
Ujumbe uliokusudiwa ni kuwa, kama uko na ndugu/ jamaa yuko hospital kama Una nafasi nenda kamuone Pengine anakuhitaji zaidi kuliko wakati mwingine wowote, kama ambavyo wafanyakazi wenzangu pamoja na shemeji yangu walivyonisaidia mimi! Pale kituo cha afya walikua na kazi ya kuniongezea Madrip ya maji tu! Mpka watu wangu walivyofika ndo heka heka zikaanza
ALamsiki!!!