Ndugu naomba ushauri akili imestack

Visanga vyote hivyo Bado tu Halmashauri ya kichwa chako unaomba ushauri!?? .... Huyo mwanamke ni kiboko ..ndio alikutoa ujana wako au kakuroga!?? Visa vyote hivyo bado unataka kwenda kuomba msamaha!??..... La msingi ni elimu ya watoto tu .... Na ole wako umuachie hao watoto hutoamini....
 

Fanya unicheck private nikushauri jambo
 
Jamaa yangu penye ukweli tukuambie:
1. Umeishi na mtoto wa watu tangu 2014 mpaka leo haujawah enda kwao kujitambulisha na kupewa baraka za kuishi naye,na mna watoto wawili halafu hapo hapo unataka kwenye matatizo yenu baba mkwe awe na nguvu ya kusuluhisha?? ndio maana anaishia kukwambia mpandishe basi arudi kwao hapo hujiongezi?

2. Mkuu mwanamke mwizi mpaka leo unamvumilia wa nini? yaani mwanamke akifua nguo na ulisahau hela unaumiza kichwa?

3. Mwanamke ana kiburi ana jeuri na kama ulivyosema lakini bado uko naye, zaidi ya kuwa bikira na hao watoto ni nini kingine imefaidika kwake?
 
Dah hii taarifa imenisikitisha sana, watu wanaeza chukulia poa ila kuona mtu mzima anakosa cha kufanya kwenye mambo binafsi kama hayo inaumiza sana.

Pole sana mkuu naimani utapata suluhisho kwenye changamoto zako.
 
Duuuh, mkuu hapo angalia namna ya kuwapata tu watoto wako, kisha achana na huyo mwanamke asiyejitambua, hapo utaishi kwa furaha maana huyo mwanamke ataendlea kukusumbua mpaka kesho, tafuta mwanamke mwengine mkuu mnyenyekevu, mpole, mchamungu, na anayependa maendeleo
 
Ushauri wangu. Hapo hakuna ndoa. Umefikia kiwango cha kumshikia kisu umchome!!! Ipo siku kama hata kuchoma basi wewe utamchoma kisu.

Cha kufanya mpe talaka. Bora uvunje uanze upya kuliko kuendelea naye.
Masingle mothers wapo ambao waliteleza... mtafute mmoja wao akuongezee heshima kwenye mtaa unaoishi...na malaika pia watakuwa pamoja nawe
 
Hahaha!

Umenikumbusha rafiki yangu mmoja alikosana na mkewe. Mke wake aliondoka na kwenda nyumbani kwao pasipo taarifa mshikaji akakaa kimya!

Wiki ya kwanza holaa mwamba hajapiga simu!

Wiki ya pili holaa mwamba hajapiga simu.

Ukweni wakampigia simu mshikaji hajapokea. Simu ikapigwa kwao ndipo yeye akapokea simu na kwenda ukweni na babu yake.

Kufika huko mwamba akawaambia nyote kuanzia baba mkwe, mama mkwe kuwa wana makosa. Watapokea vipi mke wa mtu pasipo kuwasiliana na mwenye mji.

Jamaa akarudi na mke wake. Kufika nyumbani akamwambia mke wake wazi; tabia ya kudhalilishana siipendi. Tukio kama hili likijirudia tena ukaenda kwenu utabaki kwenu moja kwa moja.

Mpaka leo mke wake katulia.
 
Anampaje talaka na hajamuoa !?? .... Ni kumuacha tu kama walivyovutana kama Bluetooth....
 
Usharogwa na kazi unayo utapoteza Kila kitu utakuwa ombaomba
 
Na kumkuta kote na bkra bado anakufanyia vtimbwiii hvyooo pole mkuu ..
Wajifunze kuna kuoa na kuna kukurupuka ohoo,
Kila mwanamke huzaliwa na bikra,. Na BILA shaka bikra Haina uhusiano na tabia ya mtu. Yani kiburi,. Ubishi, wizi haviwezi kupimwa Kwa bikra! Pole yake na aangalie lilaloridhisha zaidi moyo wake zaid
 
Kati ya wanaume mafala wewe ni mama yao
 
Ukienda utakuwa umethibitisha wewe ni boya wa kiwango cha juu kuwahi kutokea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…