Ndugu Mwigulu, kama makusanyo ya Bandari anakusanya DP World, tutakwepaje bankruptcy?

Ndugu Mwigulu, kama makusanyo ya Bandari anakusanya DP World, tutakwepaje bankruptcy?

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
21,625
Reaction score
33,688
Salaam, shalom!!

Ikiwa lango la Nchi, lililo na makusanyo makubwa kuliko yote, tumemkabidhi mgeni atukadirie mapato baada ya Kutoa gharama zake za uendesgaji na ukusanyaji tutakwepaje kuwa bankrupt?

Tuliambiwa kwamba, akiingia DP World, atasaidia kufadhili budget ya nchi yetu zaidi ya 50%

Wananchi Bado tunasubiri hiyo neema Toka Kwa mwekezaji mwarabu wa DP World.

NB: Njia ya mwongo ni fupi!!

Karibuni mnisaidie kupata majibu ya swali hapo juu🙏

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Amen
 
Kwani zile hesabu za TRA zinafanywa na DP world
 
Kwenye hii nchi mwekezaji anapendwa anatokea nchi zenye watu wenye ngozi nyeupe wenye imani kila mtawara alafu mtaji utaupata hapa tz. Nakumbuka prof wa chuo kikuu maneno yake na mwinyi marehemu babu yangu
 
Mm ningependa kufahamu ni ofisi hipi ya ukaguzi wa hesabu za kifedha itakuwa inakagua hesabu za bandari ili tuwe na wakika wa hyo asilimia 50 maana kama watajichagulia wenyewe external auditor uwezekano wakupigwa ni mkubwa.
 
50% itoke wapi wakati bandari mmeiuza? hilo shati la mtumba ulilovaa ambalo ulinunua mnadani huwa unawapa 50% waliokuuzia ?
 
Mm ningependa kufahamu ni ofisi hipi ya ukaguzi wa hesabu za kifedha itakuwa inakagua hesabu za bandari ili tuwe na wakika wa hyo asilimia 50 maana kama watajichagulia wenyewe external auditor uwezekano wakupigwa ni mkubwa.
Ni mapichapicha ndugu,

Practically Hilo Haiwezekani, we angalia DP world kufika tu, gharama ya Kutoa Mzigo bandarini imedouble.

Huko mbeleni, tutawakimbiza Hawa wawekezaji Uchwara!!
 
Back
Top Bottom