Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 17,047
- 63,206
Mwalimu Nyerere alionya sana tabia za kutumia dini na kabila kwenye kutafuta uongozi wa kisiasa.
Mwalimu alisema, kwenye kipindi kama hiki cha uchaguzi kuna watu hukimbilia kwenye dini na makabila badala ya sera kwenye kusaka uongozi.
Katika miaka mitano iliyopita kumekuwepo na ndoa haramu kati ya baadhi ya viongozi wa dini na utawala wa rais Magufuli ambapo mara kibao ameonekana kutumia taasisi za kidini kisiasa mfano mzuri ni kongamano la juzi hapa la kusifu "juhudi" za awamu ya tano, na pia mara kibao rais Magufuli amekuwa akitumia madhabahu makanisani kutoa hotuba za mwelekeo wa nchi katika masuala mbalimbali.
Pamoja na CCM kudhani kuwa wanaweza kutembelea mbeleko ya dini kwa ajili ya kupata uungwaji mkono kutoka kwa wananchi mbinu hiyo ni upanga wenye makali pande zote na wasipokuwa makini haitowasaidia bali kuwadhuru wao wenyewe.
Katika jumuia za kidini, nikichunguza waungaji mkono wa serikali hii na raisi magufuli kwa kwa nguvu na shauku kubwa zaidi ni viongozi wa taasisi za BAKWATA na wale wa Makanisa ya Kilokole.
Viongozi wa makanisa ya Kilutheri wamekuwa makini sana kutoingia katika mitego ya kutumika kisiasa au kumpa Magufuli endorsement anayojaribu kuipata kutoka kwao.
Kwa upande wa Kanisa Katoliki, wao baada ya kutoa ule waraka wao bora kabisa wa mwaka juzi wameamua kukaa kimya kuwa observers wa situation inavyokwenda, lakini inaonekana rais Magufuli amejaribu kutumia nguvu nyingi sana kuendelea kutafuta uungwaji mkono kutoka kwa kanisa hili ambalo ndilo kanisa lake
Sasa serikali ya CCM ya awamu hii inajaribu kutumia dini kama Strategy ya kisiasa, stratergy ya kutafuta uungwaji mkono kutoka kwa wananchi, Mimi nina mapendekezo yafuatayo kwa Tundu Lissu kuwageuzia kibao CCM kama wataendelea kutumia dini kwenye siasa!
1. Lissu ana advantage kwa sababu yeye na Rais Magufuli wote ni dhehebu moja.
Lissu ni mkatoliki, na raisi Magufuli naye ni mkatoliki. Kwa hiyo naamini kanisa Katoliki haliwezi kuweka nguvu zake kwa upendeleo kwa mmojawapo kati ya hao maana wote ni kondoo wake. Pia siyo rahisi kwa mgombea mmoja kujaribu kutumia kete ya dhehebu lake ili kupata uungwaji kutoka kwa watu wa dhehebu lake!. Sasa nani mnufaika hapa wa siasa za udini? - Hakuna, nani mwenye hasara? Ni Magufuli kwa sababu hatopata nguvu fully kutoka kwa Dhehebu lake kwa sababu litakuwa neutral
2. Kama CCM wataendelea kuleta siasa za kutumia dini basi Lissu azungumzie manung'uniko ya waislamu kwenye utawala huu
Waislamu katika utawala huu wanalalamikia teuzi zenye muelekeo wa udini. Sheikh Ponda majuzi alitoa waraka wenye kuelezea namna teuzi katika awamu hii jinsi zinavyowaweka pembeni waislamu. Kama Lissu ataijengea hoja hii kitu, kwa kutumia vifungu vya katiba vinavyopinga ubaguzi, akaijengea hoja ya kisiasa na kuwachapa nayo CCM hasa katika mikoa yenye waislamu wengi ya pwani na kusini. Amini nakwambia CCM haitokuwa na chao.
Namshauri Lissu asiogope hii ajenda, hii ajenda ni turufu kubwa mno, ni game changer kwenye kupata kura za waislamu nchini. Je kuna sababu ya kuogopa kuwa ni udini kuileta?.
La hasha siyo udini hata kidogo, maana takwimu zipo, na hili jambo huko. nyuma marais kama Mkapa wamewahi kujaribu kuaddress imbalances katika utumishi wa serikali na utumishi, Lakini tofauti ya awamu hii na zilizopita, awamu hii imezidi mno kwenye teuzi zilizokaa kiudiniudini sana. Lissu akilishikia bango hili CCM byebye
3. Lissu aendelee kuwakumbusha viongozi wa dini madhila waliyopitia
Nimemsikia Lissu akizungumzia mateso na manyanyaso waliyopata Masheikh wa Waislamu huko jela, Amezungumzia mateso na manyanyaso aliyopitia Askofu Kakobe kama vile kuhojiwa uraia wake, kupelekewa TRA kuchunguza sadaka!. Mateso, Manyanyaso na kusumbuliwa alikofanyiwa baba Askofu Niwemugizi, Mateso na manyanyaso aliyopitia Askofu Saba. Lissu aendelee kuwasemea hawa, aonyeshe kuwa CCM kujifanya inawapenda na kuwaheshimu viongozi wa dini siyo real, bali inatafuta uungwaji mkono tu wa kisiasa. Na aeleze kuwa wale viongozi wa dini ambao wanaihoji serikali juu ya utendaji wake inawashughulikia. Pia awashukuru viongozi wa dini wanaosimama na kutetea wananchi kweli na haki, viongozi kama Askofu Bagonza, Sheikh Ponda, Askofu Shayo na wengineo ambao wao wanatetea haki
4. Lissu aendelee kuzungumzia muujiza wa uponaji wake.
Hapa awe humble sana, asilitumie jina la Mwenyezi Mungu kisiasa hata kidogo, lakini aendelee kuwa na Shukrani kwa Mwenyezi Mungu mbele ya Umma, Uponaji wake ni muujiza mkuu miongoni mwa miujiza tuliyoishuhudia hapa nchini. CCM ambao wanapenda kulitumia Jina la Mungu kisiasa, kamwe hawatoweza kushinda ukuu wa muujiza huu wa waziwazi ambao tunauona kwa uponyaji wa Lissu. Lissu awakumbushe wananchi, kuwa wale wanaodai kumtumaini Mungu lakini wanaonea watu, hawaheshimu viapo vyao hawakuweza kufanikiwa Azma yao ndiyo maana Leo yeye Lissu yuko hai kwa rehma za Mungu ambaye hao waovu wanajinasibisha naye!.
Kwa hili pekee Lissu atapata uungwaji mkono wa wachaMungu, walokole, waislamu, wakatoliki, walutheri, wasabato, na watu wote wenye kumtumaini Mwenyezi Mungu, maana kwao Lissu kuwa hai leo ni muujiza unaotembea!
Mwisho kabisa niseme kuwa, Kete ya kutumia Dini haiwezi kuisaidia CCM, Na namshauri Lissu awageuzie CCM mzinga kuelekea upande wao wenyewe wakiendelea kutumia kete hii!