Ndugu Polepole Scandal inaweza kuwa na mwelekeo wa Watergate Scandal ya Washington Post?

Ndugu Polepole Scandal inaweza kuwa na mwelekeo wa Watergate Scandal ya Washington Post?

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2021
Posts
1,322
Reaction score
3,648
Ndugu Polepole ana hekima kubwa sana hata Mimi sina,alianza kuongea kama mwezi umepita kaeleza kwa kina kaonana na wasaidizi wa Rais wote kawaambia yoote,kaonana na Wakurugenzi wa Usalama wa Taifa wote,kawaambia yoote,kamwandikia Mh Rais barua hajapata majibu yoyote na yoote aliyowaambia hayafanyiwi kazi,ndio akasema basi anaacha kazi ili aende akayaongee kwa Watanzania,hapa tulipofika kafuata hatua zote ndio maana mwenyewe anasema viburi vinawasumbua basi ni bora Chama kikapasuka ili kuiokoa Tanzania,hayo ni maneno ya Ndugu Polepole,mwezi mzima alivyokuwa anajielezea watu walimdharau wakamwambia hana lolote la maana,kila siku anasema ipo siku nitaongea kamati kuu ya CCM mtatazamana,watu wakadharau mpaka juzi alipoachia bomu,kwa hiyo hekima yake ni kubwa sana hadi kufikia juzi kuachia lile bomu.

Kama aliyosema Ndugu Polepole,aliwaambia wasaidizi wa Mh Rais na hayakufanyiwa kazi shida ni nini?

Shida tuliyonayo ni ile ile ya kila siku,

1.Jina la Ukoo
2.Ukaribu na Ukoo
3.Rafiki wa Ukoo fulani wenye nguvu.
4.Kuoneana aibu.
5.Kulipa Fadhila.
6.Kuandaa kesho yako.
7.Kuogopa kundi la wana mtandao.
8.kutofuata misingi ya Tanu.
9.Kutofuata miiko ya Uongozi
10.Rushwa na Ufisadi kupewa jina la Takrima.

Ndugu Polepole sio wa kudharauliwa kuna clip anasema alikaa yeye na Rais Magufuli kwa masaa kadhaa akimweleza mambo mbalimbali ya hujuma,hii ishu kama haijachukuliwa kwa uangalifu inakwenda kama ilivyokuwa scandal ya Watergate iliyokuja kumng'oa madarakani Rais Richard Nixon, watu walipuuza lakini wale madogo wawili waandishi wa Washington Post walivyokuwa wanashuka nayo mdogo mdogo kwa hekima kama ya Ndugu Polepole walikuwa hawana haraka hadi Nixon akawa anaweweseka na kuongea na picha za watangulizi wake ndiyo wasaidizi wake wakamwambia basi mzee inatosha achia ofisi kabla hujavua nguo hadharani. Waliosoma kile kitabu "All the presidents men" wanaelewa.

Ukifuatilia scandal ya Watergate kule Marekani utagundua uchaguzi ulifanyika na Republican wakashinda lakini kashfa ilikuja kukomaa miaka miwili baadaye.

Uadilifu ni nguzo muhimu sana kwa kiongozi,tunakumbuka scandal ya rada wakati wa awamu ya tatu iliyoongozwa na Rais Benjamin Mkapa? na ile scandal ya EPA,walikuja kufungwa Daniel Yonah na Mramba baadae sana,tukijifunza hilo tunajua kwamba haya mambo yana tabia ya kulipuka sasa na baadae.

EPA ilianzaga kidogo kidogo watu wakajifanya hawaijui ila baadae ndipo ikawa kashfa kubwa,
 
Waliosoma kile kitabu "All the presidents men" wanaelewa.

TOKA MAKTABA:

Je magazeti, vituo vya televisheni, blogs, online media za Tanzania zimeingia ganzi kuripoti kwa kina Kashfa za INEC & NIDA kutumiwa na CCM aliyobainisha Humphrey Polepole, na pia yale ya wizi wa kushangaza wa laptop 600 kutoka Ofisi ya CCM shina na 7 Msasani Bonde la Mpunga mwezi Mei 2025 na October 2025 tunatiki ?

The Watergates papers,


View: https://m.youtube.com/watch?v=UVrGZSxpBEA
Robert Redford, Bob Woodward, and Carl Bernstein recognized the 35th anniversary of the film All the President's Men at the LBJ Library on April 21, 2011. The three entertained the audience with stories of the steps it took to turn the book about Watergate into a film; they took us behind the scenes of filming; and each discussed the impact the film has today, 35 years after its release

Source : theLBJLibrary


18 April 2020
This is the full testimony of Robert Cushman before the Senate Watergate Committee...


View: https://m.youtube.com/watch?v=oo5d9Z87sXU
 
TOKA MAKTABA :

30 Mei 2025
Wasiojulikana wamevamia ofisi ya CCM, na kuvunja kuiba Laptop 600, fedha milioni 25 kisha kutokomea

1756033375120.jpeg


Chama cha Mapinduzi, shina namba 7, kata ya Msasani
Msasani, Dar es Salaam
Tanzania

Watu wasiojulikana wamevamia, kuvunja na kuiba, Laptop 600, fedha milioni 25, vifaa vya shule pamoja na vya mpira, kwenye ofisi ya Chama cha Mapinduzi, shina namba 7, iliyopo kata ya Msasani eneo la Bonde la Mpunga, wakiwa na gari yenye namba za usajili SM 14024 saa 8:00 usiku.

Akiongea na EATV, Mwenyekiti wa shina hilo, Bakari Mgaza amesema, tukio hilo limetokea Mei 30/2025, wakati viongozi wa shina hilo wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa chama hicho uliokuwa unafanyika jijini Dodoma, ndipo wakapokea taarifa za ofisi yao kuvamiwa majira ya usiku.
 
Ndio ilimuibua FDR huko america!!!

Je yaweza kumleta FDR mwingine huku kwetu!!?

Pole pole ni mtu mkubwa sana lakini ni simple man!very simple huwezi kabisa kudhania!!

KAZI na utu tunasonga mbele!
 
KASHFA YA KOMPYUTA BONDE LA MPUNGA SHINA NA 7 MSASANI, JE OFISI ILIKUWA CENTRAL COMMAND YA UCHAFUZI AU CALL CENTRE YA CHAMA DOLA KONGWE TAWALA ?

 
Tulichokua tunamlalamikia slowslow ni kitendo cha kukipa mida chama chake kifanye mabadiliko wakikaidi ndo atasema --- huu ni mgogoro mkubwa sana
 
Back
Top Bottom