Ndugu, jamaa na marafiki njooni tumtetee Makonda dhidi ya mapapa wauza unga wanaomzushia

Ndugu, jamaa na marafiki njooni tumtetee Makonda dhidi ya mapapa wauza unga wanaomzushia

Unapojiandaa kuwa kiongozi katika Tanzania jitahidi sana usiwe na makandokando vinginevyo utatamani malaika washuke waizime kabisa mitandao ya kijamii!
Umenikumbusha mbali sana "natamani malaika washuke waje wazime mitandao ya kijamii". Huyo aliyesema hivyo alishawahi kusema kuwa yeye hajaribiwi na tunajua asiyejaribiwa ni Mungu tu kwa hiyo alijiita "mungu" halafu akatamani malaika washuke wakati yeye kama "mungu" angeweza tu kuwaamuu malaika washuke waizime hii mitandao yote ya kijamii. Ni kama bwana mmoja anayemiliki shule yake binafsi na akamuajiri mkuu wa shule lakini siku moja akiwa anahutubia katika mkutano akamuinua mkuu wake wa shule aliyemuajiri/mteua kisha akasema anatamani angekuwa mkuu wa shule ili akomeshe wanafunzi wanaopiga kelele darasani. Tanzania ya vi-wonder!
 
Tupo nyuma ya makonda

ajue hivyo, wananchi wengi wako nyuma yake, hata pale kelele za vitisho na uzushi wa uongo unapofanywa

tuko na yeye muda wote
 
Ngoja nimtetee kidogo
Daudi Albert Bashite hajaghushi vyeti bali majina haya{Paul Christian Makonda) ni yake halali aliyapata kihalali kabisa km ifuatavyo

[emoji117] Paul hili jina alipewa Primary kutokana na kipaji chake cha soka wakati akichezea timu ya shule akifananishwa na Paul Scholes
[emoji117] Christian hili jina alipewa na mwalimu wake wa darasa wakati yupo form two maana darasa zima yeye peke yake ndo alikuwa Mkristo
[emoji117] Makonda hili jina alilipata akiwa form 4 alikuwa na rafiki yake ambaye walikuwa wanarudi pamoja Mwanza likizo na kufanya kazi kwenye daladala hivyo shuleni wakawa wanawaita Makonda

Hilo ndo chimbuko la majina yake wala hajaghushi jamani
Umetunga vyema
 
Nimekuelewa sana Paskali. Wakina Lizaboni na wanalumumba wote kwa upunguani wenu tafadhali njooni tumtetee Makonda dhidi ya propaganda chafu zinazoendeshwa na wauza unga wakubwa wa nchi hii akina Chid Benz, Masogange, TID, Wema Sepetu, Mch. Gwajima na Mbowe (Hawa ndio waingiziji, wasambazaji na wauzaji wakubwa wa madawa ya kulevya ambao mtukufu sana "mungu" wa Dsm ameapa kupambana nao na hata ikibidi kufa atakuwa tayari kufa). Hebu tumtetee mtukufu "mungu" wa Dsm kwa kujibu maswali hayo ya ndugu Paskali.
Yes alete majibu tu, ku clear the doubt
 
Pascal na thread za Makonda! Zimekuwa nyingi mno zinazomhusu Makonda! Kuna nini nyuma ya pazia? Yetu macho
 
Mkuu, Umemuelewa vizuri mleta uzi?
Lipi jina lake halali la Mkuu wa Mkoa wa Dar esalaam kati ya haya?
1 Daudi Albert Bashite Kalomije
2.Paul Christian Makonda.

Then tuambie uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa serikali umefanyika/unafanyika kwa haki bila upendeleo?

Pia tuwekee hapa Shule alizosoma huyo Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, kuanzia Shule ya msingi mpaka ya upili(sekondari). Na miaka yake.
Mkuu Koromije (Kolomije) ni jina la kijiji na shule aliyosoma Makonda ............... siyo sehemu ya majina yake!!
 
hivi hii ishu ni ya kujadiliwa na kufunguliwa uzi mpya kila siku? kama ukweli haujulikani mwacheni afanye kazi yake jamani mpaka hapo mtakapopata ukweli ndiyo mje kwenye media. hivi huyu mtu alikuwa anasoma shule nzima mwenyewe? wanafunzi waliokuwa wanasoma hiyo shule hasa wa darasa lake, walimu na hata wafanyakazi wa hiyo shule hakuna mtu mmoja anyejua kuingia kwenye mtandao akatoa ukweli? kila shule ina data za zaidi ya miaka 20 iliyopita japo zipo kwenye hard copy imeshindikana nini kwenda kupata fact na kuja nazo hapa ili ukweli ujulikane? mbaya zaidi wengine ni waandishi wa habari mahiri kabisa wameshindwa kufanya hata huu uchunguzi mdogo kiasi hiki?
 
Ngoja nimtetee kidogo
Daudi Albert Bashite hajaghushi vyeti bali majina haya{Paul Christian Makonda) ni yake halali aliyapata kihalali kabisa km ifuatavyo

[emoji117] Paul hili jina alipewa Primary kutokana na kipaji chake cha soka wakati akichezea timu ya shule akifananishwa na Paul Scholes
[emoji117] Christian hili jina alipewa na mwalimu wake wa darasa wakati yupo form two maana darasa zima yeye peke yake ndo alikuwa Mkristo
[emoji117] Makonda hili jina alilipata akiwa form 4 alikuwa na rafiki yake ambaye walikuwa wanarudi pamoja Mwanza likizo na kufanya kazi kwenye daladala hivyo shuleni wakawa wanawaita Makonda

Hilo ndo chimbuko la majina yake wala hajaghushi jamani
teh teh Tanzania kuna vipaji sana umenichekesha mnoo....daaah unatumia bange ya wapi mwenzangu
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la Mass Mobilization Kuunga Mkono Juhudi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Katika Vita Hii ya Madawa ya Kulevya Kwa Kuwaomba Ndugu, Jamaa na Marafiki, Wanaomjua Makonda Kwa Karibu, Njooni Tujitokeze Kwa Wingi ,Kumtetea Makonda Tunayemfahamu Dhidi ya Uongo na Uzushi Anaozushiwa na Mapapa Wauza Unga Kupitia Kwa Vibaraka Wao Kumsingizia Ameghushi Majina, Amegushi Vyeti, Amesoma Chuo Kikuu Kwa Chati Cha Kughushi na Mpaka Sasa Anatumia Majina ya Kughushi!.

Tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam awaumbue wauza unga wakuu kwa kuwataja majina live, tena bila kupepesa macho wala kumungunya maneno, mafisadi hawa, wapambe wao, makuwadi wa ufisadi na wale wote wasilitakia mema taifa hili, wameanza kampeni ya kumvunja moyo na kumkatisha tamaa Makonda kwa kumzushia kila aina ya uongo.

Sisi tunaounga mkono vita hii, tunamsisitiza akaze uzi na asitetereke, wala asipoteze muda wake wa thamani kujibu uongo wowote wa kwenye mitandao, yeye achape tuu kazi, na majibu ya tuhuma zinazoelekezwa kwake, hazina haja kabisa ya kujibiwa na Makonda mwenyewe bali ndugu zake na marafiki zake wenye nia njema, wanaweza kutusaidia.

Maswali ni haya.
1. Majina matatu ya Mzee Makonda ( baba) ni nani? .
2. Majina matatu ya Makonda (mtoto) aliyoandikishwa Primary pale
3. Alianza Shule ya msingi mwaka gani na kumaliza darasa la 7 mwaka gani? .
4. Baada ya kumaliza la 7 alijiunga na sekondari gani mwaka gani?.
5.Alitumia majina gani matatu sekondari, tukiisha pata tuu majina, tutayaona matokeo yake ya Necta hivyo kuwakata vilimilimi wazushi wote.
6. Alijiunga Mbegani mwaka gani kwa majina gani? .

Majibu ya maswali hayo, yatawakata kabisa vilimilimi wote wanaotaka kumzushia kuwa hakusoma sekondari, alipata Div. 0 na kwamba aliiba cheti cha mtu!.

Ndugu, Jamaa na Marafiki, Tujitokeze Kwa Wingi Kumtetea Makonda Kwenye Vita ya hii ya madawa ya kulevya dhidi ya mapapa wa madawa wanaotaka kumchafua Makonda wetu.

Paskali.
Ha ha ha haaaa ... Hili muvi limefikia patamu ila umeme unakatika katika ... generator nalo bovu zingekua muvi zingine za kihindi ningetoka ukumbini ... ila kwa muvi hili la kibabe ntakesha nasubiri bora mbu waning'ate ila ntasubiri miaka mia ...
 
Haki itamtetea. Makonda hahitaji utetezi wetu. Hata ukiwepo huo ni mdogo sana. Haki na kweli itamtetea.Historia itamtetea. Hata sasa unaona kila kiongozi wa nchi yetu wa ngazi yoyote akisimama anaunga mkono vita hii. Zile kelele zilizokuwepo za kumkatisha tamaa Makonda zimeendelea kupungua. Hata hiyo iliyojitokeza itapungua. Si unaona hata Marekani. Walimbeza sana Obama. Leo amemaliza kazi kweli inamtetea. Uchumi mzuri, ajira imepanda, hata hawataki Trump ajichotee sifa kwa uchumi ulioinuka wanasema "ameukuta Obama kautengeneza."Hivyo ndivyo historia inavyofanya na siyo ile ya muda mrefu tu, hapana ya muda mfupi tu. Ya zama hizi hizi tu. Sizuii mtu kumtetea Makonda. La hasha. Atetewe tu.Ila utetezi wa kudumu wa Makonda ni matokeo ya kuthubutu kwake yanayoonekana hata sasa. Dawa za Kulevya zimepungua mtaani, watumiaji wanajisalimisha kwenye vyombo husika ili kupata msaada, vijana wetu wanaona "mubashara" jinsi madawa ya kulevya yanavyoweza kuua mara moja. Wanajifunza. Punde tutaona watu wengi wakijitolea kuwasaidia watu hawa wapate "rehab'. Serikali nayo itaendelea kuweka mikakati mizito ya kuwasaidia ndugu zetu hawa. Kamishna alidokeza kidogo nia hiyo katika hotuba yake. Mashirika ya dini nayo sasa yataongeza nguvu kuwapokea waathirika hawa na kuwasaidia kimwili na kiroho. Natamani siku ile tutakapoona wale magwiji wa madawa wenyewe wakijisalimisha Polisi kama alivyofanya Pablo japo alijaribu sana kupambana na sheria na haki alijisalimisha tu ili mambo yaishe.
Mkuu umeelewa content ya hilo andiko au umeongozwa na mihemko ktk kuchangia mada?
 
Mimi nilifikiri Paskal unatuletea majibu ya maswali yetu hayo. Sasa unaalika wengine wayajibu wakati na wewe upo upande wake? Ina maana wewe upo upande wa mtu usiyemjua kwa undani? Tupe majibu ya maswali hayo paskal mayala a.k.a njaa.
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la Mass Mobilization Kuunga Mkono Juhudi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Katika Vita Hii ya Madawa ya Kulevya Kwa Kuwaomba Ndugu, Jamaa na Marafiki, Wanaomjua Makonda Kwa Karibu, Njooni Tujitokeze Kwa Wingi ,Kumtetea Makonda Tunayemfahamu Dhidi ya Uongo na Uzushi Anaozushiwa na Mapapa Wauza Unga Kupitia Kwa Vibaraka Wao Kumsingizia Ameghushi Majina, Amegushi Vyeti, Amesoma Chuo Kikuu Kwa Chati Cha Kughushi na Mpaka Sasa Anatumia Majina ya Kughushi!.

Tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam awaumbue wauza unga wakuu kwa kuwataja majina live, tena bila kupepesa macho wala kumungunya maneno, mafisadi hawa, wapambe wao, makuwadi wa ufisadi na wale wote wasilitakia mema taifa hili, wameanza kampeni ya kumvunja moyo na kumkatisha tamaa Makonda kwa kumzushia kila aina ya uongo.

Sisi tunaounga mkono vita hii, tunamsisitiza akaze uzi na asitetereke, wala asipoteze muda wake wa thamani kujibu uongo wowote wa kwenye mitandao, yeye achape tuu kazi, na majibu ya tuhuma zinazoelekezwa kwake, hazina haja kabisa ya kujibiwa na Makonda mwenyewe bali ndugu zake na marafiki zake wenye nia njema, wanaweza kutusaidia.

Maswali ni haya.
1. Majina matatu ya Mzee Makonda ( baba) ni nani? .
2. Majina matatu ya Makonda (mtoto) aliyoandikishwa Primary pale
3. Alianza Shule ya msingi mwaka gani na kumaliza darasa la 7 mwaka gani? .
4. Baada ya kumaliza la 7 alijiunga na sekondari gani mwaka gani?.
5.Alitumia majina gani matatu sekondari, tukiisha pata tuu majina, tutayaona matokeo yake ya Necta hivyo kuwakata vilimilimi wazushi wote.
6. Alijiunga Mbegani mwaka gani kwa majina gani? .

Majibu ya maswali hayo, yatawakata kabisa vilimilimi wote wanaotaka kumzushia kuwa hakusoma sekondari, alipata Div. 0 na kwamba aliiba cheti cha mtu!.

Ndugu, Jamaa na Marafiki, Tujitokeze Kwa Wingi Kumtetea Makonda Kwenye Vita ya hii ya madawa ya kulevya dhidi ya mapapa wa madawa wanaotaka kumchafua Makonda wetu.

Paskali.

Mwambie atii Mamlaka aende tu kuitika wito,mahakamani siyo kama central ambako hapastahili watu kuishi.Asiogope maana ukiamua kubwia Ngada ya MADARAKA bwia tu lakini kumbuka mwisho wa siku,ulipoanzia ndipo utakapoishia.
 
Back
Top Bottom