Ndugu wa Hamza washangazwa na uchunguzi wa Polisi

Inside10

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2011
Posts
29,909
Reaction score
32,414
Dar es Salaam. Familia ya Hamza Mohamed aliyewapiga risasi na kuwauwa askari watatu, mlinzi mmoja wa kampuni binafsi na kisha naye kuuawa kwa kupigwa risasi, wameeleza kusikitishwa na taarifa kutoka polisi kuwa ndugu yao alikuwa gaidi.

Akizungumzia uchunguzi wa polisi, jana Alhamisi, Setemba2, 2021 msemaji wa familia ya Hamza, Abdulrahman Hassan amesema wamekuwa wakimuona marehemu akiwa mtu wa kawaida ambaye hakuwa na tabia yoyote ya kigaidi.
‘‘Dah! Sisi tulikuwa tukimuona Hamza kama mtu wa kawaida asiye na mwenendo wa kigaidi, amesema kwa mshtuko.

Kuhusu Hamza kujifunza ugaidi kupitia mitandao, amesema: “Dada….! Hamza anajulikana, watu wamemzungumzia wanavyomfahamu, sisi hatuna cha kuongeza kama polisi wanadai hivyo.’’

Alipoulizwa kama familia inafahamu lolote kuhusiana na viashiria vya ugaidi vinavyodaiwa kuwa Hamza alikuwa navyo, Hassan amesisitiza walikuwa wakimuona Hamza ni mtu wa kawaida na si mwenye nyendo za kigaidi.

Kuhusu Hamza kuishi kisiri huku akiwa amegubikwa na viashiria vyote vya ugaidi na kujifunza mambo mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii, hasa ile ambayo inaonyesha matendo ya Al-Shabab na makundi kama ya ISIS,
msemaji huyo amesema hawezi kuzungumzia chochote juu ya jambo hilo

Maelezo hayo ya Hassan yametokana na taarifa ya polisi iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Camillius Wambura ambaye amesema kwamba uchunguzi wa awali umebaini kuwa Hamza alikuwa gaidi wa kujitoa mhanga.

Chanzo: Mwananchi
 
  1. Dar es Salaam. Familia ya Hamza Mohamed aliyewapiga risasi na kuwauwa askari watatu, mlinzi mmoja wa kampuni binafsi na kisha naye kuuawa kwa kupigwa risasi, wameeleza kusikitishwa na taarifa kutoka polisi kuwa ndugu yao alikuwa gaidi.
Akizungumzia uchunguzi wa polisi, jana Alhamisi, Setemba2, 2021 msemaji wa familia ya Hamza, Abdulrahman Hassan amesema wamekuwa wakimuona marehemu akiwa mtu wa kawaida ambaye hakuwa na tabia yoyote ya kigaidi.

‘‘Dah! Sisi tulikuwa tukimuona Hamza kama mtu wa kawaida asiye na mwenendo wa kigaidi, amesema kwa mshtuko.

Kuhusu Hamza kujifunza ugaidi kupitia mitandao, amesema: “Dada….! Hamza anajulikana, watu wamemzungumzia wanavyomfahamu, sisi hatuna cha kuongeza kama polisi wanadai hivyo.’’

Alipoulizwa kama familia inafahamu lolote kuhusiana na viashiria vya ugaidi vinavyodaiwa kuwa Hamza alikuwa navyo, Hassan amesisitiza walikuwa wakimuona Hamza ni mtu wa kawaida na si mwenye nyendo za kigaidi.

Kuhusu Hamza kuishi kisiri huku akiwa amegubikwa na viashiria vyote vya ugaidi na kujifunza mambo mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii, hasa ile ambayo inaonyesha matendo ya Al-Shabab na makundi kama ya ISIS, msemaji huyo amesema hawezi kuzungumzia chochote juu ya jambo hilo

Maelezo hayo ya Hassan yametokana na taarifa ya polisi iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Camillius Wambura ambaye amesema kwamba uchunguzi wa awali umebaini kuwa Hamza alikuwa gaidi wa kujitoa mhanga.

Hamza aliuawa kwa kupigwa risasi Agosti 25 baada ya kuwaua askari polisi watatu na mlinzi mmoja karibu na Ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es Salaam.

Jana akiwa jijini Mwanza jana, DCI Wambura amesema kuwa uchunguzi wao ulilenga kujua utambulisho wa Hamza, ni nini kilimpa msukumo wa kuua na washirika wake ni akina nani.
DCI Wambura amesema katika uchunguzi huo, polisi waligundua kwamba Hamza aliishi maisha ya kibinafsi sana na viashiria vyote vya ugaidi.

“Kwa muda mrefu, alikuwa akijifunza kupitia mtandao kuhusu shughuli za ugaidi wa Al-Shabab na ISIS,” amesema Wambura.

Amesema Hamza pia alikuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na watu wanaoishi katika nchi ambazo zinakabiliwa na matukio ya ugaidi hivyo kumfanya awe na msimamo mkali.

Credit: mwananchi
 
Tuseme Hamza sio gaidi haina noma!
Kwa nini alimuua askari wa kampuni binafsi ???ya ulinzi
 
Dar es Salaam. Familia ya Hamza Mohamed aliyewapiga risasi na kuwauwa askari watatu, mlinzi mmoja wa kampuni binafsi na kisha naye kuuawa kwa kupigwa risasi, wameeleza kusikitishwa na taarifa kutoka polisi kuwa ndugu yao alikuwa gaidi.

Akizungumzia uchunguzi wa polisi, jana Alhamisi, Setemba2, 2021 msemaji wa familia ya Hamza, Abdulrahman Hassan amesema wamekuwa wakimuona marehemu akiwa mtu wa kawaida ambaye hakuwa na tabia yoyote ya kigaidi.
‘‘Dah! Sisi tulikuwa tukimuona Hamza kama mtu wa kawaida asiye na mwenendo wa kigaidi, amesema kwa mshtuko.

Kuhusu Hamza kujifunza ugaidi kupitia mitandao, amesema: “Dada….! Hamza anajulikana, watu wamemzungumzia wanavyomfahamu, sisi hatuna cha kuongeza kama polisi wanadai hivyo.’’

Alipoulizwa kama familia inafahamu lolote kuhusiana na viashiria vya ugaidi vinavyodaiwa kuwa Hamza alikuwa navyo, Hassan amesisitiza walikuwa wakimuona Hamza ni mtu wa kawaida na si mwenye nyendo za kigaidi.

Kuhusu Hamza kuishi kisiri huku akiwa amegubikwa na viashiria vyote vya ugaidi na kujifunza mambo mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii, hasa ile ambayo inaonyesha matendo ya Al-Shabab na makundi kama ya ISIS,
msemaji huyo amesema hawezi kuzungumzia chochote juu ya jambo hilo

Maelezo hayo ya Hassan yametokana na taarifa ya polisi iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Camillius Wambura ambaye amesema kwamba uchunguzi wa awali umebaini kuwa Hamza alikuwa gaidi wa kujitoa mhanga.

Source: Mwananchi
Hakuna uchunguzi wa kipolisi uliowahi kuja na matokeo ya maana. Ktk msingi wa utawala bora Polisi walitakiwa kujitoa kufanya uchunguzi huo kwa sababu ya kutuhumiwa kumdhurumu marehemu. Matokeo yalitoka kabla ya kuanza uchunguzi pale mkuu wao na vyombo vya habari alipotamka ameuawa gaidi.
 
Kwako kuuliwa askari wa kampuni binafsi ni kigezo cha ugaidi!?
Mimi sipo kwenye ugaidi au kutokua gaidi make hiyo ni siri NZITO kwetu!
"Tatizo langu ni kwa nini aliua askari wa kampuni binafsi "
 
Huo uchunguzi wameufanyia wapi kama hata Ndugu wanashangaa hili hitimisho la Polisi? Maana Kwa maelezo ya hao wanafamilia, inaonesha Polisi hawakwenda kuwahoji wao.. Au Polisi walimuhoji Marehemu akiwa Mochwari?
 
😛😛😛 hivi unaweza ukajifunza kutumia SMG youtube na kwa mara ya kwanza ukaitumia vizuri eh??
haiwezekani lazima itakusumbua.

ndio maana hata marehem aliua kwa kutumia pistol ambayo anaimudu vyema.
 
huyo askari Si alijipendekeza kukoki Bunduki wakamuwai na Shujaa Hamza.Hata ungekuwa we ni Hamza ungemuua tu
tuliza matako,hata hujui kilichotokea unaandika ulivyosimuliwa tu.
 
Hata mbakaji huwa anatetewa Na ndugu Zake sembuse muuaji?
 
Mimi sipo kwenye ugaidi au kutokua gaidi make hiyo ni siri NZITO kwetu!
"Tatizo langu ni kwa nini aliua askari wa kampuni binafsi "
Ni dhahiri Hamza hakulenga kumwua mlinzi wa kampuni binafsi. Mlinzi wa kampuni binafsi aliuawa baada ya kuamua kuwasaidia polisi. Lakini kwa maelezonya abiria waliokuwemo kwenye mabasi, Hamza aliwatuliza raia hao kuwa wasiwe na wasiwasi, yeye anawatafuta polisi. Akasema hataki dhuluma.
 
Hamza hakuwa na viashiria vya ugaidi. Polisi imejitungia ikiamini hakuna wa kuwajibu.
 
Back
Top Bottom