Ndugu wana lawama sana

Kuna mahali umeandika " NIKAMPA MTAJI ". sasa kama mtaji ulimpa hata faida nayo niyakwake sema umemnyang'anya faida na mtaji...

Maelezo yako tuu yameshakufunga hata akikusema ni sawa.

Ungesema nilimkopa mtaji na kisha nikachukua na riba yangu...
Kiongozi wataka tuelezane neno Kwa neno, ukisoma hicho kifungu Cha maneno huwez kupata picha kuwa nimemaanisha Nini?

Sa Nilimkopa mtaji ndo Nini? Emu nenda kwenye mada bhana acha kukompliketisha mambo.

Wewe hujaelewa au unataka ubishi tu? Makubaliano yalikuwa nimpe mtaji afanyie kazi, sio nimkopeshe
 
Hivi kuumpa mtu mtaji maana yake nini? Pengine mimi mgumu kuelewa mambo madogo
 
Makubaliano Yenu Yalikuaje Kwani?Mara ya Kwanza Faida Kiduchu Mkagawana Nusu Kwa Nusu Hukuona Ubaya Wa Ndugu,,,Mara ya Pili Mambo Yameenda Poa Ukakiuka Makubaliano ya Nusu Kwa Nusu,,Ndugu amekuwa mbaya.
Ilikuwa ni ela ndogo saana, nikampa tu ili aweze kununua Walau chochote.. hii Sasa hivi imekuja Hiyo nikaona huko kiasi kinatosha kabsa Kwa yy kutokana na kazi aliyofanya
 
Na hawo watu baki ufanye nao makubaliano kwa maandishi tofauti na hapo watapita na mtaji wenyewe
 
Bado kuna misscall, zaidi ya 10 kila siku na sio kuuliza angalau mwili wako utakuja lini tuupokee.
Kizinga tena🥲
Mimi wakinipigiaga naliaga kama mbuzi meeeh meeeh meeh na sauti ya kujamba mbrrrr mbrrr kuwakatisha tamaa wasinisumbue lakini waapii yani mfulululizo wa mzinga ya hataree.

Magonjwa Mtambuka 😡 Chaliifrancisco (uumbwaaa)

Nyau de adriz
 
Hizo biashara za nusu kwa nusu,mnawezaje? Fanya biashara yako mwenyewe biashara za kushirikisha watu kwa miadi ya kugawana faida ni kirusi kinachokuwa taratibu.
 
ukipewa lift hutakiwi kulalamikia spidi ya gari

sioni mahali dogo kaonewa

dogo hajui unyenyekevu
Ahadi deni
Ukihaidi kuwa utamlipa nusu ya faida, timiza ahadi

Ndio mana walivyopata kidogo, dogo hakulalamika

Jamaa kapata tamaa alipopata pakubwa

Sasa dogo anafidia kidogo alichopata last time kwa kazi kubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…