Ndugu wagoma kuchukua mwili wa marehemu, washinikiza Jeshi la Polisi kumkamata Mfanyabiashara madini

Ndugu wagoma kuchukua mwili wa marehemu, washinikiza Jeshi la Polisi kumkamata Mfanyabiashara madini

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,284
Reaction score
7,708
Familia ya Marehemu Ediga Mwaniwe wa Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi kwa siku sita imekataa kwenda kuchukua mwili wa ndugu yao kwa ajili maziko uliohifadhiwa katika hospital ya Manispaa hiyo kwa lengo la kushinikiza Jeshi la Polisi Mkoani humo kutenda haki ya kumkamata mfanyabiashara wa madini ambaye wanamtuhumu kufanya mauaji.

Msemaji wa familia hiyo, Charles Mwaniwe amesema mazingira ya kifo cha ndugu yao niya mazingira tata ambapo Jeshi la Polisi linapaswa kumkamata mtuhumiwa na kutenda haki.


=====================​

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KUHUSU TUKIO HILO...

photo_2025-05-03_14-40-26.jpg


TAARIFA KWA UMMA

WATU 07 WASHIKILIWA KWA TUHUMA ZA MAUAJI
​

Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linawashikilia watu saba (07) ambao ni Fredrick Azizi (24) Langula Mbiha (36), Kurwa Alfonce (36), Kashindye Saidi (32) Molah John (35), Joseph Japhet (30) na John Shuli (30) wote wakazi wa kijiji cha Magula kwa tuhuma za mauaji ya Edga Mwanyile, (38) mkazi wa mtaa wa kilimahewa Mpanda baada ya kumshambulia kwa fimbo maeneo mbalimbali ya mwili wake kitendo kilichopelekea kifo chake.

Tukio hilo limetokea Aprili 28, 2025 saa 07:30 mchana huko Magula kata ya Sitalike Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi baada ya marehemu Aprili 27, 2025 kutuhumiwa kuuza madini aina ya dhahabu feki yenye dhamani ya Tsh 570,000/= (laki tano na elfu sabini) katika ofisi ya Robart Benedict iliyopo kijiji cha Magula.

Siku ya tukio marehemu alirudi tena kuuza dhahabu ofisini pale ndipo mnunuzi alimgundua kuwa ni yule ambae aliuza dhahabu feki. Marehemu baada ya kuona kuwa ametambuliwa alitupa nje dhahabu alizokuwa nazo ndio mzozo ulianza baina yao na kundi kubwa la watu lilijitokeza na kuanza kumshambulia maeneo mbalimbali ya mwili wake.

Mmiliki wa ofisi hiyo anaetambulika kwa jina la Robart Benedict alifika katika eneo hilo na kumkuta ndugu Edga Mwanyile akiwa anashambuliwa ambapo alimchukua mpaka katika kituo cha Polisi kati Mpanda. Mhanga alipelekwa Hospitali ya Manispaa Mpanda kwa matibabu ndipo alifariki dunia.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linatoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na badala yake wawasilishe changamoto zao kwa mamlaka husika kwa ajili ya ufumbuzi.

IMETOLEWA NA:-

Kamanda wa Polisi

Mkoa wa Katavi.
 
Hii ni balaa, mauwaji nchi hii yameshamili sana jamani,Ni muhimu Kwa Jeshi la Polisi kuchukua hatua kali
 
Back
Top Bottom