Ndugu wa James wana jimwambafai Dar es Salaam nyumbani kwa ndugu yao

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,438
James ni mtoto wa pekee kuzaliwa, wazazi wake walikuwa fukara mno na uzazi uliwapa shida. Mama yake alipata ujauzito akiwa na miaka 40+ bahati mbaya alifariki akiwa anajifungua. Ndugu walimsaidia baba James kumlea mtoto mpaka alipofika umri wa kwenda shule.

Wakati huo mzee umri umesogea akiwa na miaka takriban 50. James alisoma shule ya msingi na kupata nafasi katika shule ya watoto wenye vipaji kwa kidato cha kwanza. Baba yake alilia kwa furaha pia huzuni ya kuwa hana uwezo wa kumpeleka shule.

James alimuendea Baba Paroko akiomba kazi ya kutunza bustani za kanisa kwani hataweza kuendelea na shule. Baba Paroko alichukua jukumu la kumsomesha James.

Akiwa chuoni alipata bahati ya kufanya internship katika Benki ya Dunia ambako alipata ajira. James amejenga nyumba ya ghorofa ndogo tu ya vyumba vinne vya kulala. Chumba cha wageni kikiwa chini na vyumba vitatu juu kwa ajili yake na watoto wake.

Mzee wake wa miaka 80 ameamua kuishi nae. Amepewa chumba cha wageni. Ndugu 20 wamepanda basi kutoka kijijini kuja kumjulia hali baba James. Wamekuta nyumba ya ghorofa wamepiga simu kijijini kuelezea ufalme wa James.

James akinunua nyama kilo kumi, zote zinachomwa bbq wakati James na mke wako kazini. Vyoo vimeziba kwani ndugu hawa wanabeba toilet rolls kwaajili ya mafua huku wakitumia magazeti ya zamani na maji chooni.

Huu upendo wa ndugu umeleta hasara kubwa kwenye maisha ya James na familia yake.
 
Akiwa chuoni alipata bahati ya kufanya internship katika Benk ya Dunia ambako alipata ajira. James amejenga nyumba ya ghorofa ndogo tu ya vyumba vinne vya kulala. Chumba cha wageni kikiwa chini na vyumba vitatu juu kwa ajili yake na watoto wake.

Mzee wake wa miaka 80 ameamua kuishi nae. Amepewa chumba cha wageni. Ndugu 20 wamepanda basi kutoka kijijini kuja kumjulia hali baba James. Wamekuta nyumba ya ghorofa wamepiga simu kijijini kuelezea ufalme wa James.

James akinunua nyama kilo kumi, zote zinachomwa bbq wakati James na mke wako kazini. Vyoo vimeziba kwani ndugu hawa wanabeba toilet rolls kwaajili ya mafua huku wakitumia magazeti ya zamani na maji chooni.

Huu upendo wa ndugu umeleta hasara kubwa kwenye maisha ya James na familia yake.
Waafrika na mila zetu eehhh...ni shida kwa uhalisia wa maisha ya kisasa, ila yeye na mke wake wakiweka ngumu angalia shida itakayokuja, itakuwa mbaya sana hata si ajabu ndugu wengine watakataa kumzika siku ya siku Bw. James...
 
Katika maisha weka principles zako, asiyeweza kuendana nazo aende. Kwa kifupi hao ndugu ni wanafiki. Baba James angekua kijijini fukara asingetembelewa na ndugu 20.
 
Ujamaa ni maisha yetu. Kufanikiwa kwako ni furaha kwa wengi. Mafanikio yako si yako pekeako, bali ni ya wengi, hivyo Mali zako si zako bali zetu sote tuliochangia mafanikio yako hata Kama ni kukupa 500 ya nauli miaka 26 iliyopita. Na hicho ndio kinachomtafuta bwana James.
 
Kastori kazuri mpaka wote tumekubari kaishie hpa hpa
 
Ukiwaga Night shift unamambo wewe. Muache james na ndugu zake wa kijijini.
 
James ni mtoto wa pekee kuzaliwa, wazazi wake walikuwa fukara mno na uzazi uliwapa shida. Mama yake alipata ujauzito akiwa na miaka 40+ bahati mbaya alifariki akiwa anajifungua. Ndugu walimsaidia baba James kumlea mtoto mpaka alipofika umri wa kwenda shule.

Wakati huo mzee umri umesogea akiwa na miaka takriban 50. James alisoma shule ya msingi na kupata nafasi katika shule ya watoto wenye vipaji kwa kidato cha kwanza. Baba yake alilia kwa furaha pia huzuni ya kuwa hana uwezo wa kumpeleka shule.

James alimuendea Baba Paroko akiomba kazi ya kutunza bustani za kanisa kwani hataweza kuendelea na shule. Baba Paroko alichukua jukumu la kumsomesha James.

Akiwa chuoni alipata bahati ya kufanya internship katika Benki ya Dunia ambako alipata ajira. James amejenga nyumba ya ghorofa ndogo tu ya vyumba vinne vya kulala. Chumba cha wageni kikiwa chini na vyumba vitatu juu kwa ajili yake na watoto wake.

Mzee wake wa miaka 80 ameamua kuishi nae. Amepewa chumba cha wageni. Ndugu 20 wamepanda basi kutoka kijijini kuja kumjulia hali baba James. Wamekuta nyumba ya ghorofa wamepiga simu kijijini kuelezea ufalme wa James.

James akinunua nyama kilo kumi, zote zinachomwa bbq wakati James na mke wako kazini. Vyoo vimeziba kwani ndugu hawa wanabeba toilet rolls kwaajili ya mafua huku wakitumia magazeti ya zamani na maji chooni.

Huu upendo wa ndugu umeleta hasara kubwa kwenye maisha ya James na familia yake.
Nikajua DOTTO JAMES....
 
Pole zake james ana wakati mgumu sana kipindi hichi cha awamu ya 5
 
Haha kwa dar, watu kama James hawapo, watu wanaoishi dar wananyanyapaa ndugu zao wanaoishi mikoani Sky Eclat
 
Back
Top Bottom