Ndugu Jumanne Kishimba ni mtu wa aina gani haswa? Mbona ana uwezo mkubwa wa kujenga hoja tofauti na tulivyodhani?

Yule kitano aliyenyooshwa na jiwe vipi bado ana ukorofi ziwani au amekua umri umemtupa.
Kanda ya ziwa palikuwa na matajiri primitives Sana kama kina zakaria waliwachapa bakora abiria waliogoma kushuka kwenye bus walipokatisha ruti,Jiwe akawanyoosha siku hizi wamekua na wamerudi kanisani.
 
Mzee alianza kulangua Zahabu na Almasi miaka ya 80 huko wakati Nyerere na Mzee Rukhsa.

Na inasemekana hana mkono wa birika kwa watu wake wanaomjua.
Watu watoaji hubarikiwa sana
 
Kishimba ajipange vizuri ajue kabisa wimbi la upinzani kuzoa viti vya ubunge 2025 halitamuacha salama ni bora azichange karata zake vizuri ahamie CHADEMA.
 
Ndie muanzilishi wa kuchakata Zahabu kwa njia maludio leaching, kwa wachimbaji wadogowadogo.

Mzee wa Isagehe huyo.

Kabisa na kwa Tanzania haikuepo yeye aliichota zimbabwe na south, japo kwa sasa hadeal tena na dhahabu kama zamani
 

Kilichomkimbiza ni kwa kua alisapoti upinzani, akabambikiwa makodi makubwa kama kawaida ya ccm na enzi hizo alikua mkapa, akatokomea zimland, kikwete kufika zimbabwe akamkuta akamueleza rudi nyumbani, ndio akafungua kwanza imalaseko supermarket Dar posta, baadae akaingia deal na bodi ya pamba akaanza kuingiza mbegu za pamba maana pamba ilikua imekufa, ndio kutoka zimbabwe akaleta issue ya kuchenjua marudio ya dhahabu
 
Ni mwekezaji mkubwa wa apartments Tanzania karibu yote, kila wilaya au mji unaofahamu kuna center nzuri kibiashara lazima kuna estate zake na kwa Tanzania nadhani atakua moja ya watu wenye nyumba nyingi sana
 
Uccm wake ni wa mchongo,alilazimoshwa na akina Mkapa kuingia huko ili biashara zake zisivurugwe
 
Uccm wake ni wa mchongo,alilazimoshwa na akina Mkapa kuingia huko ili biashara zake zisivurugwe

Alikuaga CCM , sasa yeye kishimba, Dani Makanga, john cheyo, shibuda ndio ilikua miamba lake zone, kosa la kishimba ni kuwapa pesa akina Makanga, ndio maana miaka Dani Makanga anatoka UDP anarudi ccm ndio kishimba nae alirudi zake, kwahiyo kusema ni ccm wa mchongo unakua haufahamu siasa za Shinyanga hiyo, hadi mwanza yake miaka hiyo
 
Mzee ana nyumba za kupangisha kwenye Majiji yetu kama Mchele.
 
Mtu yoyote aliyeanza ujana mpaka uzee huo, akiwa mtafutaji wa mtaani na mashambani, anakua anajua maisha halisi karibu kwa 98%,hivyo akiwa Bungeni hoja zake ni zenye nguvu japo wanaojiita wasomi hawawezi kumuelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…