Ndugu Mwigulu, VAT ikishushwa Kwa 2%, Serikali haitapata HASARA ya bil 600 Bali itaongeza idadi ya walipa kodi!!!

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
21,625
Reaction score
33,688
Salaam, Shalom!!

Sina ugomvi binafsi na Ndugu Mwigulu, ugomvi wangu ni juu ya Elimu ya Uchumi na maamuzi ya mtu huyu mwenye kibri ajiitaye msomi kuliko wasomi wengine.

HIZI HAPA FAIDA ZA KUPUNGUZA KODI HASA KWA WATU WA KIPATO CHA KATI NA WA KIPATO CHA CHINI.

1. BIASHARA ZILIZOKUFA ZITAFUFUKA.

Kinachoua biashara nyingi na kupunguza idadi ya walipa kodi ni utitiri wa Kodi, kupunguza Kodi, ni kuongeza idadi ya walipa kodi hivyo kimahesabu, kapu litatuna.

2. ITAONDOA NA KUPUNGUZA UKWEPAJI WA KODI.

Kodi himilivu haikimbiwi, na utalipwa Kwa Tabasamu tele usomi.

3. MAPATO NA MAKUSANYO YA KODI YATAONGEZEKA.

Biashara zikiongezeka, mapato yataongezeka sababu ya faida ya wingi.

4. UCHUMI UTAKUA MARA DUFU.

Wingi wa walipajidi lazima utakuza Uchumi.

5. MZUNGUKO WA FEDHA UTAKUA.

Ushiriki wa wengi kwenye Uchumi, utaleta manufaa makubwa.

HITIMISHO.

Aina ya Uchumi unayoenda nayo ndugu Mwigulu, utalipeleka Taifa pabaya, ni maombi yangu mamlaka za juu zikupumzishe Ili tupate changamoto mpya.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿. Amen.

Karibuni 🙏
 
Kwanini jitiada hazifanyiki kuongeza idadi ya walipa kodi?

Kuondoa utitiri wa Kodi ni kupata faida ya namba hivyo hakuna HASARA.

Ni kama tu kwenye biashara, Ukiwa na uhakika wa kupata mauzo makubwa, na mzunguko mkubwa Kwa kupunguza Bei kidogo, HAKIKA HASARA haitokuwepo Bali faida.

Mwigulu apumzishwe🙏
 
Hata Mimi Ile hotuba yake imenishangaza sana Yani tuna viongozi ambao maono Yao ni madogo sana

VAT ilitakiwa ishuke Hadi 10% angeona jinsi database ya walipa Kodi inavyoongezeka

Hivi ajiulizi maswali haya
1) Kwa Nini wafanya biashara wagumu kutoa risiti?

2) Kwanini wanaandika bei pungufu?

Mfanye biashara anatakiwa alipe Kodi huku Kwa hiyari sio Kwa kulazimishwa


Hi nchi mwenye PHD na alioishia darasa la saba wote sawa tu
 
Nch
Nchi gani ya Afrika mashariki in VAT ya 10%
 
Tatizo siyo kushusha viwango, hatuna utamaduni wa kulipa kodi kama nchi Mkuu.

Unafikiri endapo wafanyakazi wangekuwa wanapewa mshahara wote then wao wakalipe kodi badala ya kukatwa Moja kwa moja kama sasa, unadhani wangapi wangepeleka yote?

Tusilee non compliance nchini
 
Ukiwa siyo kiongozi ni rahisi sana kufikiri viongozi wanazingua kwenye haya mambo ya viwango vya kodi.

Rejea bwana Ruto, alivyokuwa anasema kabla ya kuwa Rais na sasa ni kina Ruto tofauti kabisa
 
Ukiwa siyo kiongozi ni rahisi sana kufikiri viongozi wanazingua kwenye haya mambo ya viwango vya kodi.

Rejea bwana Ruto, alivyokuwa anasema kabla ya kuwa Rais na sasa ni kina Ruto tofauti kabisa
Haya mambo ni Rahisi sana,

Kama ambavyo Bei ikipunguzwa wateja huongezeka na kupata faida itokanayo na mzunguko na mauzo, Hivyo hivyo, kupunguza Kodi, Kuna uhusiano mkubwa na kuongeza mzunguko wa pesa na kuongeza mapato nk nk
 
Shida pia wezi wengi ndio maana watu wanaona bora kujifidia tu CAG kila siku analeta madudu ila hakuna anayeshughulikiwa.
 
Hmmm

Suala la kodi na kulipa kodi ni 'fumbo la imani'...

Lina 'Ushetani' zaidi na si umalaika...

Kimoja tu kinachoweza kuondoa 'Ushetani'--UCHUMI MAMA...

Kinachotokea Kenya hata Tanzania kina 'Kimvuli' chake...

Ikiwa tunaweza kutiana nuru, mageuzi bila 'machafuko' yanawezekana... Mageuzi hayafananii kuja na kiongozi yeyote aliyeko madarakani....

Ni wanachi wenyewe, mageuzi yenyewe...

KAMWE yeyote asidanganyike na visomo vya UCHUMI na mashauri ya Uchumi na Kodi kwa ustaarabu na ustawi wa kileo June 2024... Ni mambo ya kulishana 'Matango Pori'... Majibu ya Haki na Amani kupitia Riziki yanahitaji namna ya uchumi unaojiengua na mambo ya 'mikopo na ufadhili'...

HILI LINAWEZEKANA.... Hata kama ni safari ya miaka 25-50...


View: https://www.youtube.com/watch?v=JZor3JLWKLU&t=1480s
Je, huyo mzungu anayezungumzia kuhusu Kodi na Kumeza mitaji ya biashara, Tanzania, anaeleweka?

Kodi na 'kibano chake' vina uhusiano na kulemewa na madeni ya kitaifa na mataifa...

IPO NAMNA YA KULIAMUA HILI... Japo hii inahitaji sana UMMA na VIONGOZI washikane kwa moja--kusimama katika UONO NA UFIKIRIFU MIFUMO kwa umma wote...

Majibu ya 'Utangamano' wa jamii katika riziki, maendeleo na utu bora yapo akilini na mioyoni pa wengi ambao 'Wamejisahau'...
 
Ngoja nirudie kusoma tena.
 
Watawala ni waoga sana kwenye kugusa kodi wao hufikiriaxmatumizi na kuongeza kodi
 
Watawala ni waoga sana kwenye kugusa kodi wao hufikiriaxmatumizi na kuongeza kodi
Hawataki kuambiwa wao wafunge mikanda Kwa kubana matumizi,

Lakini wananchi wa kawaida wanaambiwa wavumilie!!
 
Toa upuuzi wako wewe,weka hapa calculated reversal itakayoonesha walipakodi watakaoongezeka Ili kuziba pengo.

Unajaribu kudanganya nani ikiwa USA kwenye Kodi ndogo Bado watu wanakwepa? Unadhani Kwa Ajili Yako mbovu Kuna mfanyabiashara anapenda kulipa Kodi?
 
Kwamba uwiano wa idadi ya walipa kodi wa Marekani na Tanzania ni sawa!!
 
Kwamba uwiano wa idadi ya walipa kodi wa Marekani na Tanzania ni sawa!!
Wewe kichwa chako ni maji ,weka hapa hesabu zinazoonesha jinsi Serikali itaziba Hilo gap.

USA ni mfano tuu wa wenye Kodi ndogo na watu wanakwepa,hoja ya uwiano Inatoka wapi?

Ndio ujinga huu mumepanga kwenda kuongea eti mnachambua Bajeti ambayo imeshapitishwa? Mna akili kweli nyie Machadema? 😂😂

Mwisho Serikali itapunguza hiyo VAT hatua Kwa hatua pale tuu ikipata chanzo Cha kuziba hiyo gap ,probably next year wataounguza at least 1% na itakuwa hiyo mwaka haid mwaka kadiri uchumi unavyokua.

Unaweza kuziba Gap ya Bil.300 kwa.mwkaa mmja ila sio ya Bilioni 600.
 
Ningekuwa mimi ningeshauri,

Kupata hicho kiasi kinachopungua Serikali iache kununua ma V8.

Kisha ningeshauri safari za nje ya Nchi zifutwe.

Unaweza kuniambia safari Moja ya kiongozi wetu kwenda nje ya Nchi na watu wake ni shilingi ngapi?

Tuanzie hapo.

Tuanzie kwanza kupunguza matumizi ya Serikali.
 
UCHUMI wa kileo unakichochezi cha 'Kuibiana' kwa ajili ya 'kujihami' ama 'kujitengenezea salama'--Haijalishi hili 'linakaushiwa' na wanajamii--iwe wanajamii wenyewe, viongozi, wasomi na jumuiya ya kimataifa...

Kwa hivyo aidha watu waanze kuzungumza kinaga ubaga jinsi ambavyo wao wenyewe wanaweza kukemea na kulaani rushwa; na wasisahau kujinyooshea kidole wao wenyewe: hali yao ya kushiriki kwenye uchumi unaozalisha rushwa bila ukomo -- wanajamii wanaoishi na huu uchumi wao wenyewe kwa kupenda ama kutokupenda; na kama vile 'wamepumbazika'-- hawajui kusema 'Jongoo atupwe na Mjiti wake'...

Wananchi wao wenyewe wanaridhia kuishi kinyonge kwa kukosa ujasiri--na hili likumbushe wananchi wasio jasiri huwa viongozi wasio wajasiri vile vile... Ujasiri wa viongozi wa jamii hii huwa ni viburi, kutishia na 'kuwapanga wananchi'. SI ujasiri wa 'UTU BORA' bali hulka za 'UDHALIMU'.

Wananchi hawapaswi 'kulala'--mambo bado, na mapambano kati ya 'Nuru ya Ufahamu' na 'Udhalimu' katika utu ni 'Jihadi'... Kila mtu yampasa na kupambana na nafsi yake ya kiza na aishinde, ndipo ataweza kuwa 'Simba'; siyo nyau wa kutishia 'wenye madaraka'...

Kenya viongozi wamesahau, wamepuuzia na 'wanachezea shilingi shimoni' na hali 'wamepata kusikia mapema juu ya dosari za ubepari'...

Ubepari ni Ushetani unaweza kujivikaa ngozi ya kondoo--kwa kuwa hili ndilo 'jina la mchezo wenyewe'...

Kwa hivyo mambo ya fedha, benki yanaasili ya 'kuvuruga akili' umma kwa ajili ya haya kudumu kuwepo... Huvutia Viongozi, wa umma na hata dini, wasomi na 'wadanganyika wengine wote'--kalamu na ulimwengu wa watu waliojikataa...

Adha za mitihani ya Kiroho, maadili na miiko kuhusu fedha ni fumbo la imani ndani ya mtu mmoja mmoja.

Ikiwa wengi mtihani huu unawatia 'Kishawishini' basi Fedha ni amana ya Ushetani, na kama ulimwengu wa fedha ni nguo basi Nguo ya Kuazima haistiri maungo ya 'Muungwana'...

Viongozi wanaongia madarakani pasipo kujimulika nafsi zao ili kubaini wanatafuta kuingia madarakano kwa ajili ya utumishi ama matumbo yao--kutafuta umaarufu na kuacha majina; hawa ni 'wadau wa himaya ya Shetani'...

Only fools rush in ... Husema kwa kiingereza wenye busara...

Wananchi wanasahau 'mazuri/mema' ya Mwalimu Nyerere: Wito kilijenga taifa la 'Simba' na siyo 'Kondoo wa Matoleo'... CHAMA CHA MAPINDUZI IMARA ni wananchi wenyewe kuwa ndiyo wenye nchi; kuwa mwenye nchi siyo 'mikato ya kulalamikia serikali kila kukicha'...

Kuwa mwenyenchi ni kusemezana na kusikilizana katika ukweli, maarifa na Ufahamu--siyo porojo, kusemana semana, kuombea 'mabaya' viongozi wadhalimu wafe ama wapinduliwe... Kwa kuwa haya yote pia ni 'Sarakasi za Shetani'...

Hmmmm
 
 
Wewe nimekwambia akili huna , Serikali inatumipa Bilioni 600 kununua V8?

Mwisho napokwambi wewe ni zwazwa uwe unaelewa,jumlisha safari za Marais wote kuanzia Nyerere hadi Samia hiyo pesa haifiki.

Nyie Machadema mnachoweza ni kesi Sidhani kama uchumi mnaujua,jielimishe hapa Kutoka Bungeni, Serikali imesema Itakata OC Kwa 20%,Magari Kwa 50%, Matengenezo Kwa 50%.Itaondoa Kodi kwenye gesi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…