Ndugu wa James wana jimwambafai Dar es Salaam nyumbani kwa ndugu yao

Ndugu wa James wana jimwambafai Dar es Salaam nyumbani kwa ndugu yao

Watakua Wasukuma tu hao
James ni mtoto wa pekee kuzaliwa, wazazi wake walikuwa fukara mno na uzazi uliwapa shida. Mama yake alipata ujauzito akiwa na miaka 40+ bahati mbaya alifariki akiwa anajifungua. Ndugu walimsaidia baba James kumlea mtoto mpaka alipofika umri wa kwenda shule.

Wakati huo mzee umri umesogea akiwa na miaka takriban 50. James alisoma shule ya msingi na kupata nafasi katika shule ya watoto wenye vipaji kwa kidato cha kwanza. Baba yake alilia kwa furaha pia huzuni ya kuwa hana uwezo wa kumpeleka shule.

James alimuendea Baba Paroko akiomba kazi ya kutunza bustani za kanisa kwani hataweza kuendelea na shule. Baba Paroko alichukua jukumu la kumsomesha James.

Akiwa chuoni alipata bahati ya kufanya internship katika Benki ya Dunia ambako alipata ajira. James amejenga nyumba ya ghorofa ndogo tu ya vyumba vinne vya kulala. Chumba cha wageni kikiwa chini na vyumba vitatu juu kwa ajili yake na watoto wake.

Mzee wake wa miaka 80 ameamua kuishi nae. Amepewa chumba cha wageni. Ndugu 20 wamepanda basi kutoka kijijini kuja kumjulia hali baba James. Wamekuta nyumba ya ghorofa wamepiga simu kijijini kuelezea ufalme wa James.

James akinunua nyama kilo kumi, zote zinachomwa bbq wakati James na mke wako kazini. Vyoo vimeziba kwani ndugu hawa wanabeba toilet rolls kwaajili ya mafua huku wakitumia magazeti ya zamani na maji chooni.

Huu upendo wa ndugu umeleta hasara kubwa kwenye maisha ya James na familia yake.
 
Huwa sipendagi kukosa bando lakuingia jf Kati ya jumamosi najuma pili maana wafanyakazi wamagufuli huku ndio wanapozimaliziaga stress zao.
 
Back
Top Bottom