Dr wa Manesi
JF-Expert Member
- Aug 19, 2024
- 6,479
- 4,974
Naona vibwebwe vimefungwa viunoni watu (wamakonde wanaita 'vanu') wakifurahia ugomvi wa jirani...........wanagongeana mikono Huku wakishusha vijineno chochezi ("ndo alivyo huyo!", "apigwe huyo!" n.k) na vicheko (wera wera weraaaaa!!) kama vyote.
Katikati ya 'raha' hii ya kushuhudia ugomvi wa hawa ndugu, majirani, bila kutarajia, wanajikuta wanasahau yao; wanaoenda kulima wanachelewa Huku wakiwa hawajui hata vifaa wameweka wapi maana walivitupa wakati wa kushangilia na kurukaruka. Wanaoenda maofisini nao wanachelewa Huku wakijikuta wamepoteza nyaraka kadhaa wakati wa 'mzuka' wa kushangilia ugomvi huo wa ndugu. Wengine hawatoviona tena vifaa vyao (wajanja watatoka navyo mbio) Huku wengine watakuja kuviona muda ukiwa umeshapita na vikiwa vimeshadukuliwa tayari na wajanja walioviokota.
Ndugu ni ndugu, wenyewe wanasema damu nzito kuliko maji hivyo ghafla bin vuu unaweza kukuta wamepatana na kuungana kwa nguvu zaidi ya jana Huku wakiwashangaa na kuwacheka na kuwazodoa nyie majirani mliokuwa mnashadadia msilolijua asili yake. Na hapo ndipo usemi wa wahenga, "ndugu wakigombana we chukua jembe ukalime" unaleta maana.
Ila watoto wa 2000 ni wabishi sana....wajuaji (lakini wasiojua), viburi (lakini wanaopigika makofi vizuri tu) na vidomodomo sana (lakini wasio na akili). Wanajitia kupuuza ushauri huo wa wahenga na Sasa wako bize tena kuushadadia na eti kuuchambua ugomvi wa wanandugu hawa wa Toka uhuru kwa Imani kwamba wanaweza kuwafarakanisha mazima....... thubutuuuuuuuu😏😏😏😏 (ningekuwa mhuni ningesema, 'manfi yao wenyewee'.